Skip to main content

Posts

Showing posts from April 18, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tume ya Madini Morogoro ,Fadev, na Undp .Wawapiga Msasa Wachimbaji Wadogo

Tume ya Madini kwa ushirikiano wa  Shirika la Maendeleo ya Umoja wa  Mataifa (UNDP) pamoja na Taasisi ya kuendeleza Uchimbaji Mdogo (FADev) wameendelea kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika Mkoa wa Morogoro ikiwa ni Mkakati wa serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo Mradi unaofadhiriwa na UNDP.  Akiongea na Wachimbaji wa madini ujenzi katika Mkoa wa Morogoro Afisa Program kutoka FADev  Bi Rehema Mkuli amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga wachimbaji wadogo wanaojihusisha na madini ya ujenzi na viwanda, hususani madini ya kokoto kwa lengo la kuboresha uelewa wao wa kitaalamu na kuhamasisha mbinu salama na zenye tija katika shughuli za uchimbaji. Pia Bi Rehema amesema wachimbaji hao wanajifunza juu ya mbinu za Msingi za Uchoraji wa Ramani za Kijiolojia (Basic Geological Mapping), Usanifu salama na bora wa mashimo (Safe and Efficient Pit Design) Aidha Kwa upande wa wakufunzi kutoka ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro  Mjiolojia Asifiwe  Waksoni Ng...

Sitovumilia Mwalimu Kuonewa Au Kutotendewa Haki - Prof. Shemdoe

Na OWM - TAMISEMI, Bahi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema iwapo atapewa taarifa ya uhakika ya afisa yeyote anayepaswa kuwahudumia walimu na kutatua kero zao, kwamba amemuonea au kutomtendea haki mwalimu yeyote hatosita kumuondoa katika cheo alichonacho. Prof. Shemdoe ametoa tahadhari hiyo Aprili 17, 2026 akiwa wilayani Bahi, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa darasa la nne, saba, kidato cha pili na cha nne wa wilaya ya Bahi, iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Chiona wilayani humo. “Tutatue kero za walimu kwa wakati, nitakuwa mkali na sitomfumbia macho afisa yeyote wa idara ya elimu atakayemuonea au kutomtendea haki mwalimu, nitachua hatua ya kumuondolea cheo alichonacho  kwani atakuwa ameugusa moyo wangu,” amesisitiza Prof. Shemdoe. Prof. Shemdoe ameanisha kuwa, kuna maeneo yana changamoto ya kuwahudumia walimu akitoa mfa...

Silent Ocean Yaahidi Kuendelea Kudhamini Bunge Marathon Kwa Miaka Mitano Zaidi

KAMPUNI  ya kimataifa ya usafirishaji wa mizigo ya Silent Ocean, maarufu kama “Simba wa Bahari”, imetangaza kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa Bunge Marathon kwa kipindi cha miaka mitano zaidi, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi na kulinda afya zao. Akizungumza leo Aprili 18, 2026 katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma wakati wa mbio hizo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Ndg. Mohammed Soloka, amesema Kampuni hiyo imejipanga kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu na Serikali pamoja na jamii katika nyanja mbalimbali za maendeleo. “Tutaendelea kuwa sehemu ya Serikali yetu kwa kushirikiana katika kuimarisha huduma kwa jamii na kuhakikisha wananchi wanapata elimu na huduma bora kupitia kampuni ya Silent Ocean,” amesema Soloka. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, ameipongeza kampuni hiyo kwa mchango wake mkubwa uliowezesha mafanikio ya Bunge Marathon msimu wa tatu, akieleza ku...

Waziri Mkuu Apongeza Mchango wa Wanawake Ukuaji wa Uchumi

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewapongeza wanawake nchini kutokana na mchango mkubwa wanaoutoa katika kukuza uchumi uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla. Amesema kuwa zaidi ya asilimia 50 ya biashara ndogo na za kati zinamilikiwa na wanawake hivyo inaonesha wazi kuwa injini ya uchumi wa Taifa inaendeshwa kwa kiasi kikubwa na wanawake.  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 18, 2026) katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Mkutano wa Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (SMEs) na Maonesho ya Uwekezaji na Biashara yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Four Season jijini Arusha. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kusisitiza kuwa uchumi jumuishi huchochea amani na mshikamano katika jamii kwa sababu kitendo cha ushirikiano wa pamoja kinawezesha kubadilisha hali ya uchumi na kufikia maendeleo jumuishi kwa wote. “Tunapaswa kujenga uchumi jumuishi unaohusisha makundi yote ya jamii, kwa upande wetu  Serikali tutahakikisha ajenda hii inatekelezwa kwa vi...