Skip to main content

Posts

Showing posts from January 27, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Akutana na Frederick Sumaye

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 28, 2026 amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.

Waziri Kijaji Ampokea Braydon Bent

📍Atimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kuitembelea Tanzania  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amempokea shabiki mashuhuri wa klabu ya Manchester City ya Uingereza Braydon Bent ambaye ametimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kuitembelea Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali ikiwemo Serengeti na Mlima Kilimanjaro.  Ni kama safari iliyochukua karne hivi ya kutoka  tu Etihad Stdium hadi Serengeti! Shabiki huyo mtopezi wa Manchester City anasifika kwa kurekodi video akiongea Kiswahili na alipata kuahidiwa kuja Tanzania tangu mwaka 2020.  Leo, hatimaye, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi wametimiza ndoto ya shabiki huyo ambaye amepata pia kuwahoji mastaa kama Neymar, Aguero, Kocha Pep Guadiola na sasa akiwa mtangazaji wa mechi za Man City na pia akiwa na vipindi Sky News.  “Ilikuwa ndoto yangu kubwa kufika nchi hii nzuri. Kwa mapokezi haya naona kabisa tayari safari yangu imeanza ...

NIRC Yaimarisha Utunzaji wa Mazingira Kupitia Upandaji Miti Skimu ya Hombolo

📍 Hombolo, Dodoma KATIKA kuadhimisha siku ya kumbukizi ya kuzaliwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,rai imetolewa kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), kuendelea kutoa elimu kwa wakulima na jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa wito huo ameutoa leo Aprili 27, mkoani Dodoma wakati wa zoezi la upandaji miti katika Skimu ya Umwagiliaji Hombolo, lililoendeshwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Senyamule amesisitiza matumizi endelevu ya rasilimali za maji, na usimamizi shirikishi wa miundombinu ya umwagiliaji, ili kuongeza ufanisi na uimara wa miradi hii. "Serikali ya Mkoa wa Dodoma itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji pamoja na wadau wote wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa miradi ya umwagiliaji inatekelezwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na misingi bora ya uhifadhi wa mazingira, sambamba na kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla. Senyamule amewahimiza wananchi wote kushiriki kikamilifu kat...

Nemc Yapanda Miti Kumuunga Mkono Rais Samia

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan, za kuhifadhi na kusimamia mazingira kwa kushiriki zoezi la upandaji miti katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa. Hafla ya NEMC kupanda miti ilifanyika jana Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo viongozi kadhaa walihudhuria hafla hiyo. Katika kuadhimisha siku hiyo, Rais alipanda mti kama ishara ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira, ikiwa ni utekelezaji wa kaulimbiu isemayo “Uzalendo ni kutunza mazingira, shiriki kupanda miti.” Kupitia kanda zake 13 nchini kote, NEMC imeshirikiana na wizara, taasisi za umma na binafsi, asasi za kiraia pamoja na kamati za mazingira kushiriki katika zoezi la upandaji miti katika maeneo mbalimbali zikiwemo shule, zahanati na katika masoko. Akizungumza katika hafla hiyo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa  Utawala na Fedh,  Dickson Mjinja alieleza umuhimu wa kupanda miti kama njia mojawapo ya kukabiliana na a...

Dk. Samia Amepanda Mti Wenye Tafsiri Pana Kwa Taifa

Na. Habibu Mchange:  *_Muembe alioupanda unasimama kama ishara ya uongozi unaoamini katika mizizi ya umoja, shina la mshikamano, na matawi ya amani na mashirikiano yanayowafikia Watanzania wote* _* Katika picha yenye nguvu ya historia na ujumbe mzito kwa taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameichagua ardhi badala ya jukwaa, mti badala ya sherehe, na vitendo badala ya maneno, kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa tarehe 27 Januari, 2026.  Akiwa katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja, Rais Samia alipanda mti wa Muembe (Mangifera indica) tendo lililobeba maana pana kuliko tukio lenyewe. *Hapa ndipo tafakuri ya taifa inaanza*.  Kitafakuri hiki hakikuwa kitendo cha mazingira pekee, kilikuwa kitendo cha kuunganisha Taifa. Kama mizizi ya mti inavyojipenyeza ardhini na kuishikilia, ndivyo kitendo hiki kinavyoikumbatia Tanzania nzima Bara na Zanzibar, vizazi vya jana, leo na kesho katika wazo moja kuu, kwamba mustakabali wa nchi hujeng...

Serikali Kuendelea Kufanya Mageuzi Ya Sera– Dkt. Mwigulu*

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kufanya mageuzi ya sera zinazogusa moja kwa moja maslahi na ustawi wa maisha ya wananchi.  Amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia watendaji wa Serikali wanaotoa visingizio, wasiowajibika na wenye hulka ya kufanya kazi kwa mazoea, ujanja ujanja na kutoa taarifa za michakato badala ya majibu yanayotakiwa. Amesema hayo Bungeni leo (Jumanne, Januari 27, 2026) wakati akitoa hoja ya kujadili hotuba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa jijini Dodoma wakati akizindua Bunge la 13 Novemba 14, 2025. “Tunapozungumzia utendaji Serikalini, msisitizo ni uadilifu na uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi waliotuchagua ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali za nchi pamoja na kupata huduma wanazostahili.” Dkt. Mwigulu amesema kuwa hotuba aliyoitoa Rais Dkt. Samia ilitoa mwelekeo na dira ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha pili. “Hotuba ya Mheshimiwa Rais ilitoa maelekezo na kubainisha changamoto pamoja n...