▪️Ni kupitia Local Content ▪️ Yatenga Huduma na Bidhaa 20 kwa ajili ya Kampuni za kitanzania pekee* ▪️ Watanzania wanufaika asilimia 86 ya manunuzi ya bidhaa na huduma migodini* ▪️ Ajira 20,421 zalizalishwa, Watanzania wachukua asilimia 94 *📍DODOMA* Serikali imeendelea kufanya maboresho katika Sheria na Kanuni za Madini kwa lengo la kuongeza ushiriki wa Watanzania katika sekta ya madini, hususan katika utoaji wa huduma, usambazaji wa bidhaa na upatikanaji wa ajira migodini. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Agosti 14, 2026 Bungeni jijini Dodoma waliotaka kujua ni namna gani Serikali imejipanga kutekeleza mpango wa Uwajibikaji wa Wamiliki wa Leseni kwa Jamii na Ushirikishwaji wa Watanzania katika Uchumi wa Madini. Amesema kuwa, kupitia Tume ya Madini, Serikali imetenga bidhaa na huduma 20 zinazopaswa kusambazwa na kutolewa na Watanzania au kampuni zinazomilikiwa na Watanz...
Marato tv - Sauti ya Jamii