Skip to main content

Posts

Showing posts from October 2, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri mkuu kufungua mkutano wa wadau wa lishe Tanzania

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 03, 2024 anafunga mkutano wa Kumi wa Wadau wa Lishe unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Malaika Beach Resort, Jijini Mwanza. lengo la Mkutano huo ni kudumisha dhamira ya pamoja ya Serikali na wadau katika kuongeza msukumo na uwekezaji katika kutekeleza Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe ili kukabiliana na changamoto za utapiamlo katika jamii, na kupokea tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe nchini kwa mwaka uliopita. Pia, Mkutano huo umelenga kutoa fursa kwa wadau wa lishe kukutana, kujadiliana na kupata maelezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Kitaifa wa Lishe (2021/22 - 2025/26) uliouzinduliwa mwaka 2021. Kaulimbiu ya mkutano huo ni *”Kuchagiza Mchango Zaidi Wa Wadau Wa Kisekta Ili Kudumisha Matokeo Bora Ya Hali Ya Lishe Nchini Tanzania”.*

Waziri Bashe Azindua Kiwanda Cha Kubangua Korosho Mtwara

Na Elizabeth Cornely WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe, amezindua kiwanda cha kubangua korosho Newala mkoani Mtwara. Kwa mujibu wa Bashe, kiwanda hicho kimegharimu Sh.bilioni 3.4. Chama Kikuu cha Ushirikia cha TANECU  kimeanza safari ya kuwa na ushirikia imara kwa kujenga kiwanda cha kubangua korosho Newala, mkoani Mtwara. Bashe ambaye yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi, amekipongeza TANECU kwa kuwa mfano mzuri wa kuonesha ushirika unaozidi kuwa imara kwa kuhakikisha uwekezaji huo wa kiwanda ni wa wakulima wenyewe.  Pia, alielekeza kijengwe kiwanda kingine kama hicho Tandahimba na kiwe tayari msimu ujao. Kiwanda hicho cha kubangua korosho kilichozinduliwa, kina uwezo wa kubangua tani 3,500 kwa mwaka na kwamba mkakati ni kuwa na viwanda 20 vya Kubangua Korosho chini ya TANECU katika Mkoa wa Mtwara ambapo 10 vitajengwa Newala na 10 vingine vitajengwa Tandahimba.

Mbunge Esther Matiko amwaga misaada ya mamilioni Tarime Mjini

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe Esther Matiko ameendelea na ziara yake ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa kufika Shule ya Sekondari Tagota na kuzungumza na Walimu na Wanafunzi wa Shule hiyo. Akiwa Shuleni hapo kupitia taasisi ya Matiko Foundation,Mhe Esther Matiko amekabidhi Tank la Maji Lita 5,000 lenye thamani ya Tsh 1,350,000/= kwa ajili ya uvunaji wa maji yatakayotumiwa na Walimu na Wanafunzi wa Shule hiyo.  Mhe Esther Matiko ameweza pia kutoa vifaa vya michezo kwa wanafunzi wa Shule hiyo kupitia taasisi ya Matiko Foundation ambavyo ni Mipira Pete na Mguu na Jezi Mpira wa Pete na Miguu vyenye thamani ya Tsh 850,000/= Akipokea changamoto za Walimu shuleni hapo kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Shule Mwl Nulu Mwalukasa be amemueleza Mhe Matiko Shule hiyo haina jengo la utawala jambo ambalo linaleta usumbufu kwa walimu. Mhe Esther Matiko ameahidi kwenda kuliwakilisha bungeni suala hilo kwani ukosefu wa jengo la utawala limeonekana kuwa changamoto kubwa kwa Shule za Wilaya ya...

Mbunge Mathayo atembelea vijiwe vya bodaboda na kumwaga pikipiki za mikopo nafuu

Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amekutana na waendesha pikipiki za abiria " bodaboda" na kuwakumbusha ahadi yake ya mkopo nafuu wa pikipiki. Akizungumza na uongozi wa wasafirishaji hao pamoja na baadhi ya waendeshaji leo oktoba 2 amesema fursa bado ipo na ametoa siku 30 kupata pikipiki kwa wale watakaokamilisha taratibu. Amesema alipokuwa akikabidhi vyeti baada ya mafunzo ya udereva chuo cha Veta Musoma aliahidi kudhamini mkopo wa pikipiki kwa kianzio cha shilingi laki 3 kutoka benki ya Azania lakini muitikio umekuwa mdogo. Mathayo amesema dhamana aliyoiomba Azania ni ya pikipiki 200 lakini ni zaidi ya miezi 2 ni watu 2 tu ambao wametimiza masharti. Amesema kwenye masomo ya udereva aliyoyafadhili yalikuwa na muitikio mkubwa lakini kwenye kupata pikipiki kwa mkopo nafuu kumekuwa na kusuasua. " Ndugu zangu tunajikwamisha wenyewe kupata fursa zilizopo kutokana na kuto kuzingatia utaratibu. " Tulikubaliana kuwa kwenye vikundi vya...

Watatu mbaroni Masasi kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya million 139 za ushirika

 Na Mwandishi Wetu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ametoa saa 24 kwa kampuni ya RV inayonunua mazao Masasi mkoani  Lindi kulipa madeni ya wakulima. Akizungumza katika muendelezo wa ziara yake mkoani mtwara,Waziri Bashe ameelekeza kampuni ya RV ambayo ilishiriki mnada wa mbaazi kuhakikisha inalipa wakulima pesa ndani ya saa 24. Bashe pia ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwashikilia viongozi wastaafu wa ushirika kwa tuhuma za kuhusika na ubadhirifu wa zaidi ya sh.milioni 139. Agizo hilo amelitoa kufuatia malalamiko ya wakulima kuhusu kucheleweshewa malipo yao na Kampuni hiyo ya RV.   Hali kadhalika ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwashikilia waliokuwa watendaji wa vyama vya ushirika Hashim na Yusuph Mataula kutokana na tuhuma mbalimbali zaubadhirifu wa fedha za wakulima. “Hawa kwa kuwa wamekiri, watatusaidia kujua wenzao waliotafuna fedha za wakulima ni lazima fedha hizi za wanyonge zirudi, haiwezekani mtu anapiga fedha katika ushirika anakimbilia katika ...

Ifikapo 2030 korosho zote zitabanguliwa nchini-Ba

Na NIRC, Mtwara Waziri wa kilimo Hussein Bashe, (Mb) amesema ujenzi wa Kongani ya Viwanda Maranje Newala mkoani Mtwara unalenga kuhakikisha ifikapo 2030, korosho zote zinabanguliwa nchini. Amesema, lengo ni kuhakikisha wakulima hawauzi korosho ghafi nje ya nchi. Bashe amesema hayo katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Mtwara, wakati akizindua kiwanda cha kubangua Korosho cha TANECU kilichopo katika kijiji cha Mmovo, kata ya Kitangali Halmashauri ya Newala mkoani Mtwara Amesema, kiwanda hicho kilicho gharimu zaidi ya sh. Bilioni 3.4 kimelenga kufungua milango ya ujenzi wa mradi wa kongani ya viwanda Newala ambapo hadi kufikia mwaka 2030 korosho zote zitabanguliwa nchini. Kiwanda hicho ni moja kati ya viwanda/Kongani kumi vitakavyojengwa katika eneo lenye mita za mraba 99,000.  Uwezo wa kiwanda kimoja ni kubangua tani 3,500 za korosho ghafi kwa mwaka. Ametumia fursa hiyo kuutaka Ushirika nchini kubadili mfumo wake wa uendeshaji na kuzingatia mahitaji ya wakulima. Waziri Bashe amesem...