Skip to main content

Posts

Showing posts from September 1, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

JWTZ LATAJA MCHANGO WA MIAKA 62, LAVUTIA USHIRIKIANO WA MAJESHI YA EAC KATIKA KUWA HUDUMIA WANANCHI

 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeadhimisha miaka 62 tangu kuanzishwa kwake Septemba 1, 1964, huku maadhimisho hayo yakifanyika sambamba na kufungwa kwa Wiki ya Sita ya Ushirikiano wa Kijeshi na Kiraia ya Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Viwanja vya Gofu vya Lugalo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Jacob John Mkunda, amesema historia ya JWTZ imejengwa kupitia utekelezaji wa majukumu ya kulinda taifa pamoja na kushiriki katika shughuli zinazogusa maisha ya wananchi. Jenerali Mkunda amesema JWTZ limeendelea kuimarisha uwezo wa askari wake ili kukabiliana na majukumu mbalimbali ya kitaifa, huku misingi ya uzalendo, weledi na uwajibikaji ikiendelea kuwa sehemu ya utendaji wa jeshi hilo. Kwa mujibu wa Jenerali Mkunda, maadhimisho hayo yamekuja wakati ambapo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaendelea kutafuta njia za kuongeza ushirikiano wa majeshi yao, si katika masuala ya kijeshi...

MWENGE WA UHURU WAPONGEZA MRADI WA VIJANA WA VIZIMBA VYA SAMAKI HALMASHAURI YA BUKOBA

 Na Angela Sebastian, Bukoba MWENGE wa Uhuru mwaka 2026 umekagua na kupongeza mradi wa vijana 47 wanaojishughulisha na ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba, unaotekelezwa na vikundi saba katika Kata ya Kemondo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.  Mradi huo upo chini ya programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT-Uvuvi), inayolenga kuwawezesha vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi kupitia sekta za kilimo, mifugo na uvuvi. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, Wazo Mwang’onda, alimpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuwawezesha vijana kupitia miradi ya kiuchumi, huku akiipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.  Alisema Serikali imeendelea kuhakikisha vikundi vinavyonufaika vinapatiwa nyenzo za kazi, mafunzo kwa vitendo, mikopo yenye masharti nafuu pamoja na pembejeo zinazohitajika katika shughuli za uvuvi na ufugaji wa samaki. “Tumeukagua mradi huu na kuona kuwa ni mzuri,...

BEI ZA MAFUTA SEPTEMBA ZASHUKA NCHINI*

 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za bidhaa za mafuta kwa mwezi Septemba 2026. Bei ya petroli imeshuka kwa Shilingi 102 kwa lita, huku bei ya dizeli ikishuka kwa Shilingi 101 kwa lita. Bei hizo zitaanza kutumika kuanzia tarehe 2 Septemba 2026, saa 6:01 usiku. EWURA inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia, ambapo mabadiliko ya bei yanaendelea kuathiriwa pamoja na mambo mengine na hali ya kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati. Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015, bei za mafuta zinaendelea kupangwa kwa kuzingatia mfumo wa soko. Wafanyabiashara wote wa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zisizozidi bei elekezi, na wananchi wanashauriwa kutoa taarifa EWURA kwa kituo chochote cha mafuta kitakachouza zaidi ya bei elekezi.

WAZIRI WA ULINZI NA JKT AKUTANA NA VIJANA WALIOSHIRIKI UJENZI WA IKULU YA CHAMWINO

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb),Tarehe 01 Septemba 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walioshiriki katika ujenzi wa mradi wa kihistoria wa Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma. Mazungumzo hayo yalilenga kuwasikiliza vijana hao, kuwapongeza na kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa katika kutekeleza ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, ambayo ni moja ya alama muhimu za Taifa na Ofisi ya Juu katika mfumo wa Utawala na Uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza na vijana hao, Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Rhimo Nyansaho, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatambua na kuthamini mchango, uzalendo na kujituma kwa vijana hao katika utekelezaji wa mradi huo wa kihistoria. Dkt. Nyansaho amesema Serikali inatambua uvumilivu, nidhamu na kujitolea kwa vijana hao, ambao walishir...

MAKAMU WA RAIS AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS SAMIA ILI AWEZE KUTEKELEZA MAJUKUMU VEMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasalimu Wananchi wa Mbuyuni, Wilayani Moshi waliokusanyika kumlaki akiwa katika ziara binafsi mkoani Kilimanjaro leo tarehe 01 Septemba 2026. Akiwasalimu wananchi hao, Makamu wa Rais amewasihi kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na yeye ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Amesema kwa imani ya maombi ataweza kumsaidia kwa hekima na utii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Makamu wa Rais amesema ataendelea kutekeleza wajibu wake kwa uadilifu, umakini na kujituma, akisisitiza utayari wake wa kushirikiana na viongozi pamoja na wananchi. Akizungumza kwa msisitizo, Makamu wa Rais amesema: “Hatawazingua Wana wala hatamzingua Mama,” kauli ambayo aliitoa pia mkoani Dodoma, kwa wananchi wa Chamwino, mara baada ya kuapishwa. Awali, Makamu wa Rais aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo alipokelewa na v...

MAVUNDE, BALOZI WA UINGEREZA WAZUNGUMZIA FURSA ZA UWEKEZAJI MADINI

 Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mheshimiwa Marianne Young, jijini Dodoma, ambapo wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya madini na kuongeza fursa za uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili kwa kina maeneo ya uwekezaji katika sekta ya madini, uongezaji wa thamani ya madini nchini, pamoja na namna ya kuhakikisha rasilimali hizo zinaendelea kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi jumuishi na wenye manufaa kwa wananchi. Mkutano huo pia umeangazia umuhimu wa kuendeleza mazingira yatakayowezesha ushirikiano na uwekezaji wenye tija katika sekta ya madini, huku Tanzania ikiendelea kutumia rasilimali zake za madini kama fursa ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi. Tanzania na Uingereza zimeeleza dhamira ya kuendelea kushirikiana katika maeneo yenye manufaa kwa pande zote mbili, kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya nchi hizo na kukuza ustawi na maendeleo ya wananchi wa ma...

TMA YATOA ANGALIZO, WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI MWELEKEO WA MVUA ZA VULI

 Na Mwanamkuu Mwandoro,Tanga.  Wananchi mkoani Tanga wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa kufuatia mvua zinazotarajiwa kunyesha na kutopuuzia utabiri wa hali ya hewa kwani kuna uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa katika msimu ujao wa mvua, huku kukiwa na dalili za kuwepo kwa hali ya hewa ya El Niño. Angalizo hilo limetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa mkoa wa Tanga Kurwa Mbwambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alizitaka pia kamati za maafa kuzingatia taarifa za hali ya hewa na kuchukua tahadhari mapema. Aidha Mbwambo aliongeza kuwa viashiria vya hali ya hewa vinaonesha uwepo wa hali ya El Niño ambayo inaweza kuathiri mwendo wa mvua katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba utabiri wa sasa unaonesha kuwepo kwa mvua za vipindi vifupi,na huku mvua za vuli zikitarajiwa kuanza kunyesha katika juma la kwanza/pili la mwezi oktoba 2026 hadi Januari 2027. “Wananchi wasipuuze taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa sababu zinatolewa ili kuwaweze...

STANDI YA MABASI RASMI KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 8.

 Na Mwanamkuu Mwandoro,Tanga  Serikali mkoani Tanga imetoa agizo Kwa wamiliki wote wa Mabasi yanayosafirisha abiria kwenda nje ya mkoa,nchi jirani na maeneo mbalimbali ya nchi kuhakikisha kuwa ifikapo September 8,2026 Magari yote yanaanza na kumaliza safari zake katika kituo kikuu cha Mabasi kilichopo Kange. Agizo hilo linatokana na maadhimio yaliyotolewa na ofisi ya Waziri mkuu, Kamati ya Bunge inayoshughulika na Ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 'TAMISEMI' pamoja na wamiliki na wadau wa usafirishaji kwa lengo la kuhakikisha huduma ya usafirishaji inaimarika pamoja na kuchangia maendeleo ya mkoa huo hususani kwa Halmashauri ya jiji la Tanga kupitia kituo hicho ambacho kinatarajia kuwa kitovu cha uchumi. Akizungumza katika kikao cha pamoja na wadau wa usafirishaji wakiwemo wamiliki wa Mabasi Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani amesema kuwa utekelezaji wa agizo hilo umezingatia utekelezaji wa Sheria ndogo ya Halmashauri 'by laws' ya mwa...

SHABIBY AWAKABIDHI VIJANA PIKIPIKI 370, ATOA WITO WA UAMINIFU NA BIDII

 Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby, amekabidhi pikipiki 370 kwa vijana wa Jimbo la Gairo kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kujenga vyanzo vyao vya kipato. Akizungumza katika hafla ya kiwakabidhi pikipiki hizo 370, Mbunge huyo wa Jimbo la Gairo Shabiby amesema pikipiki hizo zimetolewa kwa kuzingatia zaidi vijana wenye uhitaji na wasio na uwezo wa kuanzia, akisisitiza kuwa umaskini ni miongoni mwa vigezo vilivyozingatiwa katika kuwafikia wanufaika. Amesema mpango huo utaendelea, ambapo kila mwisho wa mwezi vikundi vitano vitapatiwa pikipiki 50 kwa mfumo wa mkopo, huku akieleza kuwa mpango huo unalenga kuwafikia vijana wengi zaidi ndani na nje ya Gairo. Shabiby amewataka vijana waliopatiwa pikipiki hizo kuzitumia kwa uangalifu, kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanarejesha mikopo kwa wakati, akisema uaminifu wao ndio utakaowezesha vijana wengine kupata fursa hiyo. “Ninyi mliochukua pikipiki si kwamba ndiyo mwisho kupata pikipiki. Ninyi sasa ni mabalozi wazuri. Mtakapoli...

MOI YAZIDI KUBORESHA UPASUAJI KWA TEKNOLOJIA ZA KISASA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema taasisi hiyo imeendelea kutumia teknolojia za kisasa na akili unde katika kuboresha huduma za upasuaji, uchunguzi na matibabu kwa wagonjwa. Akizungumza leo, Septemba 1, 2026, Dkt. Ulisubisya amesema MOI inatumia teknolojia inayochakata taarifa za mgonjwa na kutengeneza ramani maalum inayomwongoza daktari wakati wa upasuaji, hivyo kumwezesha kufika kwa usahihi katika eneo lenye tatizo na kupunguza hatari wakati wa matibabu. Amesema teknolojia hiyo pia imeanza kutumika katika uchukuaji wa sampuli za uvimbe kwa ajili ya uchunguzi wa maabara, ambapo vifaa vidogo humsaidia daktari kufikia eneo lenye tatizo na kuchukua sampuli bila kulazimika kufanya upasuaji mkubwa kama ilivyokuwa awali. Kwa mujibu wa Dkt. Ulisubisya, matumizi ya teknolojia hiyo yamewezesha kupunguza ukubwa wa afua, muda wa mgonjwa kukaa hospitalini na kuongeza ufanisi wa huduma za uchunguzi na matibab...