JESHI la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) linakusudia kuzindua mashindano yanayolenga kuhuisha Sanaa, na muziki wa dansi wenye asili ya kitanzania na Africa. Uamuzi huo wa JWTZ umechukuliwa baada ya kubaini kuanza kusahaulika kwa Sanaa hiyo na kwamba mashindano hayo yatawezesha watanzania kujivunia utamaduni wao, na kuleta mabadiliko makubwa ya kimaadili kwa Taifa. Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na Mkuu Wa Majeshi Jenerali Jacob John Mkunda, kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo ya muziki wa dansi na ngoma za asili, Meja Jenerali Mbaraka Mkeremy ,ametangaza uamuzi huo leo Agosti 10-2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa jeshi wa Msasani Club Jijini Dar es Salaam. Amesema baada ya kuzorota kwa Sanaa hiyo hapa nchini, jeshi la ulinzi wa wananchi kupitia kwa mkuu wake wa majeshi,aliunda kamati kwa kushirikisha wadau mbalimbali ambayo pamoja na mambo mengine imeandaa mashindano hayo ili kuhuisha Sanaa hiyo nchini. Meja jenearali Mkeremy,amesema kuto...
Marato tv - Sauti ya Jamii