NA: MWANDISHI WETU, DODOMA Wanawake, vijana na wenye mahitaji maalum sasa wamefikiwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027, kufuatia bajeti hiyo kuongeza asilimia za mikopo ya makundi hayo kutoka asilimia kumi hadi 15. Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mary Chatanda, Juni 23, 2026, Jijini Dodoma, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anayajali makundi hayo kwa maneno na kwa matendo, ndiyo maana ameamua kuongeza asilimia za mikopo yao. "Uwezeshaji wananchi kiuchumi hasa makundi ya wanawake, vijana na wenye mahitaji maalum ni miongoni mwa vipaumbele vya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameona asilimia kumi haitoshi, ameongeza asilimia tano zaidi ili kuhakikisha makundi hayo yananufaika na fursa za kiuchumi kwa ustawi wao," amesema Chatanda. Sambamba na hilo, Chatanda amesema katika mipango ya maendeleo ni vyema kuhakikisha makund...
Marato tv - Sauti ya Jamii