Skip to main content

Posts

Showing posts from July 13, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo ya Umahiri Kwa Mkuu Wa Kitengo Cha Mawasiliano Wizara ya Nishati

*📌Ni kufuatia Umahiri wa masuala ya Mawasiliano kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025*  ðŸ“Œ *Ampongeza kwa kuwa Kiongozi wa mfano wakati wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji na Utalii Osaka Expo 2025* Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo tarehe 13 Julai, 2025 amemkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati, Bi Neema Chalila Mbuja tuzo ya umahiri kufuatia mchango wake  alioutoa wakati wa Maonesho ya Dunia ya Biashara ya Osaka nchini Japan kwa upande wa Mawasiliano na kuitangaza nchi. Mhe Majaliwa amempongeza Bi. Mbuja wakati wa kilele cha  Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba 2025. Sambamba na hilo Mhe Majaliwa amempongeza Bi. Mbuja kwa kuwa muongozaji wa shughuli na kuwa mahiri wakati wa Kongamano la Kimataifa la Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025. Kwa upande wake Bi. Mbuja amemshukuru Mhe. Majaliwa kwa kukabidhi tuzo hiyo iliyotolew...

Hospitali ya Benjamin Mkapa nchini Tanzania kutoa matibabu ya kibingwa nchini Burundi

 

Waziri Mkuu aiagiza TanTrade kufanya tafiti za masoko ndani na nje ya nchi

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuendeleza juhudi za kutafuta masoko ya nje ili kuongeza mauzo yatakayowezesha nchi kupata fedha za Kigeni. Amesema kuwa TanTrade inapaswa kufanya tafiti za uhakika na uchambuzi wa masoko ambayo bidhaa za Tanzania zinaweza kuuzwa na kutoa taarifa hizo kwa wafanyabiashara kote nchini. Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Julai 13, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufungaji wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar-es-Salaam. “Masoko yamekuwa ya ushindani sana siku hizi, nilipotaja Soko Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) nilikuwa nataka kuwaambia kwamba leo hii tunapotaka kufanya uchambuzi wa masoko yetu, hayo ndio maeneo ya kufanya biashara, TanTrade fanyeni tafiti za uhakika na uchambuzi wa kina” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wazalishaji wote nchini kuweka mkakati ...

Mkuu wa Mawaziri Kenya Atofautiana na Rais Ruto Kuhusu Kuwapiga Risasi Waandamanaji

Mkuu wa Mawaziri Nchini Kenya Musalia Mudavadi ametofautiana na Rais William Ruto huku akivitaka vyombo vya usalama visiwaumize Wakenya wakati wa maandamano. Kwa mujibu wa Bw Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mashauri ya Mambo ya Kigeni,Wakenya wanaoandamana wanatekeleza tu majukumu yao ya kikatiba.  Hata hivyo Mudavadi Kupitia Taarifa yake kwa Vyombo vya Habari, amewataka Wakenya wanaoandamana nao pia waheshimu haki za wengine kwa kuwa huo ndio msingi wa demokrasia. “Tufikirie na tutathmini haki zetu ninapowaomba maafisa wetu wa usalama wasiwajeruhi raia wanaoandamana. Wale wanaoandamana nao pia waheshimu haki za wengine,” akasema Bw Mudavadi katika video ambayo imesambaa mitandaoni. Kauli yake inakuja baada ya Rais William Ruto wiki jana kuwataka polisi wawalenge kwa risasi wanaoandamana miguuni ili waende hospitalini na pia kuwajibikia mashtaka kortini. Rais Ruto alisema japo hajaamrisha wauawe, polisi lazima wakabili wahalifu kwa mujibu wa sheria. 

Aliyekuwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari afariki Dunia

Rais wa Zamani wa Nigeria Jenerali Mstaafu Muhammadu Buhari amefariki dunia Nchini Uingereza alikokuwa kwa Matibabu.  Kufuatia kifo cha Buhari,Rais wa Nigeria Bola Tinubu amemwelekeza Makamu wake Kashim Shettima kwenda Nchini Uingereza kwa ajili ya kurejesha mwili wa Marehemu Nchini humo.  Rais Tinubu ametangaza kifo cha Mtangulizi wake Muhammadu Buhari siku ya Jumapili.  Buhari amefariki London siku ya Jumapili majira ya saa 5:30 za Jioni baada ya kuugua kwa Muda mrefu. Tinubu tayari amezungumza na Mjane wa Marehemu Aishat Buhari na kuwasilisha Salamu zake za pole. Marehemu Buhari aliongoza Nigeria kwa Mihula miwili Kati ya Mwaka 2015 na 2023. Wakati wa uhai wake Jenerali Muhammadu Buhari pia amepata kuliongoza Taifa la Nigeria akiwa kiongozi wa Kijeshi Kati ya January 1984 hadi August 1985. Rais Tinubu ameamuru Bendera kupepea nusu mlingoti ikiwa ni heshima kwa Hayati Muhammadu Buhari. 

Himizeni jamii kuzingatia misingi ya maadili - Waziri Mkuu Majaliwa

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa madhehebu ya dini nchini kuendelea kuihimiza jamii kuzingatia msingi ya maadili na kuepuka mienendo iliyo kinyume na tamaduni, mila na desturi ya Mtanzania Amesema kuwa moja ya eneo ambalo viongozi hao wanapaswa kukemea ni kuhusu  matumizi, biashara na usambazaji wa dawa za kulevya kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kunusuru maisha ya Watanzania hususan vijana. Amesema hayo leo (Jumapili, Julai 13, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kumweka wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Dkt. Daniel Henry Mono wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro. “Tuendelee kupambana vikali na matumizi ya dawa za kulevya sababu athari yake ni kubwa hasa kwa vijana wetu, vijana ni kundi tegemewa, matumizi ya dawa za kulevya yanaharibu uelewa na afya za vijana wetu” Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali kwa upande wake imeendelea kuweka sheria kali pamoja na kuimari...

Rushwa "Vigogo" Ccm na Fitna Chanzo cha Kukatwa Wabunge Majimboni

 Hekaheka za mchujo CCM: Sababu ya wabunge nguli kufyekwa na wajumbe hizi hapa  *Yadaiwa walikuwa bize na wananchi wakasahau 'kuwaona' wajumbe wa kamati za siasa *Wajumbe wengine walia kupunjwa mgao BAADHI ya kamati za siasa za chama cha mapinduzi CCM za wilaya nchini zinadaiwa kukiuka taratibu za chama hicho za kuwapata viongozi wa dola kwa madai ya kupokea rushwa jambo ambalo liliwafanya kuendesha vikao vyao kwa upendeleo mkubwa,chuki na fitna. Uchunguzi ambao umefanywa katika baadhi ya mikoa nchini umebaini kuwa baadhi ya viongozi wa kamati hizo hasa wenyeviti na makatibu walinunuliwa kabla ya kuanza kwa vikao hivyo vya mapendekezo kwa wagombea ubunge na udiwani. Imeelezwa kuwa chanzo cha viongozi hao kununuliwa na baadhi ya wana ccm waliokuwa tayari wamejipanga kuchukua fomu ni kutokana na baadhi ya wabunge kushindwa kuwajali binafsi badala yake walitumia muda mwingi kwa shughuli za maendeleo pamoja kuwalinda wajumbe katika maeneo hayo. Imeelezwa kuwa kutokana na wabunge ...