Skip to main content

Posts

Showing posts from May 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Ashtushwa na Kifo Cha Charles Hilary

 Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Charles Hilary, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar kilichotokea leo Mei 11, 2025. Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, familia, ndugu, jamaa na marafiki na wadau wote wa sekta ya habari nchini kwa msiba huu. Ndugu Charles Hilary atakumbukwa kwa mchango wake adhimu wa zaidi ya miaka 40 katika kukuza sekta ya habari nchini tangu akiwa redioni hadi kwenye televisheni, pamoja na unasihi kwa wanahabari wachanga. Namuomba Mwenyezi Mungu aijaalie familia yake uvumilivu na subra katika kipindi hiki kigumu, na ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema. Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea.

Dkt. Tulia Azindua Mradi Wa Kusambaza Umeme Katika Vitongoji 105 Mkoa Wa Mbeya

📌 *Zaidi ya Shilingi Bilioni 10.9 kutumika* 📌 *Wananchi wasisitizwa kulinda miundombinu ya umeme* Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson leo Mei 10, 2025 amezindua rasmi mradi wa kusambaza umeme katika Vitongoji 105 katika Mkoa wa Mbeya. Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kumkabidhi rasmi Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu, Usafirishaji na Usambazi Umeme (ETDCO), Mhe. Dkt. Tulia amewasisitiza wananchi waliopo maeneo ambapo mradi utapita waanze kufanya maandalizi ya kupokea umeme katika nyumba zao. “Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuonyesha mapenzi makubwa kwa Watanzania na hasa wananchi wa Mbeya. Fedha hizi zitakazotekeleza mradi huu zingeweza kupelekwa katika miradi mingine. Niwasisitize wananchi ambao mradi huu utapita muanze kuandaa nyumba zenu mapema kwa ajili ya kupokea umeme na kuingiza katika nyumba zenu pindi mradi utakapowafikia. Na hi...

Serikali Itaendelea Kuiamini Na Kuiunga Mkono Red Cross - Dkt. Biteko

📌 DkT Biteko amwakilisha Rais Samia Mkutano wa mwaka Red Cross 📌 Awataka kutembea kifua mbele kwa kazi za Kudumisha Ubinadamu 📌 RED CROSS yaishukuru Serikali kwa kuungwa mkono   Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali itaendelea kuiamini na kukiunga Mkono Chama cha Msalaba mwekundu (RED CROSS) ili kiendelee kufanya kazi yake nzuri ya kuwahudumia Watanzania.  Dkt. Biteko Amesema hayo Mei 10, 2025 Jijini Dodoma wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 63 ya Chama cha Msalaba Mwekundu (RED CROSS). Amewahimiza viongozi na wanachama wa chama hicho kutembea kifua mbele na kijisimamia na kujipambanua kutokana na kazi nzuri wanayoifanya bila kujali hali wala mazingira ya kazi husika. Amesema Serikali tayari kuendelea kufanya kazi na Chama cha Msalaba mwekundu ili kuhakikisha Watanzania wanaendelea kupata huduma bora ikiwemo masuala ya uokoaji maisha. “Serikali inata...

Mwili Wa Mzee Cleopa David Msuya Wafikishwa Nyumbani Kwake Upanga Dar Es Salaam

  Mwili wa Hayati Mhe. Cleopa David Msuya, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu ukiwasili nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam ambapo unapokelewa na familia, ukitokea Hospitali ya Jeshi, Lugalo, leo Mei 10, 2025.

Waziri Mkuu Amesema Dini Zina Mchango Mkubwa Katika Kuimarisha Ustawi Wa Jamii

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema madhehebu ya dini yana mchango mkubwa katika kuimarisha ustawi wa jamii na kutoa huduma za kiroho. Amesema kwa kutambua hilo, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wote amekuwa akitekeleza kwa vitendo dhamira ya kukuza ushirikiano kati ya Serikali na madhehebu ya dini. Amesema hayo leo Jumamosi (Mei 10, 2025) alipomuwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia katika kilele cha dua maalum ya kuombea viongozi wa Kitaifa, amani, uchaguzi mkuu pamoja na kuwaombea mamufti na masheikh waliotangulia mbele za haki, kwenye Viwanja vya Msikiti wa Mohammed VI, Kinondoni Dar es Salaam. “Ni ukweli usiopingika sote tumeshuhudia kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jinsi gani anawathamini, anawasilikiza na kuwashirikisha viongozi wa madhehebu ya dini katika masuala muhimu ya kitaifa”. Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amempongeza Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir bin Ali Mbwana kwa kuandaa dua hiyo kwa a...

Rc Chalamila Azindua Mpango wa Kufanya Biashara Saa 24 Wilaya ya Ubungo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amezindua mpango wa ufanyaji biashara kwa saa 24 kwenye soko la Mbezi eneo la stendi ya Malamba Mawili wilayani Ubungo na kuwahakikishia usalama wafanyabiashara huku akiwataka maafisa biashara kutowaonea wafanyabiashara Akizungunza wilayani Ubungo Jijini Dar es salaam katika uzinduzi huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye soko la mbezi mbele ya mamia ya wafanyabiashara wa Soko hilo waliokusanyika kumsikiliza Mkuu wa Mkoa huyo amesema jiji hilo ni kitovu cha biashara inayochagizwa na uwepo wa bandari,kituo cha mabasi cha Magufuli na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Nyerere hivyo hakuna sababu ya kulala.  Aidha RC Chalamila amewataka wafanyabiashara kutohofia usalama wao kwani Serikali Mkoani humo inazidi kuimarisha ulinzi na usalama ili jiji hilo liwe na amani zaidi huku akimuagiza mkuu wa wilaya ya Ubungo kutoruhusu maafisa biashara kuwaonea wafanyabiashara hao kwani vitendo hivyo ni kinyume na utaratibu Hata hivyo RC Chala...