Askari Polisi Moses Mwaulambo Atoa Elimu ya Kuzuia Uhalifu na Wahalifu Kupitia Polisi Jamii Cup 2024 Musoma
Na Shomari Binda-Musoma VIJANA kutoka Wilaya ya Musoma Mkoani Mara, wametakiwa kuwa wa kwanza kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili jamii iweze kuishi salama na kushiriki shughuli za kiuchumi Ujumbe huo umetolewa agosti 27 na Mkaguzi wa Polisi na askari Kata wa Kata ya Bweri Moses Mwaulambo, kwenye muendelezo wa mashindano ya Polisi Jamii Cup 2024 Wilaya ya Musoma Akizungumza na wachezaji wa timu ya Bweri na Mara Sport Mwaulambo, amesema mahala ambapo hakuna uhalifu shughuli za kiuchumi ikiwemo michezo ufanyika kwa ufanisi Amesema michezo kwa sasa ni sehemu kubwa ya uchumi na wachezaji wengi wanajipatia kipato hivyo ni vyema kushiriki michezo huku taarifa za uhalifu na wahalifu zikitolewa. Mwaulambo amesema wahalifu sio watu wazuri kwani wanaweza kufanya uhalifu wa wizi wa mali ambazo mwanamichezo amezitafuta hivyo ni vyema kumtolea taarifa. " Tuko hapa kwa ajili ya kushiriki michezo lakini tunapeana ujumbe wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwenye maeneo yetu. ...