Na. Calvin Katera - Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ametoa maagizo sita kwa Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Massana Mwishawa leo Julai 09, 2026, jijini Arusha alipokuwa akiongoza zoezi la uapisho kwa aliyekuwa Naibu Kamishna wa Uhifadhi baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Julai 02, 2026 kuchukua nafasi ya Kamishna wa Uhifadhi (Mstaafu) CPA Musa Nassoro Kuji aliyemaliza muda wake. Akizungumza katika hafla ya uapisho huo Waziri Kijaji amemwelekeza Kamishna Mwishawa kusimamia miundombinu ya hifadhi, kuvutia wawekezaji, kubuni bidhaa mpya za utalii, kusimamia mapato, kuimarisha uhusiano na jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi bila kusahau nidhamu, uadilifu, weledi, ustawi wa watumishi na kusimamia maslahi yao kwa wakati. Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini TANAPA, Mkuu wa Majeshi (Mst.) Jenerali George Waitara alieleza kuwa Bodi itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati na ushauri wakati wote ili kufanik...
Marato tv - Sauti ya Jamii