Accra, Ghana Nchi za Ghana na Tanzania zinaendelea kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi katika utekelezaji wa sera za Ushirikishwaji wa Wazawa katika Sekta ya Madini (Local Content), kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wananchi wa ndani katika minyororo ya thamani ya madini, kuimarisha uwezo wa taasisi za ndani na kuhakikisha manufaa ya kiuchumi yanabaki ndani ya nchi. Hayo yamebainishwa katika ziara rasmi ya kubadilishana uzoefu kati ya wawakilishi wa Tume ya Madini ya Tanzania na Tume ya Madini ya Ghana, iliyolenga kujifunza na kushirikishana mbinu bora, sera na mifumo ya utekelezaji wa Local Content katika sekta ya madini. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, Dkt. Theresia C. Numbi, amesema kuwa sera ya Local Content si takwa la kisheria pekee, bali ni nyenzo muhimu ya kuchochea maendeleo ya taifa, ujenzi wa viwanda na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wananchi. “Ningependa kusisitiza kuwa Maudhui ya Ndani katika sekta ...
Marato tv - Sauti ya Jamii