Skip to main content

Posts

Showing posts from September 1, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ni shangwe tupu mapokezi ya Dk.Nchimbi wilayani Itilima akiendelea na mikutano kuomba kura kuelekea uchaguzi mkuu

Wakazi wa Kata ya Langabilili,wilaya ya Itilima mkoani Simiyu leo Jumanne Septemba 2,2025 wamejitokeza kwa wingi kumpokea na kumkaribisha kwa shangwe Mgombea Mwenza wa Urais wa   Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiendelea na ziara mkoani Simiyu.  Dkt.Nchimbi amepokewa kwa shangwe na Wananchi wa Langabilili,ndani ya jimbo la Itilima, huku wakionesha shauku kubwa ya kutaka kumuona na kumsikiliza katika mkutano wake wa Kampeni. Dk.Nchimbi ambaye alitokea mkoani Mara na sasa ameingia mkoa wa Simiyu kuendelea na mikutano ya kampeni katika Mkoa huo,baada ya kutoka Busega,Bariadi Vijijini na sasa ameingia jimbo la Itilima  kufanya mkutano mkubwa wa Kampeni Akiwahutubia wananchi katika stendi ya Mabasi ya Langabilili, Itilima mkoani Simiyu, katika muendelezo wa mikutano yake ya Kampeni,Balozi Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Itilima,Njalu Daudi Silanga sambamba na Wagombea Ubu...

Majaliwa Kufungua Kongamano la Chama Cha Madereva

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Septemba 02, 2025 anafungua Kongamano la nne la Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania, linalofanyika katika Kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Mkutano huo unakaulimbiu isemayo:- _DEREVA WA SERIKALI, EPUKA AJALI, LINDA GARI LAKO NA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA NA OKTOBA SHIRIKI UCHAGUZI MKUU_

Rc Makalla Awatembelea Viongozi wa Dini.

. _Lengo ni kujitambulisha na kuomba ushirikiano. . Asema ushirikiano wa serikali na  Taasisi za dini ni muhimu._  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Makalla Leo Jumatatu Septemba Mosi, 2025 amefanya ziara ya kuwatembelea viongozi wa Dini Mkoani Arusha kwa lengo la kujitambulisha na  kubadilishana uzoefu katika mambo mbalimbali. Ziara ya mkuu wa mkoa ni muendelezo wa ziara zake za kujitambulisha na kupata taarifa za taasisi mbalimbali katika mkoa wa Arusha. Katika ziara hiyo kwa Askofu wa tatu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Askofu Dkt. Godson Abel Mollel, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Sheikh Shaaban Juma Abdallah na Nabii Mkuu Dkt. GeorDavie M. K wa Kanisa la Ngurumo ya Upako, Mhe. Makalla amewaomba pia Viongozi hao ushirikiano  pamoja na kuliombea Taifa la Tanzania ili liendelee kuwa na Amani na utulivu. Kwa upande wao Viongozi hao wa dini, mbali ya kumshukuru Mhe. Makalla kwa kuwatembelea, kujitambulisha na kuomba us...

Dkt.Nchimbi Awanadi Wagombea Ubunge,Madiwani wa Simiyu Kwa Wananchi

MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel  John Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa CCM,wilaya ya Bariadi Vijijini  mkoani Simiyu kuendelea na mkutano wa Kampeni, leo Jumatatu Septemba 1,2025. Dk.Nchimbi aliyekuwa Mkoa wa Mara na sasa ameingia Mkoa wa  Simiyu kuendelea na kampeni,akianzia jimbo la Busega na baadae kuelekea  jimbo la Bariadi Vijijini na kufanya mikutano mikubwa ya hadhara. Akiwahutubia wananchi wa Bariadi Vijijini  mkoani Simiyu, Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi Vijijini,Masanja  Kungu Kadogosa sambamba na wagombea ubunge wengine pamoja na Madiwani wa mkoa huo. Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania  kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, katika Uchaguzi mkuu una...

Maboresho bandari ya Tanga yataleta tija Kimataifa

Na Mwandishi Wetu, Tanga Serikali imesema uwekezaji uliofanyika katika Bandari ya Tanga unaenda kuleta nafasi kubwa kiuchumi Kitaifa na Kimataifa. Hayo yamesemwa leo Septemba  Mosi, 2025 na Msajili wa Hazina ( OTR)  Nehemia Kyando Mchechu mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika bandari hiyo. Akiongea mara baada ya kupokea taarifa ya utendajikazi wa bandari hiyo, Mchechu alisema kuwa  uwekezaji uliofanywa na Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan uliogharimu kiasi cha shilingi za Kitanzania Bilioni 429.1  umefanya meli kubwa kuweza kutia nanga katika bandari hiyo. “Uwekezaji huu ukianza na sehemu ya kutolea huduma yenye urefu wa mita 450, kina cha maji kutoka mita 3 kuwa mita 13, na lango la kuingilia kutaniliwa kufikia upana wa mita 135 lakini bado kuna mipango inayofanyika ya kuongeza tena mita 900”. Aliongeza Mchechu  Aidha Mchechu alisema kuwa,ukiangalia  uwekezaji huu tunahakikisha kuwa sekta binafsi pamoja na sekta za umma zinaungana  kati...