Na Angela Sebastatian- Bukoba MAHAKAMA ya hakimu mkazi Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imefunga rasmi mwenendo kabidhi kuhusu shauri namba 17740 linalowakabiri washitakiwa tisa akiwemo padri wa kanisa Katoliki pamoja na baba mzazi wa mtoto Noela Asimwe Novart (2.5) ambaye aliuawa na kisha kukatwa mikono yako na mwili kutelekezwa katika karavati. Waziri Magumbo mwendesha mashitaka wa mkoa wa Kagera kwa kushirikiana wa mawakili wenzake wanne wa serikali akiwemo Erick Mabagala alisema kuwa kesi hiyo ilifikishwa mbele ya hakimu Mkazi mfawidhi mahakama ya wilaya Bukoba Elipokea Yona kwa mara ya kwanza Juni 28 mwaka. Amesema Mei 30 mwaka huu mtoto Noela aliibwa na watu wasiojulikama ambao walifika nyumbani kwao marehemu huyo na kumpola mikononi mwa mama yake kisha kutokomea kusikojulikana ambapo Juni 17mwaka huu mwili wa Noela ulipatikana ukiwa umetelekezwa katika karavati lililoko barabara ya Ruhanga ukiwa umekatwa mikono. Magumbo akisaidiana mawakili wanne wa Jamhuri ...
Marato tv - Sauti ya Jamii