Skip to main content

Posts

Showing posts from February 12, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Sagini apeleka Mradi wa kisima cha Maji kwa Wakazi 600 Kitongoji cha Makundusini

Jumla ya Wakazi 600 wa Kitongoji cha Makundusini, Kijiji cha Singu Kata ya Kukirango Wilaya ya Butiama mkoani Mara wamenufaika na Mradi wa Maji uliofanikishwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Jumanne Abdallah Sagini kupitia Taasisi ya Direct Aid Society Tawi la Tanzania kutoka Kuwaït. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kisima cha Maji chenye uwezo za kuzalisha zaidi ya lita 20000 kwa siku, Mgeni Rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Thecla Mkuchika amepongeza juhudi zilizofanywa na Mbunge Mstaafu wa Jimbo hilo Mhe. Jumanne Sagini  kwa kitendo cha kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sera ya kumtua ndoo mama kichwani pia amesema mradi huo utapelekea kuondokana na magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.  Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Direct Aid Society Tawi la Tanzania kutoka Kuwaït Bw. Abdelhamid Ismail amesema kuwa taasisi ilianza kutoa hudu...

Kamati ya Bunge Yaahidi Kushirikiana na Tamisemi Katika Usimamizi wa Elimu Msingi Nchini

Na OWM - TAMISEMI, Dodoma Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Florent Kyombo amesema kamati yake itashirikiana kwa karibu na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM -TAMISEMI) katika usimamizi na uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari ili wanafunzi wapate ufaulu mzuri  utakaowezesha kutimiza ndoto zao kitaaluma. Mhe. Kyombo ametoa ahadi hiyo leo Februari 12, 2026 wakati wa kikao cha mafunzo kwa wajumbe wa kamati yake, yaliyohusu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM),   katika Ukumbi wa Anne Makinda Bungeni Jijini Dodoma. “Mhe. Waziri wa TAMISEMI tunakuamini wewe pamoja na watendaji wa ofisi yako, hivyo sisi tunakuahidi ushirikiano ili kuiwezesha ofisi yako kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,” amesisitiza Mhe. Kyombo. Aidha, Mhe. Kyombo amesema, wajumbe wa kamati yake wamepata uelewa mzuri kuhusu Usimamizi na Uendesha...

Dkt. Mwigulu Ataka Mikakati ya Kulinda Viwanda Vya Ndani

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaka Taasisi za udhibiti za Serikali kuweka kipaumbele katika kulinda viwanda vya ndani na biashara badala ya kuwa kikwazo katika kufikia mafanikio. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa haitakuwa rahisi kulinda viwanda na biashara za ndani kama Tanzania itakuwa jalala la bidhaa kutoka nje. Amesema hayo leo Alhamisi (Februari 12, 2026) alipozindua kiwanda cha mabati cha Lodhia kilichopo Mkuranga mkoani Pwani. “Wizara ya fedha hakikisheni hamtoi msamaha wala unafuu wa kodi katika bidhaa za nje ambazo zinapatikana ndani ya nchi. Toeni unafuu wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi kama uzalishaji ndani ya nchi hatujitoshelezi” Aidha, Dkt. Mwigulu ameitaka  Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania na Vyombo vya ulinzi kuhakikisha hakuna bidhaa za  magendo zinazoingia nchini. “Taasisi zote na vyombo vya ulinzi simamieni uingizaji wa bidhaa ndani na ufuate utaratibu, msipofanya hivyo mtaua uwekezaji unaofanywa ndani.” Amesema kuw...

Dkt. Mwigulu Ataka Ushirikiano wa Kikanda Kwenye Mapambano Dhidi ya Saratani

_▪Asisitiza Tanzania itaendelea kuwa kituo bora cha ushirikiano wa kikanda na Afrika_ _▪Asema shilingi bilioni 18.5 zimetengwa kwa ajili ya uanzishaji wa huduma za PET-CT Scan na mashine ya Cyclotron_ _▪Asema Tanzania inalenga kupunguza vifo vitokanavyo na saratani kwa angalau asilimia 30 ifikapo mwaka 2030_   WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Afrika haiwezi kushinda vita dhidi ya saratani ikiwa kila nchi itafanya kazi peke yake.  Amesema kuwa ili kufikia malengo ya mapambano dhidi ya saratani, kunahitajika kuwepo kwa ushirikiano wa kikanda na wa bara zima katika utafiti, mafunzo, kubadilishana wataalamu na kubadilishana rasilimali, teknolojia pamoja na uzoefu. Ametoa wito huo leo Alhamisi (Februari 12, 2026) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 30 ya  Taasisi ya Saratani Ocean Road, yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  “Tanzania iko tayari kushirik...

Waziri Mkuu Kuanza Ziara ya Siku Tano Mkoani Tanga

Na MASHAKA MHANDO,Tanga WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Tanga Ijumaa February 13, ambapo atakagua na kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 758.1. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Buriani, akizungumza na waandishi wa habari Leo February 12 ofisini kwake alisema Waziri Mkuu atapokelewa majira ya saa tatu asubuhi katika eneo la Mkata, Wilayani Handeni, akitokea mkoani Pwani. Akiwa Handeni, Waziri Mkuu atakagua mradi mkubwa wa umeme utakaohudumia wilaya za Pangani, Muheza na Korogwe, kisha atazindua chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na kuweka jiwe la msingi la ujenzi. Baada ya hapo, msafara utaelekea wilayani Kilindi kukagua mradi wa tenki la maji na hospitali ya wilaya, kabla ya kuelekea Korogwe kwa ajili ya ukaguzi wa mradi mkubwa wa maji wa miji 28. Ratiba inaonyesha kuwa Februari 15, Waziri Mkuu atakuwa wilayani Mkinga kukagua ujenzi wa Chuo Kikuu Mzum...

Dkt Migiro Afanya Mazungumzo na Balozi wa Namibia, Wajadili Kuimarisha Urafiki wa Kidugu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Asha-Rose Migiro, leo, Alhamis, Februari 12, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Namibia hapa nchini, Mheshimiwa Gabriel Pandureni Sinimbo. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao, wamejadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na urafiki wa kidugu kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha SWAPO, pamoja na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Namibia.