Na Angela Sebastian ;Bukoba MKUUU wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ameunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya tendo la uhuruma kwa watoto yatima,wanaoishi mazingira magumu na wenye uhitaji katika sikukuu ya Christmas. Hajat Mwassa amewaalika watoto zaidi ya 200 kutoka katika vituo vinne vya kulelea watoto yatima na wale wenye uhitaji vilivyoko Manispaa ya Bukoba ambapo amepika chakula na kisha kula nao mlo wa mchana lengo,likiwa ni kusherehekea sikukuu hiyo muhimu ili nao wajione kuwa wanayo haki ya kuungana na wengine wakati wa furaha. "Nimeamua kupika mwenyewe hapa Ikulu ndogo ya mkoa wa Kagera kisha kupakua,kula na kunywa na watoto hawa wenye uhitaji na yatima ili tufurahi wote katika sikukuu hii,maana tumezoea kubeba vyakula,nyama na vinywaji kupeleka vutuoni na kuacha lakini mimi nimeona tendo hilo la huruma nilitekeleze kwa njia hii"ameeleza Mwassa Kwa upande wa mwenyekiti wa cha Mapinduzi (CCM) Wilay...
Marato tv - Sauti ya Jamii