Skip to main content

Posts

Showing posts from November 8, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Kuanzisha Mchakato wa Maridhiano-Makamu wa Rais

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Emmanuel Nchinbi amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itaanzisha mchakato wa mazungumzo ya maridhiano ili kuimarisha umoja, amani na mshikamano wa kitaifa. Akizungumza kwa niaba ya Rais, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao Dk. Nchimbi amesema serikali imejizatiti kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuishi kwa utulivu na chini ya misingi ya utawala wa sheria. “Ni dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunaanzisha mazungumzo ya maridhiano ili hata hao wachache wanapata nafasi ya kusikilizwa na kuwa na taifa lenye amani na utulivu,” amesema Dk Nchimbi akiwashukuru viongozi wa SADC.

Dkt Tulia ameonesha ukomavu mkubwa wa kiuongozi - Msama

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Msama Promotion Ndugu Alex Msama amesema ameona Watanzania wengi wakikosoa au kulaumu kitendo cha Dkt. Tulia Ackson kujiondoa kwenye michuano wa kugombea Uspika wa Bunge kwamba labda kuna kitu kibaya, au hatakiwi au amesusa. Msama amesema kujitoa kwa Dkt. Tulia ni jambo zuri linaloashilia ukomavu wake wa kiuongozi na Kidemokrasia, amesema Dkt. Tulia hana kashfa mbaya, sio fisadi, sio mla rushwa bali ameonesha kwa vitendo ubora wake katika Uongozi hadi kuchaguliwa kuwa Rais wa Wabunge wote Duniani. "Amewaachia nafasi wengine waweze kupata baada ya yeye kufanya vizuri katika kipindi chake, inaonesha hana tamaa na madaraka, na kwa uwezo wake mkubwa ni matumaini yangu kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atamteua katika nafasi nyingine kubwa ili andelee kuwatumikia Watanzania' - amesema Msama.

Wabunge Waanza Kujisali

 Waheshimiwa Wabunge Wateule leo tarehe 8 Novemba, 2025 wakijisajili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Kumi na Tatu unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 Novemba, 2025.