Skip to main content

Posts

Showing posts from July 21, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

EMEDO Yaeleza Juhudi Zake Kwenye Kusimamia Miradi inayogusa Jamii

Mwandishi wetu ;TANGA Shirika la Environmental Management and  Economic Development Organization  (EMEDO)limefafanua utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija katika jamii kwenye kikao cha pamoja Kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja Mashirika yasiyo ya Kiserikali  kinachofanyika Jijini Tanga. Afisa Mawasiliano wa EMEDO Peter Kimisha akishiriki  hatua ya awali ya  kueleza mategemeo ya Shirika kwenye mkutano huo  aliweka bayana kuwa EMEDO inakiona kikao hicho kuwa ni fursa ya kueleza mbele ya wadau wengine utekelezaji wa kazi zake Kwa Mwaka 2025 - 2026 pamoja na kutengeneza mahusiano mkakati na wadau wengine. Peter Pia alieleza umuhimu wa kikao hicho ni kuuelewa vyema muongozo wa mashirikiano baina ya Sekta ya Uvuvi na Asasi za Kiraia zinazofanya kazi kwenye eneo la uvuvi. Naye Bwana Edwin Soko, Mjumbe wa Bodi wa EMEDO alitoa wasilisho zuri lililoeleza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika la EMEDO kwenye eneo la uchumi na mazingira ndani ya se...

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awasili Nchini Belarus Kwa Ziara ya Kikazi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amewasili jijini Minsk, Belarus kwa ziara ya kikazi ya siku nne kuanzia tarehe 21 hadi 24 Julai 2024.  Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa nchi hiyo, Mhe. Waziri Mkuu alipokewa na Naibu Waziri Mkuu wa Belarus, Mhe. Viktor Karankevich na viongozi wengine waandamizi wa nchi zote mbili akiwemo Waziri wa Uwekezaji, Zanzibar, Mhe. Sharif Ali Sharif; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Fredrick Kibuta. Ziara hiyo ambayo  ni ya kwanza kwa kiongozi wa ngazi ya juu nchini Tanzania kuifanya nchini Belarus, inalenga kuendeleza mkakati wa Serikali zote mbili wa kuimarisha uhusiano wa uwili hususan katika sekta za kimkakati ikiwemo kilimo, elimu, afya, utalii, uwekezaji, biashara na uhaulishaji wa teknolojia. Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Waziri Mkuu atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Belarus, Mhe. ...

Kambi ya Kutengeneza Mishipa ya Damu, Upandikizaji Figo Yaanza Rasmi Muhimbili Mloganzila

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeanza kambi maalum ya kutengeneza mishipa ya kuchuja damu sambamba na kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye changamoto za figo ambayo itahitimishwa rasmi Julai 23, 2025. Kambi hiyo inafanywa na wataalam wa Muhimbili Mloganzila kwa kushirikiana na jopo la wataalam kutoka Korea Kusini linalo ongozwa na Prof. Park Kwan Tae ambaye ni Daktari Bingwa Bobezi wa Upasuaji chini ya uaratibu wa Taasisi ya Africa Future Foundation (AFF) ya nchini Korea Kusini. Upandikizaji wa figo unafanyika kwa kuvuna figo kutoka kwa mchangiaji kwa kutumia matundu madogo (Laparascopic Hand Assisted Donor Nephroctomy) utaalam ambao kwa hapa nchini unapatikana Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila pekee. Aidha,wataalam mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanajengewa uwezo wa kutoa huduma hizo katika maeneo yao ili kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kwenda mbali na maeneo yao kufuata huduma hizo. Hadi kuhitimishwa kwa kambi hiyo wananchi takribani 60 watanufaika na huduma ...