Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amemuondoa katika nafasi yake Meneja wa RUWASA wilayani Misungwi Mhandisi Marwa Kisibo kutokana na kutosimamia utekelezaji wa miradi ipasavyo katika wilaya yake. Waziri Aweso amefanya maamuzi hayo alipotembelea Mradi wa Maji wa Ukiliguru - Usagara - Kolomije - Sumve wa Chanzo cha Ziwa Victoria unaogharimu kiasi cha zaidi ya Bilioni 32 wilayani Misungwi na Kwimba Mkoa wa Mwanza. Ziara hii ni Maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi alipofanya ziara yake mkoani Mwanza wilaya ya Simiyu na kupata malalamiko ya hali ya upatikanaji Maji na kusuasua kwa Miradi. Dkt Nchimbi alimuelekeza Aweso kufika Misungwi na kufanyia kazi changamoto zote Katika ziara hiyo, Mhe Aweso ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri. Mradi huu utanufaisha vijiji 19 wilaya ya Misungwi na vijiji 5 vya wilaya ya Kwimba vyenye jumla ya watu 85,400 na kuondoa kero ya maji katika maeneo makubwa ya Usagara na Nyashishi. Aidha Aweso ...
Marato tv - Sauti ya Jamii