Skip to main content

Posts

Showing posts from August 11, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wananchi Kisiwa Cha Rukuba Wafurahia Mradi wa Umeme Jua

WANANCHI wa waishio kisiwa cha Rukuba kilichopo jimbo la Musoma vijijini wamefurahia kupata mradi wa umeme jua( Solal Energy) ambao wamesema utasaidia kupunguza Changamoto wa upatikanaji wa Nishati hiyo. Wakizungumza  kwa njia ya simu na George Marato TV wamesema mradi huo umekuja kuondoa changamoto nyingi kwao kutokana na Kuishi kisiwani. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Rajabu Msweta amesema wamekuwa hawapati huduma za uhakika za umeme kutokana na kuwa kisiwani. Amesema serikali kupitia Tanesco wanawapelekea  mradi wa umemejua ambao wanaamini utakuwa suluhisho la matatizo. Rajabu amesema umeme ni uhitaji mkubwa kisiwani hapo kwa shughuli za maendeleo na kuishukuru serikali kwa mradi huo. Juma Hamisi mkazi wa kisiwa hicho amesema wamekuwa wakifanyia shughuli za uchomereaji nje ya kisiwa hicho na kutumia gharama kubwa na kumshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwa mfatiliaji wa miradi ya maendeleo. Mbunge wa jimbo la Musom...

SAGINI: Vijiji Vinavyopitiwa na Mradi wa Maji Butiama Kupata Huduma ya Maji Safi na Salama

William Mabusi – WyKS Butiama* Mbunge wa Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amewaahidi wananchi wa Kata ya Busegwe kuwa watapatiwa maji kutoka Mradi mkubwa wa maji wa Mgango, Kiabakari na Butiama kama sera ya maji inavyosema.  Mhe. Sagini ameyasema hayo kwenye Mikutano wa hadhara aliyoifanya kwa nyakati tofauti kwenye Vijiji vya Nyanza, Busegwe na Kigori Kata ya Busegwe, Agosti 11, 2024.  “Mradi wa maji wa Mgango, Kiabakari hadi Butiama umeshafika kijiji cha Bumangi, kinachotakiwa kufanyika ni usambazaji wa maji kwenye vijiji vinavyozunguka bomba kubwa la mradi huo kwa kipenyo cha kilomita 25, yaani vijiji vilivyo umbali wa kilomita kumi na mbili na nusu upande mmoja wa bomba na kilomita kumi na mbili na nusu upande mwingine.” Alisema. Akiongelea uhitaji wa umeme kwa wananchi wa Kata hiyo Diwani wa Kata ya Busegwe Mhe. Hesha Kisibo amesema jumla ya vitongoji kumi na nne vya Kata yake ni vinne tu vimepata umeme na kwa kuwa katika Mpango wa TANESCO M...

Rais Samia Ajivunia Uweledi Mkubwa wa JWTZ

  Na George Marato-Mapinga WAZIRI wa ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dtk Stergomena Lawrence Tax amesema Tanzania itaendeleza mahusiano na nchi rafiki ikiwemo China katika kuimarisha Diplomasia ya ulinzi ili kuongeza uwezo kwa jeshi la Ulinzi la Wananchi katika kukabiliana na matukio mbalimbali ya matishio ya amani duniani.  Akizungumza wakati wa kufunga zoezi la Medani la ushirikiano wa miaka 60 kati ya JWTZ na jeshi la ukombozi la watu wa China,waziri huyo wa Ulinzi na JKT,mbali na kumpongeza Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa  kuridhia zoezi hilo kufanyika hapa nchini,amesema zoezi  hilo linaimarisha ushirikiano na undugu kwa mataifa haya mawili. Amesema Tanzania na China zina historia kubwa kimahusiano na kwamba mahusiano hayo kwa sasa yako kwenye hali ya juu,lakini pia zoezi hilo la medani kwa kuhusisha majeshi ya nchi hizi mbili,limewezesha kubadilisha ujuzi na kuimarisha kwa kiasi kikubwa sekta yetu ya uli...

Serikali Kuendelea Kuajiri Watumishi Sekta Elimu na Afya

Naibu waziri Ofisi wa Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa - TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainab Katimba amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa Kagera kuwa Serikali inaendelea kukabiliana na tatizo upungufu wa watumishi katika kada ya Elimu na Afya baada ya hivi karibuni Serikali kutoa tangazo la ajira hizo. Mhe. katimba amesema hayo kwenye mkutano wa hazara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi - CCM uliofanyika Agosti 10 katika uwanja wa Mashujaa Bukoba mjini wakati akijibu kero zilizoibuliwa na wananchi kuhusu tatizo la upungufu wa watumishi katika kada ya Elimu na Afya ambapo amesema Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi  Umma na Utawala bora imeshatangaza ajira 9,400 katika kada ya Afya na watumishi 11,000 katika kada ya Elimu na katika idadi hiyo mkoa wa Kagera ni mnufaika wa ajira hizo. “Mheshimiwa Katibu Mkuu haya ni maelekezo kuwa tutatue changamoto na naomba niwatangazie wananchi wa Bukoba Mjini katika ajira hizi zilizotangazwa muwe na uhakika mtapata mgao wenu wa wa...