MHESHIMIWA Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameihakikishia Jamhuri ya Belarus kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano na nchini hiyo na kwamba amewaalika wawekezaji na wafanyabiashara kuja nchini kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta za kilimo, uvuvi, elimu na afya. Kauli hiyo imetolewa leo (Jumanne, Aprili 28, 2026) na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov, Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam. Pia, Dkt. Mwigulu amepokea kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaliko wa ziara ya kikazi nchini Belarus wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Belarus, Mheshimiwa Alexander Lukashenko. Waziri Mkuu, amesema Serikali imeboresha mazingira ya uwekezaji na biashara, pia Tanzania kibiashara ipo katika eneo la kimkakati kijiografia kwa kuwa ni kitovu cha Mataifa ya Ukanda wa Afrika Mashariki na ya Kusini mwa Afrika. “Ni kutokana na umuhimu huo, Tanzania kupitia Di...
Marato tv - Sauti ya Jamii