Skip to main content

Posts

Showing posts from January 9, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wananchi Zanzibar Waomba Masoko ya Madini

📍 Zanzibar | Januari 10, 2026 Wananchi wa Zanzibar wameiomba Serikali kupitia Tume ya Madini kuanzisha masoko na minada rasmi ya madini Visiwani humo ili kuwawezesha wafanyabiashara, wachimbaji wadogo na wawekezaji kufanya biashara ya madini kwa uwazi, usalama na bei shindani. Ombi hilo limetolewa na wananchi waliotembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar yanayoendelea kufanyika Fumba, ambapo wameeleza kuwa ukosefu wa masoko rasmi na minada ya madini umekuwa kikwazo kwao kushiriki kikamilifu katika biashara ya madini. Wamesema kuwepo kwa masoko na minada ya madini kutachochea ukuaji wa uchumi wa Zanzibar, kuongeza ajira kwa vijana na wanawake, kuongeza kipato kwa wananchi pamoja na kudhibiti biashara holela ya madini. Kupitia maonesho hayo, Tume ya Madini inaonesha fursa katika utafutaji wa madini, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani, biashara ya madini pamoja na utoaji wa bidhaa na huduma kwa shughuli za migodini. Akizungumza katika...

Waziri Kijaji Azindua Bodi ya Wakurugenzi ya Tawa*

Na Joyce Ndunguru, Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), ameizindua rasmi Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) leo Januari 9, 2026, jijini Arusha. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Dkt. Kijaji amewapongeza wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA kwa kuteuliwa kwao, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko. “Kwa namna ya kipekee nikupongeza sana Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko kwa kuendelea kuaminiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa awamu nyingine tena. Kwa dhati ya moyo wangu, ninawapongeza wote kwa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi ya TAWA, hongereni sana”, amesema Waziri Kijaji. Sambamba na pongezi hizo, Waziri Kijaji ametoa rai kwa Bodi ya TAWA kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika uboreshaji wa miundombinu kwenye maeneo ya hifadhi, kwa lengo la kuyaongezea thamani,...

Rais Samia Azindua Hotel ya Kitalii Kusini Unguja Zanzibar

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Jaz Elite Aurora, Bw. Hamed El Chiaty kuashiria uzinduzi wa Hoteli hiyo katika hafla iliyofanyika Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Januari, 2026.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Hoteli ya Jaz Elite Aurora katika hafla iliyofanyika Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Januari, 2026.  Taswira ya Hoteli ya Jaz Elite Aurora iliyopo Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 09 Januari, 2026. 

Silinde: Awataka Wakandarasi Wazawa Wahakikishe Kunakuwa na Tija Katika Miradi ya Umwagiliaji

📍 Bariadi- Simiyu  Serikali imewataka wakandarasi wazawa wanaotekeleza miradi ya Umwagiliaji nchini kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa wakulima na taifa kwa ujumla, ikisisitiza kuwa uzembe au kuchelewesha utekelezaji kutaibua hatua kali za kisheria dhidi yao. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) akiwa katika muendelezo wa ziara yake mkoani Simiyu, wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji la Kasoli lililopo Kijiji cha Kasoli, Kata ya Kasoli. Bwawa hilo lina ujazo wa takribani mita za ujazo milioni 2.7 na linatarajiwa kuhudumia mashamba yenye ukubwa wa hekta 650. Mhe. Silinde amesema kuwa uamuzi wa Serikali kuwapa wakandarasi wazawa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo ya Umwagiliaji, unalenga kuwajengea uwezo na kukuza ujuzi wa ndani ili wazawa washiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi yao. Amesisitiza kuwa imani hiyo lazima iendane na uwajibikaji, ubora wa kazi na kukamilisha miradi kwa wakati uliopangwa. “Serika...

Dk.Migiro:Ccm lnajengwa Kuanzia Ngazi ya Mashina Sio Majukwaani

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Asha-Rose Migiro amesema Chama hicho hakijengwi katika majukwaa bali hujengwa kuanzia ngazi ya mashina na matawi huku akibainisha majukwaa hutumika zaidi kwa ajili ya kutoa hamasa. Dk.Migiro ametoa kauli hiyo leo Januari 9,2026 alipokuwa akizungumza na viongozi wa mashina na matawi wa Wilaya za Kinondoni na Ubungo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kwa viongozi hao. “CCM haijengwi kwenye majukwaa bali hujengwa kuanzia ngazi ya mashina, huku akibainisha kuwa majukwaa hutumika zaidi kwa ajili ya kutoa hamasa,”amesema Dk.Migiro. Akieleza zaidi amesema uhai na uimara wa Chama hicho unatokana na nguvu ya ngazi za mashina, akisisitiza kuwa ndiko kunakojengwa misingi halisi ya CCM. Aidha ametoa maelekezo kwa viongozi wa ngazi zote kushiriki kikamilifu vikao vya mashina ili kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi na kuimarisha uhusiano wao na wananchi. “Mashina ndiyo moyo wa CCM kwa kuwa ndiyo yanayokutanisha Chama na wananchi moja kwa moja kupitia vika...