Skip to main content

Posts

Showing posts from December 1, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko akiwasili Karimjee Kuaga Mwili wa Ndugulile

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Disemba 02, 2024 akisaini Kitabu cha Maombolezo kwenye msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile. Dkt. Ndugulile alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 27, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Foundation for Disabilities Hope Yapata Ufadhili WA Kuimarisha Uongozi na Demokrasia

Na Hamida Ramadhan- Dodoma Foundation For Disabilities Hope,  (FDH)taasisi isiyokuwa ya kiserikali, imepata ufadhili wa shilingi milioni 40 kwa ajili ya mradi wa kuwawezesha watu wenye ulemavu katika masuala ya uongozi na kukuza demokrasia.  Ufadhili huo umetolewa na shirika la Abilis Foundation yenye ofisi zake nchini Tanzania, mkoani Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Foundation For Disabilities Hope, Michael Salali, alisema mradi huo unalenga kuwafikia watu 300 wenye ulemavu katika wilaya ya Kondoa. “Tunaimani mradi huu umekuja kwa wakati muafaka, hasa baada ya uchaguzi mdogo na kuelekea uchaguzi mkuu.  "Tunataka kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu kujitokeza kuchagua na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi bila kujihisi wanyonge,” alisema Salali. Hata hivyo Tasisi hiyo imeishukuru Abilis Foundation kwa kufanikisha mradi huo muhimu. Kwa upande wake Furaha William, Afisa Habari wa taasisi hiyo, alieleza kuwa mradi huo pia unalenga wanawake na was...

Waziri Kikwete aongoza Matembezi Kuchangia Wenye Ulemavu

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana,ajira na  wenye ulemavu mh Ridhwani Kikwete ameongoza Matembezi yanayojulikana kama Sunset Walk kuunga mkono taasisi inayosimamia haki za wenye Ualbino (TAS) na Lions Club. Matembezi hayo yamelenga kuchangia fedha kusaidia kupatikana kwa mahitaji muhimu kama Mafuta ya Ngozi, kofia kinga n.k .  Katika hotuba yeke Kikwete  amewakumbusha juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali ikiwemo mpango kazi wa kupambania haki za wenye Ulemavu wakiwemo wenye Ualbino utakao zinduliwa hivi karibuni..

Rais Samia Kuunda Tume Mbili Kuchunguza Malalamiko ya Ngorongoro

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Samia Suluhu Hassan ametangaza kuunda tume mbili kuchunguza malalamiko ya wakazi wa Ngorongoro mkoani Arusha. Rais Samia ametangaza uamuzi huo leo Desemba mosi 2024 katika Ikulu ndogo ya Arusha, wakati akizungumza na Viongozi wa jamii ya Kimaasai inayoishi katika eneo hilo la Ngorongoro kwa lengo la kuwasikiliza baada ya kuwepo kwa baadhi ya malalamiko kufuatia uamuzi wa Serikali juu ya eneo hilo. Amesema katika tume hizo mbili atakazoziunda moja itachunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Ngorongoro na nyingine itaangakia itekelezaji wa zoezi zima la uhamiaji kwa hiari kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro. Rais Samia amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea Kuimarisha Utendaji kazi wa Mamlaka ya eneo la Ngorongoro(NCAA) kwa lengo la Kuimarisha Mahusiano kati ta Serikali na Jamii hiyo.  Vilevile amesisitiza Ulazima wa Wananchi Kushirikishwa ipasavyo katika Upangaji na Utekelezaji wa Miradi i...

Serikali imetoa ahadi kubwa kwa vijana Nch

Itaendelea kuboresha na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali imejidhatiti kuweka mazingira yanayowezesha vijana kutoka kwenye uchumi usio rasmi kuelekea uchumi ulio rasmi. “Serikali inaendelea kuimarisha sera zinazowezesha nguvu kazi ya taifa, kuondoa vikwazo vya Kibiurokrasi, kutoa msaada wa kiufundi  na kifedha kwa Vijana” amesema. . Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Novemba 29, 2024 Jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa uchambuzi wa kina wa sekta isiyo rasmi katika biashara zinazoongozwa na Vijana. Aidha, amesema tafiti zilizofanywa sekta zisizo rasmi zitasaidia kupata majawabu ya matatizo ya Vijana katika kukabiliana na changamoto isiyo rasmi. Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkurugenzi  wa Shirikia la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Caroline Mugalla, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE Bi. Suzanne Ndomba na Watafiti Mashuhuri.

Rais Samia akutana na Viongozi wa Jamii ya Kabila la Kimaasai Ikulu Ndogo Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wa kimila wa jamii ya Kimasai (Malaigwanani) wanaoishi Ngorongoro na maeneo jirani katika Ikulu ndogo ya Arusha tarehe 01 Desemba, 2024.