Skip to main content

Posts

Showing posts from April 22, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu: Tuepuke Migogoro na Mizozo

_Asema kuna miradi inakwama utekelezaji sababu ya migawanyiko_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa waepuke migogoro na mizozo kwa sababu kuna miradi inakwama utekelezaji kutokana na migawanyiko. “Twendeni tukatimize wajibu wetu, tuache migawanyiko kwa sababu hayo si matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesisitiza wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika ukumbi wa mikutano wa AICC, jijini Arusha. Ametoa wito huo leo jioni (Jumatano, Aprili 22, 2026) wakati akifungua mkutano huo wa siku mbili ulioanza leo na kusisitiza kuwa waangalie uwezekano wa kuondoa uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti ambao hivi sasa unafanyika kila mwaka. “Tuepuke migogoro, Waheshimiwa Mameya, Madiwani na Wenyeviti; kuna baadhi ya maeneo tunachelewa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa sababu ya migogoro inayotengeneza migawanyiko.” “Ondoeni utaratibu wa kuchagua Mak...

Bilioni 94.1 za Rais Samia, Dhamira ya Kweli ya Kuwainua Kiuchumi Wajasiriamali

  NA: DK. REUBENI LUMBAGALA, TANGA Moja ya ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wake ni kuwawezesha kiuchumi kwa kujenga mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao. Pia, kuwawezesha kimitaji kufikia malengo yao ya kukuza biashara na ustawi wao kwa ujumla. Hakuna ubishi kuwa maendeleo ya nchi yamebebwa kwa kiasi kikubwa na sekta binafsi. Unahitajika ushirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi (Public and Private Partnership - PPP) kufanikisha kasi ya maendeleo nchini. Kwa kutambua umuhimu wa sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi na  maendeleo kwa ujumla, serikali imeanzisha Kituo cha Sekta ya Umma na Binafsi ili kuwezesha utekelezaji wa mipango ya kimaendeleo kwa kuzingatia kuwa wadau hawa wawili - sekta ya umma na binafsi ni muhimu. Wananchi kwa kutambua ukweli kuwa serikalini kuna ajira chache na sekta binafsi ndiyo injini ya maendeleo, kumekuwa na mwamko wa baadhi ya wananchi kujiajiri wenyewe ili kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na kuchangia pato la T...

Tasnia ya Mazao ya Bustani Ni Sekta ya Kimkakati-Dkt. Mwigulu

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa tasnia ya mazao  ya bustani siyo tu sehemu ya sekta ya kilimo, bali ni sekta ya kimkakati ya biashara ya kimataifa inayounganisha Tanzania na Masoko ya Dunia. Amesema kuwa kwa kutambua umuhimu huo, Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa ruzuku ya pembejeo iliyosaidia kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya bustani kutoka tani milioni 7. 5 kwa mwaka 2023/2024 hadi kufikia tani milioni 9. 7 kwa mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 30.2. Amesema hayo leo (Jumatano, Aprili 22, 2026) alipozindua maandalizi kuelekea Jukwaa la Hotikacha la Kimataifa la Biashara na Uwekezaji (Hortilogistica Africa 2026) lenye lengo la kukuza biashara ya mazao ya bustani, hafla hiyo imefanyika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jukwaa la Kilimo wa Dkt. John Samwel Malecela Nzuguni jijini Dodoma. Jukwaa hilo linatarajiwa kufanyika jijini Arusha, Novemba 08 hadi 10, Mwaka huu.  “Ni dhahiri  kuwa wadau wote tukishirikiana katika kuendeleza tasnia hii, ...

Bajeti ya Kimkakati Wizara ya Nishati

 DODOMA. WIZARA ya Nishati imeomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya shilingi trilioni 2.5 kwa ajili ya matumizi ya wizara ya hiyo na taasisi zake katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Hayo yameelezwa leo Aprili 22, 2026 na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma.  Amesema kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 2.4 sawa na asilimia 97.5 ya bajeti yote ya wizara ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo huku shilingi bilioni 63 sawa na asilimia 2.5 ya bajeti ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida. "Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa lijadili na kuidhinisha Bajeti ya jumla ya Shilingi Trilioni Mbili, Bilioni Mia Tano Ishirini na Tano, Milioni Mia Nne na Moja, Mia Moja Ishirini na Tisa Elfu (Shilingi 2,525,401,129,000) kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa mwaka 2026/27". Ameomba Kadhalika waziri Nde...

Dkt. Mwigulu Awasili Mkoani Arusha Kufungua Mkutano wa Alat

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 22, 2026 amewasili mkoani Arusha, ambapo anatarajiwa kufungua mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC)