Skip to main content

Posts

Showing posts from October 15, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ruto Ashusha Bendera za Nchi ya Kenya, Kifo cha Raiila Odinga

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga amefariki akiwa na umri wa miaka 80. Raila amefariki wakati akifanyiwa matibabu katika hospitali moja nchini India. Rais wa Kenya William Ruto ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga. Katika hotuba yake kwa taifa kupitia televisheni, Rais Ruto alimtaja Odinga kama "mzalendo mwenye ujasiri usio wa kawaida." Alisema bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kote nchini Kenya na katika balozi zote za Kenya nje ya nchi. Kama ishara ya heshima, nimeahirisha shughuli zangu zote za umma kwa siku zijazo, na ninawaomba wafanyikazi wengine wote wa umma na viongozi kufanya vivyo hivyo ili tujiunge na taifa katika kipindi hiki cha maombolezo," Ruto alisema. Rais Ruto pia ametangaza kuwa Odinga ataandaliwa mazishi ya kitaifa kwa heshima kamili. Aliongeza kuwa serikali ya India, ambapo waziri mkuu huyo wa zamani alifariki alipokuwa akipokea matibabu, imejitolea kuwezesha kurejeshwa...

Mativila Aagiza Mkandarasi Kufanya Kazi Usiku na Mchana

Rufiji, Pwani  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amemtaka Mkandarasi JUIN Company Ltd anayekarabati barabara ya Nyamwage-Tawi-Kikobo yenye urefu wa Kilomita 56 kwa kiwango cha changarawe wilayani Rufiji mkoani Pwani, kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati. Mhandisi Mativila ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa barabara hiyo ya Nyamwage-Tawi-Kikobo ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 35.  "Mradi huu umechelewa na mvua zinakuja, kwa hali ilivyo mvua zikianza kunyesha kazi zitakuwa hazifanyiki, ninachosisitiza kabla mvua hazijanyesha Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana ili kazi ikamilike kwa wakati, pia naomba TARURA msimamie kwa ukaribu ili barabara hii iweze kupitika”, amesema. Aidha, Mhandisi Mativila amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza fedha za bajeti ya TARURA kutoka Shilingi Bilioni 275 hadi Shilingi Bilioni 700 kwa ajili...

Serikali Yaendelea Kuimarisha Huduma za Ustawi Kwa Wazee

Na Jackline Minja - WMJJWM ;Dar Es Salaam. Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kudumisha huduma bora kwa wazee kwa kuhakikisha kundi hilo linapata huduma za msingi zinazowawezesha kuishi maisha yenye heshima na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu tarehe 15 Oktoba, 2025 wakati wa ziara yake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza cha Tushikamane Pamoja Foundation yaliyopo Kata ya Kwembe, Manispaa ya Ubungo mkoani Dar Es Salaam. Dkt. Jingu amesema wazee ni sehemu ya taifa kwakua wamelitumikia kwa muda mrefu kwa uaminifu na kujitolea hivyo jamii ya Watanzania wana wanawajibu wa kuwasaidia na kuwaenzi wazee kama ishara ya kuthamini mchango wao kwa maendeleo ya nchi. “Lengo la kuwatembelea ni kuwaona kuwajulia hali na kuendelea kuwaenzi pamoja na kuthamini mchango wenu mkubwa katika ku...

Mgombea Ubunge Jimbo la Kyerwa Ampa Tano Dkt Samia

  Na Angela Sebastian; Karagwe  Mgombea ubunge wa jimbo la Kyerwa kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Khaldi Mussa Nsekela amemshukuru Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi bilioni 84 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Kyerwa tangu alipoingia madarakani. Nsekela ametoa shukrani hizo leo katika mkutano mkubwa wa kunadi Ilani ya CCM na kuomba kura za mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan uliofanyika uwanja wa Kayanga Wilayani Karagwe. Amesema Dk.Samia hana deni kwa wana Kyerwa bali wao ndio wanapaswa kulipa shukrani kwa kumpigia kura nyingi ifikapo Oktoba 29 mwaka huu. "Wanakyerwa wanasema wanasubiri wakati ufike wakupigie kura za kutosha kutokana na sababu zifuatazo ambazo ni pamoja na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya Elimu,Afya,maji na Umeme ambayo imegharimu sh.bil 84 na kupanda kwa bei ya zao la kahawa kutoka sh.1000 hadi 8000 kwa kilo"anasema Nsekela  Anasema Ilani ya CCM imesheheni mambo mengi mazuri y...

Tanzania Yazindua Mradi wa Dunia Kukabiliana na Magonjwa ya Mlipuko na Dharura za Kiafya

📌 Dkt. Biteko ataka utekelezaji wa kuleta matokeo chanya 📌 Mradi kugharimu Dola za Kimarekani milioni 38.7 📌 WHO, FAO, UNICEF na Pandemic Fund zaipongeza Tanzania   Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua Mradi wa Dunia wa kukabiliana na magonjwa ya Mlipuko nchini na kuzitaka wizara zote tawala za mikoa na serikali za mitaa pamoja na taasisi kutekeleza shughuli za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na dharura za kiafya. Dkt. Biteko ametoa agizo hilo Oktoba 15, 2025 jijini Mwanza na kusema mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 38.7 unalenga kuboresha huduma za afya kwa watanzania na kuchochea maendeleo ya nchi. Amesisitiza kuwa wizara, taasisi na washirika wa maendeleo wanatakiwa kusimamia utekelezaji katika uwekezaji huo na kuhakikisha yanapatikana matokeo chanya kama ilivyokusudiwa. “Wizara zote, Tawala za mikoa na Taasisi , tekelezeni shughuli zote za kipaumbele...