Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Sillo ametoa tracksuit 25 za mazoezi kwa wanafunzi mbalimbali wa shule za msingi waliopo kwenye kambi ya maandalizi ya mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya mkoa na baadaye taifa. Kambi hiyo ya maandalizi imewekwa katika Shule ya Msingi Dareda kati wilayani Babati, ambapo wanafunzi hao wanaendelea kujifua kwa ajili ya kuiwakilisha Halmashauri ya Wilaya ya Babati katika mashindano hayo muhimu ya michezo na sanaa. Tracksuit hizo zimekabidhiwa kwa niaba ya mbunge huyo na Katibu wa Mbunge, Waziri Juma, ambaye amewatakia kila la heri wanafunzi hao wanapojiandaa kwenda kushindana na wenzao kutoka halmashauri mbalimbali za mkoa na taifa. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Waziri Juma amesema Mheshimiwa Sillo anaendelea kuthamini michezo kama sehemu muhimu ya kukuza vipaji vya watoto, kuimarisha afya pamoja na kujenga nid...
Marato tv - Sauti ya Jamii