Skip to main content

Posts

Showing posts from August 26, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Nina deni kubwa la kuijenga Korogwe mpya-Njama

📍 Aishukuru Kamati Kuu ya Halmashauri ya Kuu ya CCM Taifa kwa kumteua kuwa mgombea  Na Mwandishi Wetu, Korogwe MGOMBEA wa kiti cha ubunge Jimbo la Korogwe Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Charles Njama amesema dhamana aliyopewa kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyang'anyiro cha ubunge, ni deni kubwa kwake la kuleta maendeleo mjini Korogwe. Akizungumza tarehe 26/8 katika ofisi za chama hicho zilizopo eneo la Majengo mjini hapa mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea ubunge na msimamizi wa uchaguzi Elinlaa Kivaya, Njama alisema anaishukuru Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kwa kumuamini na kurejesha jina lake ili agombee ubunge katika Jimbo hilo. "Naishukuru Kamati Kuu, Kamati ya Siasa mkoa, Kamati ya Siasa wilaya na wajumbe walionichagua, kwa kujenga imani na Mimi kati ya wenzangu Saba kupeperusha bendera ya chama, Mimi siyo mshindi kilichoshinda ni chama," alisema. Njama alisema imani aliyopewa na chama ni deni kubwa ambalo lipo moyoni m...

Kibaki na Raila Walivyorarua Katiba ya Kenya 2010

  RAIS wa tatu wa Kenya hayati Mwai Kibaki na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga walipuuza vipengele muhimu vya Katiba ambayo ilikusudiwa kuunda kaunti 14 pekee, na badala yake wakaongeza kaunti hizo hadi 47 . Ufichuzi huu umetolewa na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula katika mahojiano na Vyombo vya habari kuhusu miaka 15 tangu kupitishwa kwa Katiba ya 2010, ambapo alisema kuwa huu ni wakati mwafaka wa kuibadilisha. Kwa mujibu wa Bw Wetang’ula, kwenye rasimu ya awali ya Bomas, Wakenya walikuwa wamekubaliana kuhusu maeneo 14 ya kiutawala. Katika mpango huo, maeneo ya Magharibi, Nyanza na Kati yangegawanywa kila moja kuwa Kaunti mbili, Bonde la Ufa na Mashariki kuwa vitatu kila moja, huku Pwani ikibaki kama eneo moja. Nairobi ilikuwa imeorodheshwa kama eneo la kipekee kwa hivyo halingekuwa sehemu ya serikali ya ugatuzi wala serikali kuu, bali lingekuwa kitovu huru cha serikali ya kitaifa ambapo vitengo vingine vingeshughulikia masuala ya kitaifa. “Huo ungekuwa mpango mzuri s...

Balozi Dkt Nchimbi Amkabidhi Ofisi Dkt Migiro

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt,Emmanuel John Nchimbi ambaye kwa sasa ni Mgombea Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akimkabidhi nyaraka Katibu Mkuu mpya wa chama hicho Balozi Dkt.Asha Rose Migiro wakati wa makabidhiano rasmi ya Ofisi, yaliyofanyika leo Jumanne Agosti 26, 2025, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

Dkt. Doto Biteko Achukua Fomu Kugombea Ubunge Jimbo la Bukombe

📌 Wanachama zaidi ya 1000 wajitokeza kumdhamini 📌 Dkt. Biteko ahimiza Kampeni za kistaarabu, mshikamano na upendo 📌 Awaomba Wana Bukombe kumchagua Dkt. Samia, Biteko na madiwani wa CCM Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukombe, Zedekiah Solomon Osan amemkabidhi fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Agosti 26, 2025 katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bukombe - Mkoani Geita. Makabidhiano hayo ya fomu ni utekelezaji wa ratiba kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka 2025 Aidha, Maelefu ya wana CCM na wapenzi wa chama hicho wamemsindikiza mgombea kwa ajili ya kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa na Tume huru ya Uchaguzi. Katika hali isiyo ya kawaida, zaidi ya wanachama 1000 wamejotokeza kumdhamini Dkt. Biteko ikilinganishwa na mahitaji ya wadhamini 31 waliohitajika kisheria. Akizungumza na wanaCCM katika viwanja Ofisi ya ...

Waziri Mkuu Alipongeza Jeshi la Magereza Urasimishaji Ujuzi Kwa Wafungwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amelipongeza Jeshi la Magereza Tanzania kwa kufanya urasimishaji wa ujuzi wanaoupata wafungwa kupitia VETA na kuwawezesha kupata ajira au kuanzisha biashara zao baada ya kumaliza kifungo. Ameongeza kuwa kupitia mitaala mipya ya mafunzo ya amali na stadi za kazi, jeshi hilo limefanikiwa kuwanufaisha zaidi ya wafungwa 5,000 ambapo baadhi yao wameweza kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza vifungo vyao. Ametoa pongezi hizo leo Jumanne (Agosti 26, 2025) wakati aliposhiriki katika maadhimisho ya kilele cha miaka 64 ya Jeshi la Magereza Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam. “Ninatoa pongezi za dhati kwa jeshi la magereza kwa mafanikio haya, huu ni mpango kazi wenu, na tumeona faida na vijana hawa waliokuja hapa wameeleza namna ambavyo wamenufaika na kazi hizi” Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini amelipongeza Jeshi la Magereza kwa wepesi katika kutafsiri na ...

Rais Mstaafu Kabila Aombewa Adhabu ya Kifo

Waendesha mashtaka wa kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamemuombea hukumu ya Kifo rais wa zamani wa nchi hiyo Joseph Kabila kwa tuhuma za uhaini na kushirikiana na kundi la waasi la AFC/M23. Anashtakiwa kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa na vuguvugu la M23, na njama ya kupindua serikali. Wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya Ijumaa, mji mkuu Kinshasa, Waendesha mashtaka pia uliomba mali zake zote zichukuliwe. Kabila, ambaye hakufika mahakamani, hajatoa tangazo lolote la umma mara moja kuhusu  hukumu ya kifo aliyoombewa. Hata hivyo Jumamosi kupitia jukwaa lake la X, Kabila alisema: ''Iwe Mashariki wala Magharibi haitaweza kutugeuza kutoka kwa njia yetu.  Watu wa Congo hawatavumilia tena udikteta au udhalimu uliotokana na uchoyo. Mwisho wako tayari umeandikwa, kama jua linalotua kila jioni kwenye upeo wa macho. Kwa maana mapenzi ya watu waliosimama imara yana nguvu kuliko nguvu zote kwa pamoja''. Baadhi ya vyombo vya habari na baadhi y...

Kasi ya ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani madini yaongezeka nchini Tanzania

  ☑️Waziri Mavunde aweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Kusindika na Kuyeyusha Nikeli na Shaba - Dodoma ☑️Ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia kuyaongezea thamani madini ndani ya nchi. ☑️ Mradi kuchakata takribani tani  200,00 za nikeli na Shaba kwa mwaka 📍Dodoma, Tanzania  Serikali imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania kupitia uongezaji thamani ndani ya nchi ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi wa kijani (green economy)  hususan katika utengenezaji wa magari ya umeme, betri za magari, nishati safi na vifaa vya kielektroniki. Hayo yamewekwa wazi leo Agosti 26, 2025 na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony  Mavunde, wakati akiweka jiwe la msingi la Kiwanda cha kusafisha na kusindika Madini ya Nikeli na Shaba kinachojengwa na Kampuni ya Zhongzhou Mining Co. Ltd, eneo la Zamahero, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma. Amesema kuwa, Mradi huo utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Su...