MSALALA, SHINYANGA Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ameielekeza Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kuhakikisha inatekeleza kwa wakati mapendekezo yote yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akisisitiza kuwa hatua hiyo itaimarisha uwajibikaji, uwazi na matumizi sahihi ya rasilimali za umma. Mhe. Mhita ametoa maelekezo hayo leo, Julai 8, 2026, wakati akifungua Baraza Maalumu la kujadili na kupitia hoja za ukaguzi wa CAG kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30, 2026, lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala. Amesema utekelezaji wa hoja za CAG si suala la hiari, bali ni wajibu wa kila taasisi ya umma kuhakikisha dosari zilizobainishwa zinarekebishwa kwa wakati ili kuongeza ufanisi wa usimamizi wa fedha za Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi. "Hoja za CAG zinapaswa kutazamwa kama fursa ya kuboresha utendaji wetu. Hakikisheni kila hoja inafanyiwa kazi kwa wakati na kufungwa kwa mujibu wa taratibu," amesis...
Marato tv - Sauti ya Jamii