Skip to main content

Posts

Showing posts from February 13, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rasi Mwinyi: Zanzibar itaendelea kuimarisha ushirikiano na Romania

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kuimarisha Ushirikiano na Romania katika nyanja mbalimbali za Maendeleo  na Kiuchumi. Rais Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Balozi wa Romania nchini Tanzania , Mhe.Gentiana Serbu aliyefika Ikulu Zanzibar kuonana naye. Aidha Rais Dkt.Mwinyi amemuelezea Balozi Gentiana kuwa  yapo Maeneo mengi ambayo hizo zinaweza kushirikiana ikiwemo Elimu , Afya, Mafuta na Gesi , Usimamizi wa Maafa na  Udhibiti wa Taka Kitaalamu pamoja na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Akizungumzia suala la Mazingira Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa  Zanzibar inakabiliwa na tatizo kubwa  la Taka  za plastiki zinazotishia Uhai wa Viumbe vya Baharini na Ustawi wa Sekta ya Utalii na kuiomba Romania kulizingatia eneo hilo. Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amevikaribisha Vyuo Vikuu vya Romania kuja nchini kuangalia maeneo ya Ushirikiano na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA). Vilev...

Balozi Dkt Nchimbi Amesema Ccm Itaendelea Kuimarisha Ushirikiano Wa Ndani na Nje Ya Nchi

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza dhamira yake ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa ndani na kimataifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.  CCM ambacho ni chama tawala nchini kimeeleza kuwa kitasimamia Serikali ili kuendeleza uhusiano mzuri na mataifa na taasisi mbalimbali, ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, alipokutana kwa nyakati tofauti na mabalozi wa Korea Kusini, Norway na Uingereza katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi, tarehe 13 Februari 2025. Katika mazungumzo yake na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Ahn Eunju, Balozi Nchimbi alisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Korea Kusini, hasa katika nyanja za maendeleo ya kiuchumi na teknolojia.  Kwa sasa, Tanzania inanufaika na mkopo nafuu wa...

Maelfu ya Wananchi Wajitokeza Sirari Mkutano Wa John Heche

 Makamu Mwenyekiti Taifa Mh John Heche akizungumza na wananchi wa kata ya Sirari Jimbo la Tarime Vijijini leo