Serikali imewahakikishia wananchi kuwa ina dhamira ya dhati ya kutekeleza mpango wa bima ya afya kwa wote, na kutoa wito kwa washiriki wa kongamano la mpango wa bima ya afya kwa wote na mdahalo wa kitaifa kuhusu ufadhili wa sekta ya afya kuja na mapendekezo yatakayosaidia kutimiza dhamira hiyo. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) wakati anafungua matukio hayo mawili yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha jijini Arusha Oktoba 30, 2024. Matukio hayo yanayofanyika kwa siku nne hadi Novemba 1, 2024 yamekusanya wadau wa afya kutoka ndani na nje ya nchi ili kwa pamoja kujadili mikakati na mbinu bora zitakazoiwezesha Serikali kuwa na mipango endelevu ya kuhakikisha kuwa kila mwananchi, anakuwa na bima ya afya itakayomwezesha kupata matibabu bila kuangalia kipato chake. Waziri Mkuu ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali katika hafla hiyo ya ufunguzi, wakiwemo Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama (Mb),...
Marato tv - Sauti ya Jamii