Skip to main content

Posts

Showing posts from November 27, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mnada wa Madini ya Vito Waongeza uwazi na kudhibiti utoroshaji nchini

Arusha, Novemba 27, 2025 Sekta ya madini inaendelea kunufaika na mageuzi ya kidijitali, baada ya mfumo wa mnada wa madini ya vito kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) kuonyesha matokeo chanya katika kuongeza uwazi, ushindani na kudhibiti utoroshaji wa madini nchini. Akizungumza katika mnada wa tatu wa madini ya vito uliofanyika katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, CPA Venance Kasiki, amesema mfumo huo umeleta mapinduzi katika namna wafanyabiashara wanavyonunua madini. Kasiki amesema kupitia TMX, ununuzi unafanyika kwa njia ya kidijitali na kwa uwazi mkubwa ambapo washiriki wote wanaona hatua kwa hatua mwenendo wa bei, hatua inayotofautiana na utaratibu wa zamani wa matumizi ya bahasha ambao haukuwa na uwazi wa kutosha. Ameeleza kuwa mageuzi hayo yameongeza hamasa kwa wafanyabiashara kushiriki kwa wingi katika minada, huku Serikali ikipata mapato halali na wauzaji wakipata bei stahiki. “Mfumo huu unaimarisha uwazi...

Vijana 423 wa Mirerani & Lemishuku Wakabidhiwa Leseni Kupitia Mradi Wa Mbt

  ▪︎ Ahadi ya Mhe. Rais Dkt. Samia kugawa leseni kwa vijana wachimbaji wa madini ya vito imeanza kutekelezwa Lemshuku na Mirerani ▪️ Ni leseni mpya za uchimbaji na ufanyaji biashara madini ▪️Utafiti wa madini kwa kutumia ndege nyuki kuanza mwezi Februari, 2026 Simanjiro ▪️Wachimbaji wadogo waapa kulinda amani ya nchi *Simanjiro,Manyara* Serikali imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika uchumi wa madini kupitia programu jumuishi ya Mining for Better Tomorrow (MBT), inayolenga kuwawezesha vijana na wanawake kunufaika moja kwa moja na rasilimali za taifa. Dhamira hiyo imesisitizwa leo, Novemba 27, 2025, na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, wakati akizungumza na mamia ya wachimbaji wadogo vijana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Lemshuku, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara. Akizungumza kwa msisitizo, Waziri Mavunde amesema anataka kuona uchumi wa madini nchini ukimilikiwa na Watanzania wenyewe, na kwamba Tanzania inakuwa ...

Katibu Mkuu CCM Aongoza Kikao cha Sekreterieti

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro akiongoza Kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, leo Alhamis, tarehe 27 Novemba 2025, Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Zanzibar. 

Vijana Kyela Kufanya Kazi Saa 24 – Waziri Nanauka

Na: OR - MV, Kyela Vijana wa Wilaya ya Kyela wameshukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kuondoa zuio la wananchi kuacha kufanya kazi ifikapo saa 6 usiku kufuatia matukio ya baada ya uchaguzi mkuu ambapo kuanzia leo wananchi wanaruhusiwa kufanya kazi masaa 24. Kauli hiyo ya Serikali imekuja ikiwa ni mafanikio ya ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka mara baada ya kuzungumza na vijana katika mkutano uliofanyika Soko la Kyela leo (27 Novemba 2025) baada ya vijana kuwasilisha malalamiko hayo. Waziri Nanauka alitoa fursa ya vijana kutoa mawazo na maoni yao ambapo Saimon Charles alieleza kuwa kufuatia maandamano na vurugu za baada ya uchaguzi mkuu Serikali iliweka zuio la wananchi kufanya shughuli baada ya saa sita usiku hali ambayo imepelekea vijana hususan waendesha pikipiki na biashara ndogondogo kukosa kazi. “Hapa Kyela kulala mwisho saa 6 usiku tunashindwa kujiachia, Polisi wanashinda barabarani kutuzuia na kutukamata hatua inayo...

Dkt. Mwigulu Aongoza Kikao cha Kazi cha Wakuu wa Mikoa

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 27, 2025 ameongoza kikao cha kazi cha Wakuu wa Mikoa Tanzania bara, kikao hicho kimefanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.

Tanzania Yashiriki Mkutano wa Pamoja wa Mabaraza Matatu ya EAC

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshiriki mkutano wa Pamoja wa Baraza la Mawaziri la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa, Baraza la Mawaziri wa Nishati na Baraza la Mawaziri wa Viwanda, Biashara, Fedha na Uwekezaji ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika kwa njia ya mtandao Novemba 27, 2025 jijini Dodoma.  Mkutano huo, pamoja na masuala mengine umeainisha miradi ya kielelezo ya miundombinu kutoka nchi Wanachama, kujadili na kupitisha ajenda zinazotarajiwa kujadiliwa katika Mkutano Kazi (Retreat) wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa EAC utakaofanyika hivi karibuni.  Mkutano huo utajadili na kupitisha miradi ya Miundombinu ya Kimkakati ya Kikanda ambayo utekelezaji wake utapewa kipaumbele kwa kutafutiwa ufadhili wa rasilimali fedha. Kwa upande wa Tanzania mkutano huo umehudhuriwa na naibu wawaziri kutoka sekta mbalimbali wakiwawakilisha Mawaziri, akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. James Kinya...