Skip to main content

Posts

Showing posts from November 6, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Vi Agroforesty laandaa maonesho ya kilimo misitu

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Maendeleo la Kiswidishi linalotekeleza miradi ya maendeleo nchini kwa kushirikiana na wabia mbalimbali Vi Agroforesty limeandaa maonesho ya 10 ya kilimomisitu yanayotarajiwa kufanyika mjini Musoma. Meneja Mkazi wa shirika hilo nchini Martha Olotu aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo muhimu linaadhimisha miaka 15 ya mafanikio katika matumizi endelevu ya ardhi, usalama wa chakula na ustahimilivu dhidi  ya mabadiliko ya tabia nchi. Alisema maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15 Novemba mwaka huu katika kituo cha mafunzo cha kilimomisitu kilichoko Bweri Musoma na yanatarajiwa kuwaleta pamoja washiriki 6,000. Alisema chini ya kauli mbiu ya ‘kilimomisitu kwa ukuaji jumuishi na endelevu’ maonesho hayo yatakuwa jukwaa la kitaifa la kubadilishana maarifa, mijadala ya kisera, na kuhamasisha ushirikiano wa pamoja . Olotu alisema maonesho hayo yatawakutanisha wakulima, watafiti, watunga sera, wabia wa maendeleo, na sekta binafsi ili kuha...