Skip to main content

Posts

Showing posts from August 27, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ingawa bado muda CCM imeonesha ukubwa wake

Maelfu kwa mamia ya wananchi wameendelea kufurika kwenye viwanja vya Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam tayari kumsikilizia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan na,  Mgombea Mwenza Dkt. Emanuel John Nchimbi ambao pamoja na kuhutubia mkutano huo pia watatambulishwa rasmi kwa wananchi  na wapiga kura wa Dar es Salaam na nchi nzima.

Mndolwa Awafunda Watumishi Wapya

📍 *NIRC Dodoma.*  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Bw. Raymond Mndolwa, amewataka watumishi wapya wa NIRC kutumia maarifa na ujuzi walionao ili kufanikisha malengo ya Tume na kuzingatia uadilifu katika utendaji.  Amesema kila mtumishi ana nafasi ya kipekee katika utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo, hivyo ni muhimu kuelewa kanuni na taratibu za utumishi wa umma, kuwa na maadili na uadilifu kwa maslahi ya Taifa.  Akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo Elekezi kwa watumishi wapya wa NIRC walioajiriwa na Serikali hivi karibuni Mndolwa amesema mafanikio ya Tume yanategemea mshikamano, weledi na utendaji bora wa kila mmoja kwa kuzingatia maadili na uadilifu.  Amefafanua kuwa kila mtumishi anapaswa kutambua kuwa kazi yake ni sehemu ya mchango mkubwa unaolenga kuboresha kilimo nchini kupitia miradi ya umwagiliaji.  “Tunaposhirikiana na kutumia ujuzi wetu kwa ubora, tunachangia moja kwa moja maendeleo ya kilimo na na kuleta tija kwa taifa. Ki...

Msama Akanusha Kuhamia Chauma

*TAARIFA KWA UMMA*   *Kukanusha Taarifa za Uzushi Kuhusu Kuhama CCM kwenda Chauma* Ndugu Watanzania, Kumekuwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya majukwaa ya kijamii zikidai kwamba mimi, Alex Msama, nimejiunga na chama cha Chauma na kwamba ninatarajia kugombea ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia chama hicho. Napenda kuwataarifu kwa uwazi na msimamo thabiti kwamba taarifa hizo ni za uongo, hazina msingi wowote, na ni uzushi wenye nia ovu ya kunichafua kisiasa na kijamii. Mimi ni mwanachama mwaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Sijawahi kufikiria, kuwaza, wala kupanga kuhama CCM. Historia yangu binafsi, imani yangu ya kisiasa, na mchango wangu katika chama hiki ni sehemu ya maisha yangu na misingi ninayoisimamia.   Nawaomba Watanzania wote wapuuze taarifa hizo za kupotosha, na waendelee kuwa na imani na uongozi wa CCM pamoja na dhamira yangu ya kukitumikia kwa uadilifu na uzalendo chama changu CCM. Aidha, nitachukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya...

MwanaFA arejesha fomu INEC, asema mwaka huu CCM itafanya kampeni bab'kubwa

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Muheza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA, jana amerejesha fomu yake ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi Jimbo hilo na kusema mwaka huu chama hicho kitafanya kampeni ili kusaka kura nyingi za mgombea Urais wa Chama hicho Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu yake kwa msimamizi wa Jimbo Serapion Bashange, alisema kuwa amehitimisha zoezi la kuchukua fomu ya kuomba uteuzi wa tume hiyo lakini amewashukuru Wana-CCM wa Muheza kwa kumuunga mkono miaka mitano iliyopita lakini pia Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kwa kumteua tena kuwa mgombea wa Chama hicho katika Jimbo hilo. "Nawashukuru Wana-Muheza kwa kuniunga mkono miaka mitano iliyopita tumefanya mambo makubwa ya maendeleo, imani mlionipa kwa kunichagua kwa asilimia 91 ni deni kubwa ambalo nawahakikishia ninakwenda kulilipa kwa vitendo baada ya uchaguzi Mkuu Oktoba 29,"  alisema. MwanaFA amemaliza ubunge akiwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,...

Waziri Mkuu atoa wito kwa watunza kumbukumbu nchini

_▪️Awataka wazingatie maadili, wadumishe uadilifu na kulinda usiri wa taarifa_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa watunza kumbukumbu wote nchini kuzingatia maadili ya kazi, kudumisha uadilifu na kulinda usiri wa taarifa zote zinazohifadhiwa kwani taarifa hizo ni nyenzo muhimu ya usalama wa Taifa na maendeleo ya nchi. Amesema kuwa Chama Cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) kinabeba dhamana kubwa ya kuhakikisha nyaraka na kumbukumbu zote muhimu za Serikali pamoja na taasisi binafsi zinatunzwa kitaalamu na zinahifadhiwa. Ametoa wito huo leo Jumatano (Agosti 27, 2025) wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. “Utunzaji sahihi wa nyaraka na kumbukumbu ni uti wa mgongo wa uwajibikaji, historia, na utawala bora. Bila masjala madhubuti, Taifa letu lingeweza kukabiliwa na changamoto kubwa za upotevu wa taarifa, ucheleweshaji wa ma...