Iringa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi-Tamisemi anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinasimamia kikamilifu zoezi la usafi wa barabara, akisisitiza kuwa serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo muhimu. Mhandisi Mativila amesema hayo mkoani Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Wenda–Mgama Km.19 inayojengwa na TARURA kupitia mradi wa RISE kwa gharama ya shilingi bilioni 29.7 ambayo imefikia asilimia 99 ya utekelezaji. Mhandisi Mativila amesema usimamizi mzuri wa barabara unahitajika ili kuhakikisha barabara hizo zinadumu na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi. "Ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha kuwa barabara hizi zinatunzwa, hasa kwa kuhakikisha zinaendelea kuwa safi na salama kwa matumizi. Hili ni jukumu la pamoja,” amesema Mativila. Ameongeza kuwa uwepo wa barabara bora unachochea shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kuwawezesha wananchi kusafirisha bidhaa na hudu...
Marato tv - Sauti ya Jamii