Skip to main content

Posts

Showing posts from December 16, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Afungwa Miaka 30 Jela kwa kubaka

  Mkazi wa Nkalalo wilayani Kiwmba mkoani Mwanza, Nicholaus James (21) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa kidato cha nne (jina linahifadhiwa) wa Sekondari ya Taro wilayani humo. Katika kesi hiyo ya Jinai namba 22882/2024, James ametiwa hatiani na Mahakama ya wilaya Kwimba kwa kosa la kumbaka binti ambaye utambulisho wake unahifadhiwa kwa sababu za kisheria (19) mwanafunzi wa kidato cha 4 shule ya sekondari Taro. Hukumu hiyo ilisomwa jana tarehe 16.12.2024 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kwimba, John Jagadi mbele ya mwendesha mashtaka wa Serikali Juma Kiparo. Awali, Mwendesha Mashtaka aliieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 07.08.2024, katika Kijiji cha Nkalalo, wilaya ya Kwimba na mkoa wa Mwanza kinyume na vifungu vya 130(1)(2)(a) pamoja na kifungu cha 131(1) cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya sheria marejeo ya mwaka 2022. Mshtakiwa alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 14.08.2024 ...

John Billy Tendwa Baba wa Demokrasia Tanzania amefariki Dunia

Chigaitan mapinduzi vijijini JOHN BILLY TENDWA, Msajili wa zamani wa vyama vya siasa, Aliyepata Mafanikio makubwa katika kuimarisha, kudumisha na kuendeleza ustawi wa Demokrasia nchini Tanzania amefariki dunia katika hospitali ya Muhimbili leo.  John Billy  Tendwa alikuwa Msajili wa vyama kwa miaka  (2001-2013) akichukua nafasi ya Jaji George Bakari Liundi mwanzilishi wa vyama vya siasa 1992 mpaka 2001 na Tendwa kuja kuvistawisha.  Chigaitan mapinduzi vijijini mara ya mwisho amekutana na John Billy Tendwa 2019 kanisa la Mt. Joseph kwenye misa ya kwanza. John  ni miongoni mwa wakatoriki safi nchini Tanzania na mfano mkubwa kwa vijana wa leo.  Nikisema Mkatoriki Safi maana yake alipenda sala maisha yake yote can you imagine umri wa John Tendwa hakosi ibada za Kanisa tena uwapo Kanisani Sauti yake inasikika ikiimba sala za kumtukuza Mungu huyu alikuwa binadamu wa kipekee katika Sala.  John Billy  Tendwa alifanya mabadiliko makubwa kwenye ofisi ya Msa...

Mawakili wa Serikali wajinoa kwa kesi za uchaguzi wa serikali za mitaa

  Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akifungua mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kuhusu Sheria na Taratibu za Uendeshaji wa Mashauri ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yaliyofanyika mkoani Morogoro. Mkurugenzi wa Idara ya Madai, ndugu Mark Mulwambo akitoa salamu za Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa niaba ya Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kuhusu Sheria na Taratubu za Uendeshaji wa Mashauri ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yaliyofanyika mkoani Morogoro. Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Robert Makaramba akitoa mada kuhusu uelewa wa jumla wa sheria zinazosimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania   wakati wa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kuhusu Sheria na Taratibu za Uendeshaji wa Mashauri ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Mwenyekiti wa CCM Simiyu afanikisha kupatikana milioni 33.2 za maendeleo ya kanisa

  Ni mwana Mama Shemsa Mohamed,apewa hati ya pongezi Kanisa KKKT lamshukuru jinsi alivyojitoa kufanikisha harambee hiyo Na Mwandishi wetu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Bi Shemsa Mohamed ameungana na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika harambee ya kuchangia maendeleo ya kanisa hilo. Katika harambee hiyo imelega kuchangia ujenzi wa hosteli na uzio wa kanisani,ikiwa ni hatua muhimu katika kuboresha miundombinu na usalama wa kanisa wa hilo. Akishiriki katika tukio hilo, Mwenyekiti Shemsa Mohamed, pamoja na wadau wengine, wamefanikiwa kuchangia kiasi milioni 15,000,000 kati ya TSh 33,200,000 zilizokusanywa kwenye harambee hiyo.  Mchango wake ulipongezwa kwa kuwa ni mfano wa kujitoa kwa dhati kusaidia taasisi za dini na jamii kwa huku viongozi wa kanisa wakintaja kama kiongozi wa mfano. Akizungumza wakati wa harambee hiyo,mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed amesisitiza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano kati...

Rais Samia afanikisha Upatikanaji wa fedha za Mradi Mkubwa wa Maji Jijini Dar es salaam

*wizara ya maji yanufaika na ziara ya rais samia korea Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema ziara iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan nchini Korea Kusini imetengeneza mahusiano mazuri na kuchangia kupatikana kwa fedha kwa ajili ya mradi mikubwa wa maji safi na usafi wa mazingira. Akizungumza Mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Mfumo wa Kutibu Majitaka Katika Jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya Ziara ya Waziri Aweso na timu nzima ya sekta ya Maji Nchini Korea Kusini. Aidha Waziri Aweso amesema "baada ya kupata nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya Korea Kusini kwa muda mfupi sana baada ya kumaliza na mimi nimepata nafasi hivi karibuni kwenda haijafika hata wiki tumepata zaidi ya dola za kimarekani zaidi ya milioni 240  kwa ajili ya uwekezaji kwenye maji taka” Ameongeza kuwa hiyo inathibitisha mahusiano mazuri na urafiki wa thamani uliopo baina ya nchi hizi mbili  ikichangiwa na ziara ya Rais...

Mkuu wa Mkoa Manyara aweka Jiwe la Msingi Nyumba za Waathirika wa Maporomoko

 Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga,ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa nyumba 109 za waathirika wa maporomoko ya matope yaliyotokea Desemba 3, 2024 Wilayani Hanang Mkoani Manyara. Wakati akiweka jiwe hilo amewataka wanufaika wa nyumba hizo kuzitumia vizuri na kuzitunza kwa manufaa yao na vizazi vijavyo viweze kunufaika. Pia RC Sendiga kwa niaba ya Wananchi wa wilaya ya Hanang' ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajengea nyumba hizo. Sambamba na hilo, RC Sendiga, ametembelea na kukagua ujenzi wa shule ya Msingi Warret inayojengwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 564, Zahanati ya kijiji cha Dawar inayojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 75,000,000., Stendi ya mabasi Katesh inayojengwa kwa shilingi bilioni 5.6 na Kituo cha Afya Gisambalang ambacho kinajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 500. Akihitimisha ziara yake ya ukaguzi wa miradi hiyo RC Sendiga amewaagiza Viongozi wa w...

Rais Mwinyi akutana na Tume ya Maboresho ya Kodi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Tume ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Maboresho ya Kodi, Ikulu Zanzibar iliyofika kujitambulisha. Katika mazungumzo na Tume hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Balozi Ombeni Sefue na ujumbe wake, Rais Dk. Mwinyi wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo mapendekezo yatakayozishauri Serikali mbili za SMZ na SMT kuhusu masuala ya kodi. Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuteua Tume hiyo na kueleza kuwa itasaidia kuimarisha na kubadilisha mifumo ya kodi kwa Serikali zote mbili za SMZ na SMT.

Benki Kuu ya Tanzania Yaainisha Sababu za Kuimarika Kwa Shilingi

  Benki kuu ya Tanzania(BOT) imebainisha  sababu mbalimbali zilizochangia kuimarika Kwa Shilingi kuwa ni pamoja na usimamizi mzuri wa Sera ya Fedha ambapo katika robo ya 4 ya mwaka 2024, BoT ilitangaza riba ya asilimia 6 ili kupunguza ukwasi wa shilingi zilizokuwa nje ya shughuli za kiuchumi.  Akizungumza na GMTV,Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba ametaja Sababu nyingine kuwa ni Kudhibitiwa Kwa magendo katika soko la fedha za kigeni (fx black market) na kupunguza uwezekano wa kununua fedha za kigeni zinazohodhiwa kwa ajili ya kuziuza baadaye kwa bei ya juu (fx speculation) BoT pia imeendelea kudhibiti Taasisi za Serikali, wafanya biashara na watu binafsi kutoza au kuuza bidhaa na huduma za ndani kwa kutumia fedha za kigeni ili kupunguza mahitaji yasiyokuwa ya lazima ya fedha za kigeni nchini, kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha sheria ya BoT.  Aidha Kumekuwepo na Ongezeko la mauzo nje (dhahabu, korosho, kahawa, mchele, mahindi, ufuta, mbaazi, dengu, choroko, n.k); kuongezek...

Tuwainue wabunifu wazawa kuŵainua kimataifa - Dkt.Biteko

 *📌 Asisitiza Mifumo iboreshwe kuakisi Maendeleo* *📌 Serikali kuweka Mazingira wezeshi kwa wadau wa STARTUPs* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa pamoja na jitihada za kuwainua wabunifu wawekezaji nchini, bado kuna umuhimu mkubwa wa kuwawezesha wabunifu wetu kukua zaidi ndani na nje ya mipaka ya nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Desemba 16, 2024 Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la Uwekezaji wa Kampuni Bunifu (STARTUPs) Amesema kuwa Tanzania imerekebisha mifumo mingi ili kuwezesha ubunifu na uwekezaji wa moja kwa moja nchini kuleta maendeleo, suala ambalo tumeona likifanikiwa na kwahiyo linahitaji kupaliliwa na kuungwa mkono kwa matokeo chanya. “Nimewasikiliza wanakongamano na kupitia majadiliano haya ni wazi kwamba bado kuna namna ya kuboresha zaidi mifumo yetu ya usimamizi na utawala ili kuhakik...

Wadau wa Mazingira Wakutana Kujadili Namna ya Kutokomeza Majanga Kwenye Makazi duni

Tatizo la uchafuzi wa mazingira ikiwemo utiririshaji wa maji taka kutoka kwenye makazi yaliyoko kwenye maeneo ya miinuko Jijini mwanza kwenda kwenye ziwa victoria limepungua baada ya baadhi ya wananchi waishio kwenye maeneo hayo kunufaika na mradi wa ujenzi wa vyoo bora. Mradi wa ujenzi wa vyoo kwenye maeneo ya Miinuko umetekelezwa na Taasisi ya kujenga uwezo na ubunifu wa Jamii nchini CCI Kupitia muungano wa vikundi vya kijamii vilivyoko kwenye makazi duni Jijini Mwanza. Miongoni mwa maeneo yaliyonufaika na ujenzi wa vyoo bora ni pamoja na Mtaa wa Mabatini Kusini ambapo baadhi ya wakazi walionufaika na ujenzi wa vyoo wamelishukuru Taasisi ya CCI kwa kuwaondolea changamoto ya Ukosefu wa Vyoo uliokuwa unawakabili. Wakazi hao Rhobi Samwel na Jackline George wamesema kuwa kabla ya kujengewa vyoo hivyo walikuwa wanatumia vyoo visivyokuwa na ubora na hivyo kuchangia uchafuzi wa mazingira ikiwemo Mto mirongo unaotiririsha maji yake kwenye ziwa victoria. Akizungumza wakati wa ziara ya Wanacha...