Skip to main content

Posts

Showing posts from July 5, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAZIRI MKUU AWASILI UFARANSA KUMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili jijini Paris, Ufaransa leo, Julai 6, 2026, kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yanayofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO. Mara baada ya kuwasili, Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Thabit Kombo, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Saidi Yakubu na maafisa wengine wa ubalozi. Katika maadhimisho hayo, Tanzania itaendelea kuonesha nafasi yake ya kipekee katika kukuza, kuhifadhi na kuieneza lugha ya Kiswahili duniani, sambamba na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kupitia lugha hiyo.

DKT. MWIGULU: SERIKALI KUBORESHA UPATIKANAJI WA MIKOPO KWA VIJANA

*_▪︎ Yaandaa maboresho kuruhusu matumizi ya dhamana zinazohamishika_* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inaandaa maboresho ya kisera na kisheria yatakayowaondolea vijana wajasiriamali kikwazo cha muda mrefu cha ukosefu wa dhamana za mikopo kwa kuimarisha mfumo wa udhamini wa mikopo na kuruhusu matumizi ya dhamana zinazohamishika. Amesema hayo leo (Jumapili, Julai 5, 2026) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya fainali za Shindano la Vijana Uchumi Challenge 2026 na utoaji wa tuzo kwa washindi, iliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Mwigulu alisema mojawapo ya changamoto kubwa zinazowakabili vijana wajasiriamali si ukosefu wa mitaji pekee, bali ukosefu wa dhamana zinazokubalika na taasisi za fedha ili kuwawezesha kupata mikopo ya kuanzisha na kuendeleza shughuli za uzalishaji. Alisema Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tayari ina dirisha la udhami...

MISUNGWI YAFUNGUA SIRI YA UFAULU, GEITA WAFIKA KUJIFUNZA

 Na Mwandishi Wetu, Misungwi Jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuinua kiwango cha elimu zimeanza kuvuka mipaka ya Mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa elimu kutoka halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Geita kutembelea wilaya hiyo kujifunza mbinu zilizoiwezesha kufanya vizuri katika mitihani ya taifa kwa miaka mitatu mfululizo. Ugeni huo ulifika Misungwi kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujifunza mikakati ya usimamizi wa elimu, ufuatiliaji wa taaluma na ushirikishwaji wa wadau, hatua zinazotajwa kuwa nguzo kuu za mafanikio ya halmashauri hiyo. Akizungumza baada ya kikao cha kubadilishana uzoefu, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Jenoveva Chuchuba, alisema ujio wa maafisa hao ni ishara kwamba kazi inayofanywa na walimu, viongozi wa elimu na jamii imeanza kutambuliwa hata nje ya mkoa. "Kwa miaka mitatu mfululizo tumekuwa tukifanya vizuri katika mitihani ya taifa. Hili limetokana na usimamizi wa karibu wa taaluma, ushirikiano wa walimu, viongozi na w...