Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, leo Agosti 7, 2026, akiwa mgeni rasmi wa zamu, ametembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Themi-Njiro, jijini Arusha. Katika ziara hiyo, Mhe. Sendiga ametoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini kujitokeza kwa wingi kutembelea maonesho hayo ili kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa za kilimo, mifugo na uvuvi zitakazochochea ongezeko la uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi. Amesema maonesho hayo yamekusanya wafanyabiashara, wabunifu na wajasiriamali kutoka ndani na nje ya nchi, jambo linalotoa fursa kwa wananchi kupata maarifa, kujifunza ubunifu na kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Maonesho ya Nanenane ya mwaka 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: "Tambua Soko, Ongeza Tija kwa Kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050."
Marato tv - Sauti ya Jamii