Skip to main content

Posts

Showing posts from March 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MwanaFA Awapa UVCCM bati 120 wapauwe nyumba ya Katibu

  Na Mwandishi Wetu, Muheza  NAIBU Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA leo tarehe 19 2025, amekabidhi bati 120 kwa ajili ya kuezekea nyumba ya mtendaji wa Umoja wa vijana (UVCCM) wilayani Muheza. Akikabidhi bati hizo kwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Muheza Aziza Mshakangoto, MwanaFA alisema ametekeleza ahadi yake ya kuziezeka nyumba tatu za jumuiya za chama wilayani hapa kuunga mkono wazo la Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ustadh Rajab Abdarahman Abdallah za kila wilaya mkoani hapa kujenga nyumba za watumishi wa Chama. MwanaFA alisema kuwa katika kipindi cha miaka minne na nusu aliyokaa katika ubunge wilaya ya Muheza imepiga hatua ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo katika chama. Alisema mwaka 1993 waliokuwa viongozi wa CCM katika wilaya hiyo, walitenga eneo la Kirumba lililopo kata ya Genge kujengwa nyumba za watumishi wa chama pamoja na ofisi za chama. "Lakini Sasa ni miaka 32 watu walikuwa wanasema watajenga lakini hapakujengwa...

Uongozi wa Shule ya Sekondari Nyaishozi Watoa Ofa Kwa Watoto wa Wakulima wa Zao la Kahawa

 Na Angela Sebastian; Bukoba  SHULE ya sekondari ya Nyaishozi iliyopo Wilayani Karagwe mkoani Kagera hutoa nafasi kwa wanafunzi 12 ambao wazazi wao hawana uwezo kiuchumi lakini ni wakulima wa zao la kahawa kwa ajili ya ufadhiri kimasomo. Mkuu wa shule hiyo Audax Gereon ameeleza hayo jana wakati akiongea na mwandishi wa habari hii baada ya kufika  shuleni hapo,kwa lengo la kujua namna gani wanatatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wa shule hiyo na kuzigeuza kuwa fursa. "Kuna watoto ambao wazazi wao ni wanaushirika lakini pengine uwezo wao ni mdogo kiuchumi ata wakiuza kahawa hawezi kuwalipia ada watoto wao hivyo tunawaleta hapa shuleni tunawapa ofa ya kusoma bure kwa ufadhili wa shule" Anasema wanafanya hivyo kwa kufuata vigezo vya kwamba uwezo wa mwanafunzi kitaaluma ni mzuri na TASAF wanamtambua kuwa ni familia duni ambapo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita wanachukua watoto 12 kila mwaka. Amesema waliona ni budi kutumia changamoto hiyo inayowakabili watoto wa w...

Wachimbaji Wampa Tuzo Dc Songwe Kwa Kutekeleza 4r za Rais Dkt Samia

  Na Mwandishi Wetu, SONGWE WACHIMBAJI wadogo wa madini ya dhahabu katika mgodi wa 614 Local Miners Songwe wamempa tuzo Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kuimarisha mahusiano ndani ya Wilaya hiyo pamoja na kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo. Wachimbaji hao wamemkabidhi Mhe. Itunda tuzo hiyo Jumanne Machi 18, 2025 katika hafla ya kukabidhi madawati 100 yenye thamani ya Shilingi Milioni 15 yaliyotolewa na wanachama wa 614 Local Miners Songwe kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa Shule ya Msingi Saza. Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji hao, Mwenyekiti wa 614 Local Miners, Dickson Kadinda amesema kuwa tuzo hiyo wameitoa kutokana na namna Mkuu huyo wa Wilaya anavyoimarisha mahusiano kati ya wachimbani na wananchi, viongozi pamoja na kutatua migogoro ya wachimbaji inayotokea katika Wilaya hiyo. “Sisi wachimbaji wadogo wa 614 Local Miners tumeamua kukupa tuzo hii kutokana na unavyosaidia kuimarisha amani, mahusiano kati ya wac...

Muwasa Yaendelea Kutoa Elimu Na Kurudishia Wananchi Huduma ua Maji Bila Faini

  Na Shomari Binda-Musoma  MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma ( MUWASA) imeendelea na zoezi la kutoa elimu ya huduma za maji na kuwarudishia waliositishiwa bila kulipa faini. Elimu hiyo inatolewa kwenye viwanja vya shule ya msingi Mukendo tangu machi 17 hadi 23 ikiwa ni wiki ya maji 2025. Akizungumza na GMTV kwenye banda la utoaji elimu lililopo kwenye uwanja huo leo machi 19, 2025 afisa wa MUWASA Joachim Saimon amesema moja ya elimu wanayoitoa ni wananchi kulinda upotevu wa maji. Amesema mwananchi anayo nafasi ya kutoa taarifa juu ya upotevu wa maji pale wanapoona mivujo kwa kuwa mabomba yapo kwenye maeneo yao. Joachim amesema wananchi wakiwa na elimu hiyo ya utoaji taarifa inakuwa rahisi kwa mafundi wa MUWASA kufika eneo la tukio na kufanya matengenezo Amesema licha ya elimu hiyo kupitia Wiki ya Maji wanapokea kero mbalimbali kutoka kwa wananchi kuhusiana na huduma ya maji wanayoitoa. Afisa huyo wa MUWASA amesema wanahakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ...

Sasa ni ahueni kwa Gen Zs, baada ya serikali kuondoa rasmi ada ya vitambulisho

  WAKENYA sasa wamepata afueni baada ya serikali kufutilia mbali ada ya Sh300 inayotozwa wanaowasilisha maombi ya vitambulisho vya kitaifa, kulingana na agizo la Rais William Ruto. Kulingana na toleo la Jumatano (Machi 19, 2025) la gazeti rasmi la serikali, Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen alifanya mabadiliko kwa Sheria ya Usajili wa Watu kuondoa ada ya kupata hati hiyo muhimu. “Kwa kutekeleza mamlaka yaliyoko katika sehemu ya 16 ya Sheria ya Usajili wa Watu, Waziri wa Usalama wa Ndani anatoa kanuni ifuatayo: Kwamba Mpangilio wa Sita wa Kanuni ya Kanuni ya Usajili wa Watu imefanyiwa mabadiliko kwa kuondoa “Sh300” inayotajwa kama ada inayotozwa mtu ambaye hajawahi kupata kitambulisho cha kitaifa. Kwa hivyo, hakuna ada yoyote itakayotozwa anayetuma maombi ya kitambulisha cha kitaifa mara ya kwanza,” Bw Murkomen akaeleza. Akiongea katika eneo la Kibra, Nairobi, wiki jana Rais Ruto alitangaza kuwa Wakenya waliotimu umri wa miaka 18 kwenda juu watapewa vitambulisho vya kita...

Mbunge Mavunde Akabidhi Vifaa Vya Masomo Kwa Watoto Yatima na Wanaoishi Mazingira Magumu Dodoma

  ▪️Ampongeza Rais Samia kwa ujenzi wa miundombinu ya Elimu ▪️Aitaka jamii kuwakumbuka wenye mahitaji ▪️Akabidhi madaftari 10,000 kwa wanafunzi wenye uhitaji ▪️Shule sita zapata ufadhili wa ukarabati majengo Dodoma Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh. Anthony Mavunde* leo amegawa vifaa vya masomo ikiwemo madaftari 10,000 kwa watoto yatima na wanaoishi mazingira magumu wa shule zote za Msingi ndani ya Dodoma Jiji. Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mazengo,ambayo ni shule aliyosoma Mbunge Mavunde,na kutanguliwa na ukaguzi wa miundombinu ya majengo ya madarasa na vyoo kisha katika tukio la kipekee Mbunge Mavunde amekutana na walimu wake wa darasa la Kwanza na kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa kwake na kuwashukuru kwa kuwachangia Bima ya Afya ya Tsh 7.4m. “Tunaishukuru serikali chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya elimu Jijini Dodoma huku tukishuhudia ujenzi wa shule mpya 12 za msingi ndani ya kipindi kifupi ...

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imejipanga Kimkakati Kwa Maslahi ya Taifa

 OFISI ya mwanasheria mkuu wa serikali imechukua hatua ya kutekeleza agizo la MH. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania MH. DK SAMIA SULUH HSSAN la kujiimarisha kisheria kuwaongezea uwezo watendaji wake katika majadiliano na usimamiziwa mikataba inayoingia baina ya serikali na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi kwa kuitisha mafunzo maalumu ya siku tano yatakayohusisha mawakili mia tatu wa serikali. Akizungumza na waandishi wa habari kwake leo mach.19. mwaka huu 2025 Mwanasheria mkuu wa serikali MH. HAMZA JOHARI amesema mafunzo hayo ya siku tano takayofanyika jijini Arusha kuanzia mach. 24 na kuendeshwa na wakufunzi wa ndani na nje ya nchi yatashirikisha maawakili wa serikali kutoka ofisi hiyo, wizara, taasisi, idara na mamlaka za serikali za mitaa nchini kote. Kwa sababu hiyo Mh. mwanasheria mkuu wa serikali amewataka waajiri katika wizara, idara taasisi na mamlaka za serikali za mkitaa kutoa ruhusa kwa mawakili wao ili waweze kushiriki katika mafunzo hayo muhimu. Mwanash...