Skip to main content

Posts

Showing posts from October 13, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Hatimaye UVCCM yahitimisha matembezi na kilele cha mbio za mwenge Nyerere day mwanza

  Na Helena Magabe. Vijana zaidi ya 1400  wa UVCCM kutoka Mikoa mbali mbali Nchini Tanzania bara pamoja  na Visiwani walianza matembenzi  ya zaidi ya kilometa 200 Oktoba 8 2024 kutoka Butiama Mkoani Mara  kuelekea Mwanza lengo likiwa ni kuenzi kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere. Matembenzi hayo yamezinduliwa na mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi Wilaya Butiama ambapo alima sema lengo ni kuenzi kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere pamoja na kuelekea wiki ya Vijana na kilele cha mbio za mwenge na uhuru . Alisema  mwaka 1967 katika ofisi   ya Kata ya CCM Mwitongo  Baba wa Taifa alianzia hapo matembenzi hadi Jijini Mwanza hivyo walitumia  fursa hiyo kumuenzi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha Vijana kugombea  na kuhamasisha Vijana wenzao kushiriki uchanguzi wa Serikali za Mitaa ifikapo Novemba 27. Aidha alisema  kilele cha matembenz...

ETDCO kujenga miundo mbinu ya umeme migodini

Na Richard Mrusha  Geita Kampuni Tanzu ya Umeme Tanesco (Etdco) inayojishughulisha na Ukarabati wa miundombinu ya Umeme katika maeneo mbalimbali imefanikiwa kujenga miundo mbinu na viunganishi vya migodi ya umeme nchini Tanzania. Katika mahojiano na waandishi wa habari kwe Viwanja vya bombambili Mkoani Geita kwenye maonesho ya saba (7) ya Teknolojia ya madini Kaimu Mkurugenzi Huduma Za Ufundi wa kampuni ya Etdco mhandisi Dismas Massawe amesema kuwa kampuni hiyo ni kampuni inayomilikiwa na Serikali yaani Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa asilimia mia moja 100%. Amesema mpaka sasa wamefanikiwa kujenga miundo mbinu kadhaa ya umeme,kujenga laini ya kilomita 100 kutoka Geita mpaka eneo la StamiGold ( Stamico ) na kuunganishia umeme. Amesema, pia wamefanikiwa kujenga mradi mwingine wa kuunganishia umeme Mgodi wa GeitaGold mine (GGML) ,kujenga kilomita 58 kuunganisha umeme katika mgodi wa Kabanga nikel Ngara. Mhandisi Dismas Massawe amesema kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa line ku...

Rais Samia;daraja la Jp Magufuli kuanza kutumika februari mwaka 2025

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Samia Suluhu Hassan,amekagua Maendeleo ya ujenzi wa daraja la kimkakati la Jp Magufuli linalojengwa ndani ya ziwa Victoria litakalounganisha eneo la Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza na kusema ameridhishwa na ujenzi huo. Rais Samia amesema kuwa Ujenzi wa daraja la Jp Magufuli unaotekelezwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi billioni Mia Saba umefikia asilimia 93. Akizungumza na wakazi wa kigongo wilayani Misungwi,Rais Samia amesema kuwa daraja hilo lenye urefu wa kilometa tatu pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 1.66 litafunguliwa februari mwakani.  Daraja la Jp Magufuli ni la kwanza kwa urefu katika nchi za afrika mashariki na kati na litakuwa kiungo muhimu cha usafiri na usafirishaji baina ya mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mataifa Jirani ikiwemo UGANDA,BURUNDI,RWANDA na JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO. Daraja hilo litakuwa na uwezo wa kubeba Tani 120 za Mizigo na linatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo feb...

Raisia aipongeza wizara ya madini kwa usimamizi madhubuti wa sekta

⚫️ Trilioni moja yatengwa kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu kupitia BOT ● Shilingi Bilioni 250 zatengwa kama dhamana ya mikopo kwa wafanyabiashara wa dhahabu ●Mwaka 2023 madini yenye thamani zaidi Trilioni mbili yaliuzwa kupitia masoko ●Serikali kuongezea mitambo ya uchorongaji 10 zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogo Na Mwandishi  wetu ;Geita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza wizara ya madini kwa usimamizi madhubuti wa sekta madini ambao umechangia ukuaji wa haraka wa mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa. Hayo yameelezwa leo Oktoba 13, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akifunga maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita. Mh Samia ameeleza katika mikakati ya kuimarisha uchumi wa nchi na upatikanaji wa fedha za kigeni Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetenga kiasi cha shilingi Trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu  kutoka kwa wachimbaji. Rais, Dkt. Sam...

Huduma ya Psssf kidijitali yarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama

  Idadi ya wanachama wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma(PSSSF)waliowasilisha maombi ya mafao kwa njia ya kidijitali nchini imeongezeka kutoka mia sita Juni mwaka huu hadi kufikia 8,760 septemba 30 mwaka huu. Meneja uhusiano wa Mfuko wa Psssf Yesaya Mwakifulefule amesema kuwa ongezeko hilo limefikiwa baada ya wanachama kuhamasishwa kujiunga pamoja na kutumia huduma za Psssf kidijitali. Akizungumza wakati wa kilele cha maonesho ya saba ya madini Mkoani Geita,Mwakifulefule amesema kuwa ongezeko hilo pia ni matunda ya kampeni ya twende kidijitali iliyomalizika mwezi uliopita. ‘’Hatusubiri mpaka Mwanachama astaafu ndipo tuweze kuwafundisha namna ya kutumia njia ya kidijitali,wapo wanaoelekea kustaafu kati ya miezi sita mpaka miaka 55,hao tunawapa semina za kustaafu,Lakini pia kupitia maonesho kama haya huwa tunawafundisha namna ya kujiunga pamoja na kuwaeleza namna ya kutumia njia hizo”alisema Mwakifulefule Aidha amebainisha kuwa Mfuko wa Psssf hivi sasa unatoa mafao nda...

Waziri mkuu amesema uwekezaji mkubwa umefanyika katika sekta ya hali ya hewa nchini

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea na jitihada za kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya hali ya hewa nchini ambapo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, Tanzania itakuwa na Rada saba ikiwa ni kiwango kikubwa cha Rada katika nchi za Afrika Mashariki na Kati. Amesema kuwa hatua hiyo ni mwendelezo Serikali za kufanya uwekezaji katika sekta ya hali ya hewa nchini kwa kufunga miundombinu ya kisasa ya hali hewa ili kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa taarifa za hali ya hewa. Amesema hayo leo (Jumapili, Oktoba 13, 2024) wakati alipotoa tamko la kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa, Jijini Mwanza. “Nitumie fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uwekezaji mkubwa katika eneo hili lakini pia kuendelea kutoa kipaumbele kwa makundi maalumu na kuweka mikakati thabiti inayolenga kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii. ” Amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanatoa fursa ya kuimarisha ushir...