Skip to main content

Posts

Showing posts from August 2, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT. MWIGULU: KUWEKEZA KWENYE UTAFITI NI NJIA SAHIHI YA MAGEUZI YA KILIMO.

 ▪️Awataka watumishi kutimiza wajibu wao_ Dodoma, Agosti 2, 2026 WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewahimiza watendaji wa Serikali kuwahudumia kikamilifu Watanzania ili miradi inayojengwa na Serikali itoe matokeo chanya. “Tunachokijenga hapa, si jengo pekee, bali tunajenga mazingira bora ya utendaji wa mfuko. Kupitia uwekezaji huu tunachochea na tunaharakisha utekelezaji wa dhamira ya dhati aliyoionesha Mheshimiwa Rais kumsaidia mkulima mdogo kwa kuwezesha kupata mikopo.” “Watumishi wote wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa bidii ili uwekezaji huu uwe na manufaa kwa Taifa. Tusiweke ofisi nzuri halafu huduma zikawa duni, tutakua hatujafikia malengo yaliyokusudiwa, ofisi nzuri lakini mwananchi akija kupata huduma anaambiwa njoo kesho, njoo kesho, majengo haya hayatakuwa na maana,” amesema Waziri Mkuu. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili Agosti 2, 2026) Iyumbu jijini Dodoma wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa makao makuu ya ofisi za Mfuko wa Udhamini wa Pembejeo za Kilimo (A...

BMT YATAJA FURSA 12 ZA AFCON 2027, WATANZANIA WAHIMIZWA KUJIANDAA MAPEMA

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza fursa 12 zitakazotokana na Tanzania kuwa mwenyeji mwenza wa Mashindano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2027 ambazo zitafungua zaidi milango ya maendeleo ya uchumi, ajira, biashara, utalii na uwekezaji nchini. Akizungumza kuhusu fursa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa BMT, Bw. Aminiel Aligaesha, amesema AFCON 2027 ni tukio la kihistoria litakalofanyika kwa mara ya kwanza Ukanda wa Afrika Mashariki na likiwa linatimiza miaka 70 mwakani tangu kuanzishwa kwake. Kwa mujibu wa Bw. Aligaesha, fursa ya kwanza ni kuongezeka kwa biashara na shughuli za kiuchumi, ambapo hoteli, nyumba za kulala wageni, migahawa, maduka pamoja na wauzaji wa bidhaa zenye nembo za mashindano watanufaika kutokana na ongezeko la wageni na mashabiki. Aidha, amesema sekta ya benki na huduma za kifedha itanufaika kupitia ongezeko la miamala ya kifedha, huduma za kubadilisha fedha za kigeni, udhamini wa matukio na utoaji wa bidhaa maalum za kifedha kwa wa...

MWENGE WA UHURU WAFIKA KWA BABA WA TAIFA BUTIAMA NA KUWASHA MWENGE WA MWITONGO

 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Wazo Michael Mwang'onda amewasha Mwenge wa Mwitongo Nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutumia Mwenge wa Uhuru katika tukuo ambalo limefanyika Agosti 2 mwaka 2026 katika kijiji Butiama eneo la Mwitongo. Wakiwa Mwitongo, Mwenge wa Uhuru umepokelewa na familia ya Baba wa Taifa wakiongozwa na Chifu wa kabila la Wazanaki Japhet Wanzagi ambaye ni kiongozi wa familia ya Chifu Burito Nyerere na msimamizi wa familia ya Baba wa Taifa. Katika tukio hilo pia limeshuhudiwa na mkuu wa Mara kanali Evans Mtambi na viongozi wengine wa Serengeti na vyama vya Siasa.

POLISI JAMII MTUMBA WAZINDUA KAMPENI YA “DAFTARI MOJA, PENI MOJA”, WAWAPA MOTISHA WANAFUNZI KIKOMBO

  JESHI la Polisi kupitia Kitengo cha Polisi Jamii Wilaya ya Kipolisi Mtumba limeendelea kuimarisha ushirikiano wake na wananchi kwa kuzindua kampeni ya "Daftari Moja, Peni Moja, Mwanafunzi Mmoja Arudi Darasani", sambamba na kugawa vifaa vya kujifunzia na kutoa zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kikombo, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma. Programu hiyo ya outreach iliyofanyika Agosti 1, 2026, iliongozwa na Afisa Polisi Jamii wa Wilaya ya Kipolisi Mtumba, ASP Charles Mwamtobe, akiwa ameambatana na Mkaguzi wa Kata ya Kikombo, INSP Chohoma Charles. Lengo lilikuwa kuhamasisha elimu, kuimarisha nidhamu, kuibua vipaji na kuwapa motisha wanafunzi ili waendelee kufanya vizuri katika masomo na kuwa raia wema wa baadaye. Katika hafla hiyo, wanafunzi walikabidhiwa vifaa mbalimbali vya kujifunzia vikiwemo madaftari, kalamu, penseli, rula, vifutio na vichongeo. Aidha, zawadi maalum zilitolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika taaluma, nidhamu, michezo, usafi, mahudhurio darasani...

WATU 8 WAFARIKI, 66 WAJERUHIWA AJALI YA MABASI MAWILI DODOMA

 Watu wanane (8) wamefariki dunia na wengine 66 kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria yaliyogongana katika Kijiji cha Ibihwa, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, kando ya barabara kuu ya Dodoma Singida. Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Isamilo lenye namba za usajili T 428 EXP, lililokuwa likitoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam, na basi la Libanika Luxury lenye usajili T 897 DUP, lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza. Kwa mujibu wa taarifa, watu Saba wamepoteza maisha papo hapo huku mmoja akipoteza maisha wakati wakipelekwa hospitali kwaajili ya kupatiwa matibabu na majeruhi wakipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, kituo cha Afya cha Wilaya Makole na Bahi kwaajili ya kupatiwa matibabu. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amefika katika eneo la tukio kujionea hali halisi ya ajali hiyo kabla ya kutembelea majeruhi waliolazwa hospitalini ambapo akiwa hospitalini, amepokea taarifa kutoka kwa wataalamu wa afya kuhusu maendeleo ya ma...

TANZANIA NA MAREKANI ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo wamefanya mazungumzo na ujumbe maalum wa Wajumbe 11 wa Baraza la Wawakilishi la Marekani (Congress) kutoka Vyama vyote viwili Vikuu nchini Marekani, ulioongozwa na Ronny Jackson, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya ya Huduma za Kijeshi, Ulinzi na Usalama ya Baraza la Wawakilishi la Marekani (House Armed Services Subcommittee). Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Makao Mkuu ya zamani ya Jeshi la Wananchi la Tanzania, Ngome Upanga, Dar es Salaam, ymelenga kujadili maeneo ya kipaumbele katika uhusiano kati ya Tanzania na Marekani, hususan ushirikiano wa biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama pamoja na hali ya amani na usalama katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Wakati wa mazungumzo hayo Marekani, imeonyesha dhamira ya kupanua ushirikiano katika biashara na uwekezaji, hususan katika sekta za kimkakati zikiwemo ...

BMT YATAJA FURSA 12 ZA AFCON 2027, WATANZANIA WAHIMIZWA KUJIANDAA MAPEMA

 Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza fursa 12 zitakazotokana na Tanzania kuwa mwenyeji mwenza wa Mashindano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2027 ambazo zitafungua zaidi milango ya maendeleo ya uchumi, ajira, biashara, utalii na uwekezaji nchini. Akizungumza kuhusu fursa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa BMT, Bw. Aminiel Aligaesha, amesema AFCON 2027 ni tukio la kihistoria litakalofanyika kwa mara ya kwanza Ukanda wa Afrika Mashariki na likiwa linatimiza miaka 70 mwakani tangu kuanzishwa kwake. Kwa mujibu wa Bw. Aligaesha, fursa ya kwanza ni kuongezeka kwa biashara na shughuli za kiuchumi, ambapo hoteli, nyumba za kulala wageni, migahawa, maduka pamoja na wauzaji wa bidhaa zenye nembo za mashindano watanufaika kutokana na ongezeko la wageni na mashabiki. Aidha, amesema sekta ya benki na huduma za kifedha itanufaika kupitia ongezeko la miamala ya kifedha, huduma za kubadilisha fedha za kigeni, udhamini wa matukio na utoaji wa bidhaa maalum za kifedha k...

ILANI YA CCM: WANANCHI 12,414 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA MILIONI 853 KILINDI

 Na Mashaka Mhando, KILINDI ZAIDI ya wananchi 12,414 wa vijiji vya Nkama, Kwastemba na Kwamwande wilayani Kilindi, wanatarajiwa kuondokana na adha ya maji kufuatia Mradi wa Maji wa Nkama Mnazi unaogharimu Shilingi 853,166,702 kufikia asilimia 75 ya utekelezaji wake. Hatua hiyo ni mwendelezo wa matunda ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM inayotoa kipaumbele kwenye uboreshaji wa huduma za maji safi na salama vijijini na mjini. Akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Tanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Songe, Mhandisi Philipo Bajuta, alisema mradi huo unaotekelezwa na mkandarasi Sajo Civil Engineering kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji HTM, unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 23, 2026. Baada ya kupokea taarifa hiyo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Mohamed Salim, aliwapongeza watendaji kwa usimamizi mzuri uliowezesha kazi kufika asilimia 75, li...