Skip to main content

Posts

Showing posts from September 9, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Nchimbi Akutana na Kufanya Mazungumzo Na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Mkoa wa Katavi

MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya ya Mariadhiano na Amani Tanzania Mkoa wa Katavi (JMAT)  leo Jumatano Septemba 10,mjini Mpanda ,Katavi. Mazungumzo yao yalijikita kuangalia jinsi gani ya kuendeleza amani na mshikamano wa wananchi wa mkoa wa Katavi hasa mnamo kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025. Balozi Dkt.Nchimbi yuko Mkoani Katavi akiendelea na Mikutano yake ya Kampeni ya kusaka kura za Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pichani akiwa na viongozi hao mara baada ya kikao hicho kwenye ukumbi wa hotel ya Home Ground mjini Mpanda.

Waziri Kombo Akutana na Katibu Mkuu wa Imo Kuimarisha Ushirikiano wa Masuala ya Bahari

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirika la Bahari Duniani (IMO), Bw. Arsenio Domínguez, jijini London. Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na IMO hususan katika nyanja za usalama wa baharini, ulinzi, utunzaji wa mazingira ya bahari na kujengeana uwezo. Mhe. Waziri Kombo alieleza jinsi Serikali ya Tanzania inavyothamini ushirikiano na IMO na mchango wake katika kuimarisha nafasi ya Tanzania kama taifa muhimu katika eneo la Bahari ya Hindi, akisisitiza nafasi ya Tanzania katika jitihada za utunzaji wa rasilimali bahari ili iendelee kuwa na mchango kwenye uchumi ikiwemo kupitia bandari ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika biashara ya kikanda na ya kimataifa. “Tunaitambua IMO kama mshirika muhimu katika kujenga uwezo wa Tanzania kwenye masuala ya bahari na kusaidia juhudi zetu za kuboresha sekta hii kwa kuzingatia viwango vya kimataifa,” alisema Mhe....

Dkt. Biteko Ahimiza Kura za Kutosha Busonzo

📌 Wananchi wa Busonzo wanufaika na miradi ya uhakika ya umeme, maji, elimu 📌 CCM yaahidi maendeleo Busonzo Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto  Mashaka Biteko amewahimiza wananchi wa Kata ya Busonzo wilayani Bukombe mkoani Geita kujitokeza kwa wingi na kuwapigia kura wagombea wa CCM ili kukipatia chama hicho ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu ujao Oktoba 29, mwaka huu. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 9, 2025 wakati akiendelea na kampeni katika Kata ya Busonzo wilayani Bukombe mkoani humo. Amesema eneo la Idoselo katika Kata ya Busonzo lilikuwa na changamoto kadhaa ikiwemo barabara na shule. Kufuatia hali hiyo, Rais Samia alielekeza wananchi wa eneo hilo wachongewe barabara, wajengewe shule na hospitali. “ Hapa Idoselo tumejenga Kituo Kikubwa cha Kuzalisha umeme megawati 5 ili wananchi waweze kupata umeme, tunataka kuongeza upatikanaji wa maji na baada ya uchaguzi tutapanua chanzo cha maji ili kuhakikisha kunakuwa na maji ya uhakika,” amesema Dkt. Biteko. Ametaj...

Maelfu ya wananchi Iramba wajitokeza mkutano wa kampeni za mgombea wa CCM

Sehemu ya Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) Iramba, mkoani Singida tarehe 10 Septemba, 2025.

Dkt.Samia aomba kura kwa wananchi wa Iramba

Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi na wanachama wa CCM wa Iramba katika muendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho Mkoani Singida tarehe 10 Septemba 2025.

Mgombea Ubunge Wa Act Jimbo La Kawe Asaka Kura Nyumba Kwa Nyumba

Matukio Katika Picha.  Siku ya tarehe 09.09.2025, tumeendelea na Kampeni za nyumba kwa nyumba. Kuomba kura kwa Wananchi wa Jimbo la Kawe, tukiwaomba watuamini tukawatumikie.  Mimi mgombea Ubunge jimbo la Kawe Glory Tausi nikiongozana na Mgombea U-Diwani wa Kata ya Bunju, Ndugu Suleiman Dinar, tukipita mitaa mbalimbali ya Bunju, na leo tulikua Mtaa wa Basihaya maeneo ya Chasimba. Kampeni hizi za nyumba kwa nyumba, si tu zinatuweka karibu na Wananchi, lakini zinatupa nafasi ya kuziona Changamoto wanazokutana nazo wananchi wa maeneo haya. Mfano maeneo ya Chasimba, barabara iliyokua inapitika hapo mwanzoni kwa sasa ni mto uliokauka.  Imetolewa na:  *Glory Tausi* *Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe*.