Skip to main content

Posts

Showing posts from May 4, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kawaandaeni Vijana wa Kitanzania kuwa Wabunifu,Wajasiriamali,Washindani katika ajira-Prof.Shemdoe

Na OWM - TAMISEMI, Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amewataka walimu wapatao 150 wa shule za amali waliopatiwa mafunzo nchini India kwenda kuwapatia ujuzi  vijana wa kitanzania katika shule wanazofundisha ambao utawawezesha kuwa wabunifu, wajasiriamali  na washindani katika ajira za ndani na nje ya nchi ili  kutoa mchango katika maendeleo ya taifa. Prof. Shemdoe ametoa wito huo Mei 04, 2026 wakati wa kikao chake na walimu hao wapatao 150 wa Shule za Amali ambao wamerejea nchini kutoka nchini India walihudhuria mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutoa elimu ya ufundi na mafunzo ya stadi za kazi kama nyenzo muhimu ya kukuza uchumi wa viwanda, kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana, na kuongeza ushindani katika soko la ajira. “Tunategemea vijana watakaotoka katika shule za amali wawe na uwezo wa kushindana katika ajira za ndani na nje ya nchi, waweze kujiajiri na kuwa wajasiriamali wenye mc...

Profesa Mkenda:Kila la Kheri Wanafunzi wa Kidato cha Sita na Walimu Tarajali Wanaoanza Mitihani

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amewatakia kila la kheri wanafunzi wa Kidato cha Sita pamoja na waalimu tarajali wote wanaoanza mitihani yao leo Mei 4,2026. Kwa mujibu wa takwimu rasmi, jumla ya wanafunzi 165,655 wa Kidato cha Sita wameanza mitihani yao leo, ambayo itaendelea hadi tarehe 15 Mei 2026. Kwa upande wa waalimu tarajali, takribani 14,669 nao wameanza mitihani yao na watahitimisha tarehe 18 Mei 2026. Akizungumza leo Mei 4,2026 katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma kuhusu zoezi hilo, waziri wa Elimu Sayansi na Teknlojia Prof. Adolf  Mkenda amesema  Serikali inaungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwapa moyo watahiniwa wote nchini. “Napenda kuwapongeza sana wanafunzi wa Kidato cha Sita pamoja na waalimu tarajali kwa kufikia hatua hii muhimu ya mitihani. Serikali inawaombea kila la heri, utulivu na mafanikio mema katika kipindi hiki.” Amesema  Aidha, amesisitiza umuhimu wa uadilifu na kufuata taratibu za ...

Serikali imetangaza fursa na Neema Kwa Wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza fursa mbalimbali kwa wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Sita, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza vipaji na kukuza wataalamu wa baadaye nchini. Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, wakati akiongea na Waandishi wa Habari leo Mei 4,2026 katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, amesema kuwa wanafunzi watakaofaulu vizuri watapata nafasi za kujiunga na vyuo vikuu kupitia mifumo ya kitaaluma pamoja na kuzingatiwa katika utoaji wa mikopo kupitia HESLB. Aidha, Prof. Mkenda Amesema Serikali kupitia Samia Scholarship itaendelea kufadhili wanafunzi bora wa sayansi kwa asilimia 100 katika vyuo vya ndani, hususan katika fani za Hisabati, TEHAMA, Sayansi Asilia, Uhandisi na Tiba. Kwa wanafunzi wa sayansi wenye ufaulu wa juu zaidi, watachaguliwa kwa mafunzo maalum katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela (NM-AIST) Arusha kabla ya kupelekwa kuendelea na masomo nje ya nchi katika vyuo vikuu mbalimbali. Pia Serikali imesisiti...

Tanzania kung'ara duniani;Miss World 2027 Kufungua Fursa Mpya za Uchumi na Utalii

TANZANIA inatarajiwa kunufaika kiuchumi na kijamii kupitia uenyeji wa Miss World 2027, tukio kubwa la kimataifa linalotarajiwa kuvutia maelfu ya wageni kutoka mataifa mbalimbali. Mashindano hayo yanatajwa kuwa kichocheo cha ukuaji wa sekta za utalii, biashara, ubunifu na ajira, huku pia yakiitangaza nchi kimataifa kama kitovu cha utamaduni na vivutio vya asili. Mafanikio hayo yamebainishwa Bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake uliowezesha Tanzania kupata heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo. “Mheshimiwa Spika, natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais kwa uongozi wake madhubuti ulioiwezesha Tanzania kupata heshima hii kubwa ya kimataifa,” alisema Waziri Makonda. Ameongeza kuwa:“Mashindano haya yataleta mapato kupitia utalii, udhamini na biashara za wageni, huku yakitoa fursa kwa wabunifu wa ndani kujifunza na ...

Makonda atoa picha kamili ya Mafanikio Michezo,AFCON 2027 yapewa kipaumbele

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Poul Makonda, amesema Serikali imeendelea kupata mafanikio makubwa katika sekta ya michezo nchini, hatua inayodhihirisha ukuaji wa vipaji na kuimarika kwa ushindani wa kimataifa. Akizungumza leo Mei 4, 2026, Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo, Makonda amesema mafanikio hayo yanatokana na uwekezaji wa kimkakati pamoja na usimamizi madhubuti wa shughuli za michezo. Ameeleza kuwa mashindano ya CHAN 2024 yaliyofanyika mwaka 2025 kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya na Uganda yameacha alama kubwa, huku timu ya Taifa “Taifa Stars” ikionesha ushindani wa hali ya juu kwa kufanikiwa kufika hatua ya robo fainali. “Hii ni ishara kuwa soka letu la ndani linazidi kukua na kuimarika,” amesema Makonda. Amesema kuwa ubora wa maandalizi na usimamizi wa mashindano hayo uliifanya Tanzania kuendelea kuaminiwa kimataifa, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alitunukiwa tuzo ya heshima na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Katika maandalizi ...

Serikali yaleta Mwelekeo Mpya Ithibati; Wanahabari Wakongwe kurejeshwa rasmi katika Tasnia ya Habari

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeandaa mwongozo maalumu wa kisheria utakaowezesha wanahabari wakongwe waliokuwa wameathiriwa na mfumo wa ithibati kurejea rasmi katika tasnia ya uandishi wa habari. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakatu akiwasilisha bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/27.  hatua hiyo inalenga kuimarisha ushiriki wa wanahabari wenye uzoefu mkubwa katika sekta ya habari nchini. “Wizara kupitia Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari tumeandaa mwongozo maalumu wa kisheria utakaowezesha wanahabari wakongwe walioathiriwa na mfumo wa ithibati kurejea katika mfumo.”. Amesema Amefafanua kuwa mwongozo huo umeandaliwa kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229, yenye lengo la kuimarisha na kudhibiti taaluma ya uandishi wa habari kwa kuweka mfumo thabiti wa usimamizi wa sekta hiyo. Kwa mujibu wa Waziri huyo, wanahabari wakongwe hawatatazamwa tu kwa...

REA Yamtambulisha Mtoa Huduma wa Majiko Banifu Kagera, Wananchi Kunufaika na Ruzuku ya Asilimia 80.

  📍 *Bukoba, Kagera*  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtambulisha rasmi mtoa huduma, kampuni ya Burn Manufacturing Company Limited, kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa Kanali Yahaya Ramadhani Kido, ikiwa ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku kwa wananchi wa mkoa huo. Utambulisho huo umefanyika katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa mkoa pamoja na wataalamu kutoka REA, ambapo ilielezwa kuwa kampuni hiyo itahusika moja kwa moja na usambazaji wa majiko hayo pamoja na kuhakikisha yanawafikia wananchi kwa bei nafuu kupitia utaratibu wa ruzuku uliowekwa na Serikali. Mradi huo unalenga kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, ambavyo vimekuwa na athari kubwa kwa afya za wananchi na mazingira. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahaya Ramadhani Kido, ameipongeza REA kwa kuendelea kuibua na kusimamia miradi yenye tija kwa wananchi, akisisi...

Chanjo ya Polio kutolewa Wilayani Misungwi Mei 7 hadi 10 Mwaka huu

Na Thomas Lutego; Misungwi   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama(kushoto)  akifungua Kikao Cha Utoaji wa Elimu na Hamasa ya Zoezi la Kampeni ya Chanjo ya Ugonjwa wa Polio kwa Watoto chini ya Miaka 10 itakayofanyika kuanzia tarehe 7 hadi 10 Mei, mwaka 2026. Wadau wa Sekta ya Afya, Viongozi wa Dini na Makundi mbalimbai Wilayani Misungwi wakiwa katika Kikao Cha Utoaji wa Elimu na Hamasa ya Zoezi la Kampeni ya Chanjo ya Ugonjwa wa Polio kwa Watoto chini ya Miaka 10 itakayofanyika kuanzia tarehe 7 hadi 10 Mei, mwaka 2026.

Waziri Mkuu asisitiza Ushirikiano wa Kikanda Kukabiliana na Uhalifu wa Kimataifa,aangazia nafasi ya Teknolojia

_▪︎ Asema mapambano dhidi ya uhalifu yanahitaji mshikamano wa kimataifa_ _▪︎ Aeleza teknolojia ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na uhalifu wa kisasa_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema ushirikiano wa kikanda na kimataifa ni sharti la mafanikio katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kimataifa unaozidi kubadilika na kuvuka mipaka. Amesema kuwa katika dunia ya sasa, aina nyingi za uhalifu hupangwa, hufadhiliwa na kuratibiwa kwa njia za kidijitali, hali inayohitaji mifumo imara ya kiteknolojia pamoja na ushirikiano wa pamoja ili kuudhibiti kwa ufanisi. Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Mei 4, 2026, wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa 11 na Kongamano la Chama cha Waendesha Mashtaka Afrika Mashariki (EAAP), unaofanyika katika Ukumbi wa Blue Sapphire, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 4 hadi 6 Mei, 2026, wenye kaulimbiu isemayo “Matumizi ya Teknolojia katika Kukabiliana na Uhalifu Dhidi ya Wanyamapori na Uhalifu wa Kimataifa Uliopangwa.” “Kama ambavyo uhalifu uliopangwa hauwezi k...