Skip to main content

Posts

Showing posts from December 29, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wasanii wamiminika JKCI ofa ya Rais Samia kupima moyo

Na Mwandishi Wetu WASANII ambao wameendelea kuchangamkia fursa ya kupima moyo bure katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wamempongeza Rais kwa kuwapa fursa hiyo. Akizungumza wakati wa uchunguzi wa moyo kwa wasanii hao jana, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk. Peter Kisenge alisema amefurahi kuona wasanii wanachangamkia fursa hiyo na kuwataka wengine kuendelea kujitokeza. “Nimemwona Zuchu, Mboso, D Voice wamekuja naomba nitumie fursa hii kuwashauri wasanii wengine waige mfano huu wa kuja kupima vipimo vya moyo bure,” alisema “Tunamshukuru sana Rais Samia kwa fursa hii ya kuwapima wasaniii bure hii ni kuhamasisha wananchi wote wawe na tabia ya kupima afya zao ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanachangia vifo vingi sana,” alisema Naye Mbwana Yusufu kutoka (WCB), maarufu kama Mboso alimshukuru Rais Samia kwa fursa hiyo akisema yeye anashida ya moyo na amekuwa akifanya vipimo mara kwa mara kujua maendeleo ya afya yake ya moyo. ...

Ruangwa kwa Maendeleo, imewezekana-Majaliwa

*Asema Rais Dkt. Samia anamchango mkubwa kwenye Maendeleo ya Wilaya hiyo. WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Wilaya ya Ruangwa imepiga kasi kubwa ya maendeleo ambayo imewawezesha wakazi wa Wilaya hiyo kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Amesema kuwa Wilaya hiyo changa ilikuwa na changamoto nyingi kwenye Sekta ya Elimu, Afya, Kilimo, Miundombinu ikiwemo barabara, maji, Umeme, Uwekezaji na hata kwenye michezo “Changamoto hizi zilitufanya tuje na kaulimbiu ya “Ruangwa kwa Maendeleo Inawezekana, na sasa imewezekana” Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Desemba 29, 2024) wakati alipozungumza na mamia ya Wakazi wa kijiji ya Mbekenyera, wilayani Ruangwa mkoani Lindi. Amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya wilaya hiyo kutokana na fedha ambazo amekuwa akitoa zilizowezesha kutekeleza miradi hiyo ya kimkakati. Akizungumza kuhusu Sekta ya Elimu Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Wilaya ya Ruangwa ilikuwa na vijiji vichache...

Mkuu wa Mkoa Manyara akabidhi Zawadi za Rais Samia kwa Makundi Maalum

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga leo Disemba 29, 2024 ametembelea vituo vitatu (3) vya watu wenye mahitaji maalumu vilivyopo katika wilaya ya Babati ikihusisha; Kituo cha kulelea wazee magugu,Kituo chakulelea Watoto wenye ulemavu unaotibika cha Zilper na kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi mazingira magumu cha Hossana na kutoa zawadi za sikukuu ya mwaka mpya 2025. RC Sendiga ameeleza kuwa zawadi hizo zimetoka kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni ishara ya upendo wa Mhe. Rais kwa wananchi hao katika sikukuu hizi za Mwisho wa Mwaka. Zawadi zilizotolewa zilihusisha Mchele, Mafuta ya kupikia, Sukari, Unga wa ngano, Viungo, Sabuni, juisi, maji, Mbuzi, madaftari na kalamu. Aidha, RC Sendiga amesema zoezi hilo la ugawaji wa zawadi kwa vituo hivyo linaendelea katika Wilaya zote za Mkoa wa Manyara.

Mandonga na Dullah Mbabe wamshukuru Dkt. Samia kwa kuendelea kusapoti Michezo nchini

Miaka minne kasoro ya Uongozi wa serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais wetu mpendwa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekuwa na mafanikio makubwa sana katika sekta ya  michezo, sekta ambayo imebeba matumaini makubwa ya vijana waliojiajiri kupitia vipaji mbalimbali walivyonavyo. Si tu katika michezo iliyozoeleka na wengi, kama mpira wa miguu, kikapu na pete, bali Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amegusa pia michezo ya Masumbwi (Boxing) kwa kuendelea kusapoti vijana wanaoshiriki michezo hiyo.  Mwishoni mwa wiki hii, tumeshuhudia Mheshimiwa Rais akitoa motisha kwa mabondia walioshiriki kwenye BOXING SAFARI iliyofanyika katika Uwanja wa Zimbihile, wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera.  Motisha ya Tsh. 10,000,000/= ilikabidhiwa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. Fatma Mwassa kwa niaba ya Mh. Rais Samia*  kwa washindi 10 waliopatikana katika mapambano 10 yaliyopigwa siku hiyo.  Washiriki wa mapambano hayo na mashabiki wa Masumbwi mkoani Kagera, kwa pamoja wanasema upendo wa Rais...

Kada wa Ccm Jack Kangoye aonesha Upendo Mkubwa Kwa Wenye Ulemavu Tarime

 Kada kijana wa chama Cha mapinduzi CCM Jack Kangoye,ameshiriki kupata chakula pamoja na watu wenye ulemavu Desemba 28-2024 nyumbani kwake mjini Tarime mkoani Mara. Kada huyo ambaye amekuwa akitoa misaada mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya jamii ametumia nafasi hiyo kusikiliza  maitaji mbalimbali ya jamii hiyo. Amesema ameona changamoto nyingi zinazowakabili watu wenye ulemavu hivyo amebeba jukumu hilo na kutoa ahadi kuwa wakati wa sikukuu ya Pasaka mwaka 2025 atakuwa ametatua baadhi ya changamoto hizo.