Skip to main content

Posts

Showing posts from September 7, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TCU YAFUNGUA AWAMU YA PILI YA UDAHILI WA VYUO

Na Mwandishi Wetu - Dodoma Wanafunzi waliokosa nafasi katika awamu ya kwanza ya udahili wa Shahada ya Kwanza sasa wamepata fursa nyingine baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kufungua Awamu ya Pili ya Udahili kwa mwaka wa masomo 2026/2027. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 8,2026 na Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa amesema awamu hiyo itafunguliwa hadi Septemba 21, 2026, huku waombaji ambao hawakuweza kukamilisha maombi au hawakupata nafasi katika awamu ya kwanza wakitakiwa kutumia fursa hiyo kuomba katika vyuo wanavyopenda. "Taarifa hiyo inakuja wakati ambapo idadi kubwa ya vijana imeonyesha uhitaji wa kuendelea na elimu ya juu nchini, katika awamu ya kwanza, jumla ya waombaji 149,645 waliomba kujiunga na vyuo 93 vinavyodahili wanafunzi katika Shahada ya Kwanza",amesema. Amesema idadi ya programu za masomo zilizowasilishwa pia imeongezeka kutoka 894 mwaka 2025/2026 hadi 1,019 mwaka huu ikiwa ni sawa na ongezeko la programu 125. "Wanafunzi z...

PSSSF NA MTANDAO WA WANABLOGU TANZANIA (TBN) WAJENGA USHIRIKIANO MKAKATI WA KUONGEZA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII

 Dar es Salaam Katika kile kinachoelezwa kuwa ni hatua madhubuti ya kupanua wigo wa utoaji wa elimu kwa umma, timu ya maofisa wa juu kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imefanya ziara rasmi katika makao makuu ya muda ya Tanzania Bloggers Network (TBN) yaliyoipo Dar es salaam, Kijitonyama na kufanya mazungumzo ya kimkakati na viongozi wakuu wa mtandao huo. Mazungumzo hayo yaliyolenga kujenga ushirikiano wa manufaa ya pande zote mbili  yamejikita katika kuimarisha uhusiano wa kisekta kwenye masuala ya habari, uelimishaji wa umma, na usambazaji wa maarifa sahihi kuhusu mifumo ya pensheni na uwekezaji nchini. Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mwenyekiti wa TBN, Beda Msimbe, alieleza utayari wa mtandao huo kusimama kidete kama chombo cha kutoa elimu na kusambaza maarifa sahihi kwa umma na katika nyanja za kidijitali (space). Hata hivyo, alisisitiza kuwa ili kufikia malengo hayo kwa ufanisi zaidi, ni muhimu wanachama wa TBN wenyewe wakapatiwa kwanza mafun...

NDEJEMBI ASHIRIKI MAZIKO YA MUME WA RAIS SAMIA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki maziko ya Marehemu Hafidh Ameir Hassan, ambaye ni mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, leo tarehe 07 Septemba 2026. Maziko hayo yamehudhuriwa na Viongozi Wakuu, Viongozi Wakuu Wastaafu, Viongozi wa Serikali, Dini, Vyama vya Siasa, Viongozi wa Mahakama, Bunge, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Familia, Marafiki pamoja na waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi. Marehemu Hafidh Ameir Hassan amefariki leo, tarehe 07 Septemba 2026 katika Hospitali ya kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar alipokuwa anapatiwa matibabu.

ISLAMIC HELP KUWASHIKA MKONO VIJANA 80 MAFUNZO YA UFUNDI STADI.

 Na Mwanamkuu Mwandoro,Tanga. Vijana wapatao 80 kutoka katika wilaya zote mkoani Tanga kunufaika na mradi wa ufadhili wa mafunzo ya ufundi stadi kutoka katika chuo cha VETA Tanga,mradi uliopo chini ya taasisi ya Islamic Help Tanzania ambapo watapatiwa mafunzo katika fani nne ambazo ni ufundi umeme wa majumbani,umeme wa magari,ufundi Bomba pamoja ufundi garage. Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwa ya muda wa miezi sita huku yakihusisha vijana wa kiume pekee lengo ikiwa ni kuwakwamua kiuchumi na kuwaepusha na mkundi hatarishi,mradi huo umefadhiliwa na Shirika la International Islamic Charity Organization 'IICO' lililopo nchini KUWAIT huku ufadhili huo utahisisha gharama zote za masomo. Akizungumza na waandshi wa habari afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka shirika la Islamic Help Tanzania Salum Shaibu amesema kuwa lengo la ufadhili huo ni kuwasaidia vijana ambao licha ya kumaliza elimu ya Sekondari wameshindwa kujiendeleza kimasomo kutokana na hali ya familiya kushindwa kumudu gharama...

TIA: MHITIMU AGEUZA MAARIFA KUWA BIASHARA NA AJIRA

 KUTOKANA na Serikali kuendelea kuwahimiza vijana nchini kujiajiri kupitia taaluma zao, mhitimu mmoja wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Nicolaus Carol Mboya, ameonesha kwa vitendo namna maarifa anayoyapata darasani yanavyoweza kugeuzwa kuwa biashara na hatimaye kuunda ajira kwa vijana wengine. Mboya, ambaye ni mhitimu wa Shahada ya Uhasibu wa Umma na Fedha katika Kampasi ya Dar es Salaam, alianza safari yake ya ujasiriamali akiwa bado mwanafunzi wa mwaka wa tatu mwaka 2025, baada ya kushinda Shindano la Wazo la Biashara lililoendeshwa na TIA. Ushindi huo ulimpa fursa ya kwenda nchini Uganda kujifunza na kupata uzoefu zaidi kuhusu biashara na ubunifu, jambo lililomsaidia kukuza na kuboresha wazo lake hadi kufikia hatua ya kulifanya kuwa biashara halisi. Mwaka 2026, wazo hilo lililozaliwa akiwa mwanafunzi liligeuka kuwa kampuni rasmi kupitia kuanzishwa kwa STEAMORA COMPANY LIMITED, kampuni ya teknolojia ya elimu (EdTech) iliyozinduliwa rasmi Aprili 1, 2026. Kupitia bidhaa yake ku...