Skip to main content

Posts

Showing posts from September 15, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Sagini Ampigia Kampeni Dkt Samia,Madiwani na Dkt Mahera Awe Mbunge Butiama

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Jumanne Sagini amehudhuria Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Butiama ambapo amemnadi na kumuombea kura za ndio Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya CCM Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea ubunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Dkt. Wilson Charles Mahera. Mhe. Sagini ameeleza kuwa kuna kila sababu ya mwananchi wa Butiama kumpa kura ya ndio Mgombea wa urais, ubunge na udiwani anayetokana na Chama Cha Mapinduzi ili kutengeneza muunganiko wa mafiga matatu ambayo yatarahisha kuleta maendeleo kama yalivyopatika katika kipindi chake cha 2020-2025. "Kipindi cha Mwaka 2020 Wilaya ya Butiama tuliongoza kutoa kura nyingi za Rais Mwaka 2025 tunaye Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Wilson Mahera pamoja na madiwani wa Kata zote 18 wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi msifanye kosa wapeni kura nyingi za ndio ili wanapoongea lugha moja maendeleo yanajaa ndani ya Butiama kwani Mhe. Rais Samia ni mtu wa huruma na nyie ni mashuhuda hatukua...

Wasira: Ujenzi Wa Reli Utafufua Uchumi, Kuneemesha Wakulima

Na MWANDISHI WETU  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kufufuliwa kwa Reli ya TAZARA, ujenzi wa reli ya kusini Mtwara -Mbamba bay) utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa mikoab ya Kusini na NyandA za Juu Kusini. Amesema ujenzi wa reli hizo ambao upo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030 na kuboreshwa kwa sekta ya kilkmo, kutasaidia kuleta ahueni kubwa ya kiuchumi kwa wakulima hususan wa mkoani Njombe. Wasira ameeleza hayo leo Septemba 15, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM kutoka kata 37 zilizo katika majimbo matatu ya Wilaya ya Njombe mkoni Njombe. "Kwa miaka mitano ijayo Rais Samia (Rais Dk. Samia Suluhu Hassan) amesaini mkataba na Zambia na China kufufua reli ya TAZARA ambayo inapita Makambako. Reli ya TAZARA itaunganisha maeneo haya na Uwanja wa Ndege wa Songwe na Bandari ya Dar es Salaam na ilikusudiwa hivyo tangu wakati wa Mwalimu Nyerere kwamba tupitishe hii reli kwa sababu kilimo hiki kitaleta mizigo ya kw...

Dkt.Nchimbi Aomba Wananchi Handeni Kuichagua Ccm Kwa Kura Nyingi Ili Ishinde Kwa Kishindo Uchaguzi Mkuu

MGOMBEA Urais mwenza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Dkt. Emmanuel  Nchimbi amewaomba wananchi wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga kukipigia kura Chama hicho ili kishinde kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025. Ametoa ombi hilo alipokuwa akihutubia maelfu ya Wananchi waliofika kumsikiliza,katika uwanja wa Kigoda leo Septemba 15, 2025 wilayani Handeni ambapo ameendelea na mikutano ya kampeni kuomba kura za mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassan,wabunge na madiwani. Dkt.Nchimbi ameanza siku yake ya kwanza  mkoani Tanga kufanya mikutano yake ya kampeni za  Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025,na mpaka sasa tayari ameshafanya mikutano yake ya kampeni ndani ya mikoa 11 mpaka sasa.

Kanali Mtambi Apongeza Ushirikiano Kati ya Tanzania na Kenya

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Mtambi ambaye alimwakilisha Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso katika kufunga Maadhimisho ya 14 ya Siku ya Mara akikagua mabanda ya Maonesho katika uwanja wa Mwenge mjini Butiama. Mhe. Mtambi amepongeza ushirikiano mzuri uliooneshwa kati ya Tanzania na Kenya katika kufanikisha maadhimisho hayo.  

Wanaomtukana Rais Samia ni Wahuni - Msama

Mkurugenzi Mkuu wa Msama Promesheni Ndugu, Alex Msama amempongeza Mgombea wa Urais Kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kampeni zake alizozifanya Ndani ya Mwezi Mmoja bila kupumnzika huku akisema ameonyesha ukakamavu wa hali ya juu. Akizungumza na Waandishi wa Habari Kinondoni Jijini Dar es Salaam Msama amesema Mapokezi makubwa waliomuonyesha Wananchi  Mikoani ni ishara yakuwa Atachaguliwa na kushinda kwa kishindo. Aidha Msama amewapa onyo wale wote wanaondelea kutoa lugha za matusi mitandaoni kuacha mara moja huku akiwasihi watanzania kuwapuuza watu hawa huku akidai wanatumika na mabeberu wasiokuwa na nia njema na Taifa la Tanzania huko nje ya nchi.

Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kupitia ACT Wazalendo awafariji Wafanyabiashara wa Soko la Kawe

Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe Jijini Dar es salaam kupitia Chama cha ACT Wazalendo Glory Tausi ametembelea Soko la Kawe lililoungua moto na kuteketeza kwa kiasi kikubwa bidhaa na mali za wafanyabiashara wa soko hilo.  Tausi amekutana na baadhi ya wafanyabiashara mmoja mmoja na kutoa pole za dhati kwa niaba ya wote walioathiriwa na tukio hilo la kusikitisha.  Mgombea huyo pia ametoa pole kwa Afisa Mtendaji wa kata ya kawe  Aidha amewaomba wakazi wote wa Kawe kushirikiana kwa pamoja katika kuwafariji na kuwasaidia wenzetu waliopoteza mali na riziki zao kufuatia tukio hilo.  "Kwa pamoja tukisimama tunaweza kuwasaidia waathirika kurejea kwenye shughuli zao na kuendelea kupambana kwa ajili ya maisha bora" Alisema Tausi Soko lililoteketea kwa moto halikuwa linatoa huduma kwa wakazi wa Kawe pekee, bali pia lilikuwa msingi wa kipato na riziki ya kila siku kwa wananchi na wafanyabiashara wa eneo hilo. "Hivyo, nipo pamoja nanyi kwa kila hatua wananchi wenzangu wa Kawe katika ki...