Skip to main content

Posts

Showing posts from September 29, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais wa mpito wa Burkina faso aimarisha upatikanaji wa huduma za afya maeneo ya vijijini

Rais wa mpito wa Burkina faso kapteni  Ibrahim Traoré amekabidhi magari kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwenye vijiji visivyokuwa na Hospitali. Magari hayo ambayo ni Hospitali zinazotembea yamekabidhiwa kwa wizara ya afya yakiwa na vifaa tiba vya kisasa pamoja na vitanda vya wagonjwa, Fridge za dawa, Mitungi ya gesi na Jenereta za Umeme.  Kapteni Traoré ambaye ameliongoza Taifa la Burkina faso tangu septemba 30 mwaka 2022 amekuwa akichukua hatua mbalimbali za kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya,elimu pamoja na usalama wa raia na Mali zao. Kiongozi huyo pia tayari amezifutia leseni za uchimbaji wa madini makampuni yote ya kigeni.  Amechukua hatua hiyo baada ya kubaini Taifa hilo halinufaiki na madini yanayochimbwa na makampuni ya kigeni ambapo kwa sasa shughuli za uchimbaji madini nchini humo zinafanywa na raia wa taifa hilo. 

Fahamu Ubunifu wa Majiko ya Solar Yenye Uwezo wa Kupika Chakula cha Wanafunzi Zaidi 600 Katika Shule Moja Nchini Tanzania

Na Emmanuel Chibasa 👉Ni teknolojia Yenye Kuleta Suluhisho ya Kupunguza Matumizi ya Kuni na Mkaa Katika Taasisi za Elimu 👉Inawezesha kupika ugali, Maharage,Makande pamoja na wali Kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wengi na wafanyakazi kwa haraka zaidi pamoja na kupunguza gharama za matumizi. Katika dunia ya leo, nishati ya umeme jua inachukua nafasi muhimu katika kukabiliana na changamoto za mazingira, kijamii na kiuchumi na taasisi za elimu zinapokua sehemu ya matumizi haya faida zake zinaonekana wazi. Matumizi ya nishati safi ya kupikia ni agenda mahususi ambayo imechukua nafasi kubwa katika Sera, Mipango na Mikakati ya Serikali mbalimbali duniani. Umuhimu wa agenda hii unasukumwa na ongezeko la uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na athari za kiafya zinazotokana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia. Umeme jua ni chanzo cha nishati kisichokua na uchafuzi wa mazingira, kwa kutumia paneli za jua, shule zinaweza kupata umeme kwa gharama nafuu kwa ajili ya ...

Uvccm yasema fomu ni moja tu ya urais 2025 kwa pande zote mbili za muungano

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa na Mlezi wa UVCCM Vyuo na Vyuo Vikuu  Mohammed Ali Kawaida ameweka bayana msimamo wa Umoja wa Vijana wa CCM ya kuwa ifikapo 2025 UVCCM itasimama na Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa Zanzibar na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Tanzania "Tunaona kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Serikali zote mbili, ifikapo 2025 Fomu ya Uraisi ni moja tu kwa Zanzibar ni Dkt Mwinyi na Bara ni Dkt Samia na katika hili hatutakuwa wanafiki tutasimama Imara kuyasema yote yaliyofanywa na Viongozi wetu" Kawaida ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Mahafali ya UVCCM Zanzibar yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Suza Tunguu Unguja Zanzibar tarehe 28 Septemba, 2024. Aidha Kawaida amewahimiza vijana wote nchini kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukisemea kwa wananchi wote ili kiendelee kuaminika kwa wananchi na kuendelea kushika Dola. 8 Umoja wa Vijana wa CCM utafanya kazi usiku na mchana kusema mazuri yote yanayofanywa na Serikali zote mbili za...