Skip to main content

Posts

Showing posts from September 3, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Balozi Dkt Nchimbi Aomba Kura Kwa Wananchi wa Mji Mdogo wa Isaka-kahama

 Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wakazi wa mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama, jimbo la Msalala,kwenye mkutano mdogo wa hadhara leo Alhamis Septemba 4,2025,mkoani Shinyanga. Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Msalala Mabula Johnson Magangila pamoja na Madiwani. Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.

Chauma Yamtangaza Kada wa Ccm Kuwa Mgombea Wake Bila Yeye Kuwa na Taarifa

 NINALAANI VIKALI UZUSHI NA UPOTOSHAJI HUU! Imeandikwa na Alex NINALAANI VIKALI UZUSHI NA UPOTOSHAJI HUU! Imeandikwa na Alex Msama Mwita. SHALOM!  BINAFSI, ni buheri wa afya njema. Hakika ninamshukuru mno Mungu wa Mbinguni, kwa kuendelea kunilinda, mimi na familia yangu, lakini zaidi sana kwa kuendelea kusimamia Amani na utulivu kwa nchi yangu niipendayo, Tanzania. Ninaendelea kumuomba Mungu azidi kusimama nasi, kama Watanzania katika kudumisha umoja, ushirikiano, mshikamano na undugu wetu, tuliorithishwa na waasisi wa Taifa letu. Ndugu zangu, saa chache zilizopita, kulisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, juu ya kile kinachotajwa kuwa orodha ya wagombea wa nafasi ya ubunge, katika majimbo mbalimbali hapa nchini, kupitia chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA). katika hali ya kushangaza, kushtusha, kuduwaza na kuacha maswali mengi, ni pale nilipoona jina langu, kuwa miongoni mwa wagombea hao wa ubunge, nikitajwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, Jimbo la Ukonga! Ndugu zangu, ...

Dk.Nchimbi Awaomba Wananchi Shinyanga Kumpigia Kura za Kishindo za Urais Dkt.Samia,Wabunge na Madiwani

MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewahutubia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba kumpigia kura za kishindo mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani. Dk.Nchimbi  ametoa ombi hilo leo Septemba 3,2025 alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara ambapo katika mkutano huo amewanadi  Wabunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi. Wengine ni  Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu, Lucy Mayenga , Jimbo la Solwa Ahmed na Itwangi na Azza Hillal pamoja na madiwani. Dkt. Nchimbi ameendelea kunadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo. Aidha amekuwa akitumia  nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hich...

Nchimbi Kutikisa. Mkoani Kagera Kuanzia Septemba 06

 Na Angela Sebastian Kagera  Katibu wa siasa,uenezi na mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera Amim Mohamud amesema, mgombea mwenza wa Urais,Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwasili mkoani Kagera Septemba sita mwaka huu kwa ajili ya kunadi sera,Ilani ya CCM 2025-2030 na kuomba kura. Mahmud amesema Dkt.Nchimbi atapokelewa Wilayani Biharamulo Septemba sita atahutubia wananchi katika eneo la Nyakanazi ambapo Septemba saba atafanya mikutano ya adhara katika Wilaya za Ngara,Kyerwa,Bukoba vijijini na mjini ambapo atahitimisha ziara yake.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ataka Sekta ya Sheria Kulinda Mazingira

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amewataka Wanasheria kuwa walinzi na kuongeza umakini katika kutoa ushauri wa sheria zinazohusu mazingira kwa maslahi ya taifa. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo tarehe 3 Septemba, 2025 wakati akifungua mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kuhusu sekta ya mazingira yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) Jijini Dodoma. Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema wanasheria hao wanatakiwa kuwa walinzi na kuongeza umakini katika kutoa ushauri wa sheria za mazingira kwa maslahi ya nchi. “Natambua zipo changamoto wakati wa utekelezaji ,mfano uelewa mdogo wa masuala ya mazingira hivyo tunawajibu wa kuzibadili changamoto hizi na kuzifanya fursa kwa kuimarisha nafasi ya NEMC katika kusimamia sheria katika sekta ya mazingira.”Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mhe. Johari amesema mafunzo hayo yatawasaidia Mawakili hao wa Serikali kuelewa vizuri sheria na taratibu zinazohusu usimamizi wa mazingira na kuf...

Doyo kuzindua kampeni za Urais Tanga

Na Mwandishi Wetu, Tanga MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, Septemba 4, 2025 atazindua kampeni zake za kugombea Urais katika viwanja vya Komesho Jijini Tanga. Katibu wa Chama hicho mkoani Tanga Boniface Gidion alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na viongozi wa Chama hicho ngazi ya kitaifa wakiongozwa na Mwenyekiti Mfaume Hamisi Hassan tayari wapo Jijini Tanga kwa ajili ya uzinduzi huo. Alisema Doyo ambaye licha ya kugombea Urais, pia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, ameongozana na mgombea mwenza, Chausiku Khatibu Mohamed. Katika hatua nyingine mgombea huyo wa Urais kupitia Chama hicho, amepokelewa kwa heshima ya kipekee na kufanyiwa dua maalum na wazee wa Kijiji cha Misima, Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga. Wazee wa kijiji hicho walijitokeza kwa wingi kumpokea Mhe. Doyo na kumfanyia dua za kumtakia kheri, baraka, na mafanikio katika safari yake ya kisiasa ya kuwania nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa Taifa. Akizungumza kwa nia...

Rais Samia Kutoa Taarifa Ya Tume Za Ngorongoro Baada Ya Uchaguzi Mkuu- Rc Makalla

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumanne Septemba 02, 2025 akiwa ziarani Wilayani Ngorongoro, amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuwa watulivu na kuendelea kudumisha amani na Mshikamano miongoni mwao, wakati wakisubiri majibu ya Tume mbili zilizoundwa na na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sale Kata ya Sale kwenye Mkutano wa hadhara, Mhe. Makalla amebainisha kuwa Busara, hekima na mapenzi ya Rais Samia kwa wananchi wa Ngorongoro, tayari Tume hizo zimekabidhi ripoti kwa Rais Samia na punde baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, hatma na maamuzi ya serikali yatatangazwa hadharani. "Niwaombe, tumesubiri muda wa kutosha, tumeipa tume muda wa kutosha, hatuwezi kushindwa kusubiri muda mdogo uliobaki tukapata majibu. Niwaombe Wazee na Viongozi wa mila wa Ngorongoro, tumahitaji hekima zenu, uongozi wenu utukubalie tumpe nafasi Mhe. Rais amalize uchaguzi na hili la kutangaza matokeo ya taarifa za Tume itakuwa moja ya kipaumbele...