Skip to main content

Posts

Showing posts from July 4, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

SERIKALI KUKAMILISHA MCHAKATO WA KUUNDA HALMASHAURI YA MWIBARA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itakamilisha mchakato wa kuunda Halmashauri ya Mwibara ili kusogeza huduma za Serikali karibu na wananchi na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za kijamii na maendeleo. Ametoa kauli hiyo leo Julai 4, 2026, alipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara, baada ya Mbunge wa Bunda Vijijini, Mhe. Boniface Mwita Getere, kuwasilisha ombi la wananchi la kuanzishwa kwa halmashauri hiyo. Waziri Mkuu alisema Serikali imepokea hoja hiyo na kutambua umuhimu wake, akibainisha kuwa utaratibu wa kuanzisha halmashauri mpya utaendelea kufuatwa ili kuhakikisha huduma za Serikali zinawafikia wananchi kwa ufanisi zaidi.  "Nimeipokea hoja hii. Serikali ina utaratibu unaofuatwa katika kugawa maeneo ya kiutawala. Nimemuelekeza Mkuu wa Mkoa pamoja na Sekretarieti ya Mkoa kuendelea na mchakato huo ili Serikali iweze kupeleka mapendekezo kwenye mamlaka husika kwa hatua zinazostahili," alisema Waziri Mkuu. ...

AGNES MARWA AWAPA TABASAMU WAJASIRIAMALI MARA KWA MIKOPO ISIYO NA RIBA

 MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Agnes Marwa, ameendelea kuwawezesha wajasiriamali wadogo kwa kuwasaidia kupata mikopo isiyo na riba ili kuwasaidia kukuza biashara zao na kujikwamua kiuchumi. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Agnes amesema ameamua kujitoa kwa kutumia sehemu ya mshahara wake kugharamia riba ya mikopo hiyo, ili kuwaondolea changamoto ya kukosa dhamana inayowakwamisha wajasiriamali wengi. Amesema hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia fursa mbalimbali za kifedha na uwezeshaji wa moja kwa moja. “Nimeamua kujinyima mimi na familia yangu ili kuhakikisha wajasiriamali hawa wanapata fursa ya kukua kiuchumi. Lengo langu ni kuona wanajenga biashara zao na kuboresha maisha yao,” amesema Mhe. Agnes Baadhi ya wajasiriamali walionufaika na mpango huo wamesema msaada huo umewapa fursa ya kupata mitaji ambayo awali ilikuwa vigumu kuipata kutokana na kukosa dhamana. Bibi Mango Ch...

PSSSF:"TUNALIPA JANA" YAENDELEA KULETA TABASAMU KWA WASTAAFU

 Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema utekelezaji wa kaulimbiu ya "Tunalipa Jana" umeendelea kuleta mafanikio makubwa, huku wastaafu wengi wakilipwa mafao yao kwa wakati mara tu baada ya kumaliza utumishi, mradi nyaraka zao zimekamilika na kuwasilishwa kwa wakati. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda la PSSSF katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo, amesema kaulimbiu hiyo, iliyoanzishwa Aprili mwaka huu, ni sehemu ya mkakati wa Mfuko wa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wanachama. Amesema PSSSF imejipanga kuhakikisha mwanachama anayeanza safari ya utumishi anakuwa na taarifa sahihi na zinazohuishwa mara kwa mara ili kufikia kipindi cha kustaafu asiwe na changamoto yoyote ya kupata mafao yake. "Dhamira yetu ni kuhakikisha mwanachama analipwa mafao yake siku ya kustaafu. Hiyo ndiyo tafsiri halisi ya kaulimbiu ya Tunalipa Jana. Tunat...

RIDHIWANI KIKWETE ASISITIZA KUIMARISHWA KWA UTUMISHI WA UMMA

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kina mchango mkubwa katika kuandaa watumishi wenye weledi, maadili na uwezo wa kutoa huduma bora kwa wananchi. Mhe. Ridhiwani amesema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi mbalimbali, wakuu wa zamani wa chuo, wadau wa maendeleo na taasisi zilizoshirikiana na chuo hicho walishiriki katika hafla hiyo. Amesema maadhimisho hayo yamekuwa fursa ya kutambua mchango wa watu binafsi na taasisi mbalimbali zilizosaidia kukijenga na kukiendeleza chuo hicho kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita. Katika hafla hiyo, vyeti na tuzo za shukrani zilitolewa kwa wahusika waliotoa mchango mkubwa katika mafanikio ya chuo. Aidha,Mhe. Ridhiwani amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika mafunzo na maendeleo...

UWT: WANAWAKE TUWE SEHEMU YA KUKATAA MAANDAMANO

 NA: MWANDISHI WETU, DODOMA Wito umetolewa kwa wanawake nchini kuwa sehemu ya hamasa ya kuelimisha jamii kuepuka uchochezi wa kufanya maandamano badala yake waitunze tunu ya amani iliyopo. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, Julai 3, 2026, Jijini Dodoma. Amesema, kama ambavyo ukimwelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima, hivyo mwanamke akisimama imara atakuwa sehemu ya kuepusha maandamano yanayoratibiwa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati, Julai 7. "Leo, nina ujumbe mahsusi kwa wanawake wenzangu. Nina wajibu wa kuongea na wanawake na wananchi kwa ujumla juu ya kutunza tunu ya amani tuliyonayo. Wanawake, hebu tukae chini na waume zetu, tuwaelimishe umuhimu wa amani na kuepuka maandamano". "Kimsingi, shughuli wanazofanya za kuingiza vipato ambavyo tunapata chakula na mahitaji muhimu ya watoto wetu wanaosoma shuleni na vyuoni hazitafanyika katikati ya vurugu na maandamano," amesema Chatanda. Aidha, Chatanda amese...

NDIVYO RAIS SAMIA ANAVYOSAKA FURSA KIMATAIFA UBORESHAJI AFYA MAMA NA MTOTO AFRIKA

 NA: DK. REUBENI LUMBAGALA  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anatambulika kimataifa katika nyanja mbalimbali kutokana na utendajikazi wake uliotukuka. Miongoni mwa maeneo yanayomtambulisha kwa upekee ni pamoja na kuwa Kinara wa Afya ya Uzazi ya Mama na Mtoto barani Afrika. Ni heshima ya kipekee aliyoipata kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanyika katika sekta ya afya, ambapo matunda yake yameonekana hasa katika kupungua kwa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua. Kwa wadhifa huu, Rais Dk. Samia anao wajibu wa kuhakikisha nchi zote 54 za barani Afrika na Tanzania ikiwemo, zinaendea kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kiwango kikubwa. Hii inatokana na ukweli kuwa, kundi la mama na mtoto ni wadau muhimu katika juhudi za maendeleo. Ni kundi ambalo linapaswa kuhakikishiwa usalama wa maisha na kamwe uzazi usio tishio la usalama wao. Juhudi za kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa sehemu kubwa zinahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali hasa katika kubadilishana uzoefu, teknolojia n...

WAZAZI SIKIENI USHAURI WA DK. BATILDA BURIANI JUU YA MALEZI YA WATOTO

 NA: DK. REUBENI LUMBAGALA  Malezi bora ya watoto yanapaswa kutiliwa mkazo ili kujenga jamii yenye watu wenye maadili, nidhamu, uzalendo na uwajibikaji katika maisha yao. Wazazi wamepata baraka ya kupata watoto kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Watoto hao wanapaswa kuendelea kuwa baraka kwa kuhakikisha wanapata malezi na matunzo muhimu. Katika miaka ya karibuni, kumekuwa na kulegalega malezi ya watoto. Baadhi ya wazazi na walezi ambao ndiyo wadau wa kwanza wa kusimamia malezi ya watoto wamekuwa walipambana na matunzo ya watoto huku wakisahau malezi yao. Wazazi na walezi wanahangaika kutafuta fedha za kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu kama vyakula, mavazi, mahitaji ya shule ili wafurahie maisha. Hili ni jambo zuri na la kupongezwa na kila mtu. Changamoto inayokuja ni pale wazazi na walezi wanapojitahidi kutoa matunzo na kusahau suala la malezi ambalo ni la muhimu sana. Julai 02, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Buriani alitoa somo zuri la malezi kwa wazazi na walezi....

SABASABA YAFUNGUA FURSA MPYA ZA MADINI, WAFANYABIASHARA WAKIRI UTAJIRI MKUBWA WA TANZANIA

 _Serikali yapongezwa kwa kuimarisha sekta ya madini, wawekezaji waendelea kuonesha imani kubwa_ 📍DAR ES SALAAM Wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini wameipongeza Serikali kwa kuendelea kuimarisha usimamizi wa sekta hiyo kupitia uwazi, utekelezaji wa sheria na matumizi ya mifumo rasmi ya biashara, hatua ambazo zimeongeza imani ya wawekezaji, ufanisi wa biashara na mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa Taifa. Pongezi hizo zimetolewa na mfanyabiashara mkubwa wa madini ya Tanzanite nchini, Taikoo Kulunju Oletipa, baada ya kutembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Taikoo amesema maboresho yanayotekelezwa na Serikali kupitia Tume ya Madini yameendelea kuboresha mazingira ya biashara, kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuongeza tija katika shughuli za madini. “Serikali kupitia Tume ya Madini imekuwa ikiwashirikisha na kuwasikiliza wadau wa sekta hii, ...

TPA YANG'ARA SABASABA, YAIBUKA NA TUZO YA UBORA WA HUDUMA

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeendelea kudhihirisha ubora wake katika utoaji wa huduma baada ya kuibuka mshindi wa tuzo maalumu kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo ilitolewa Julai 3, 2026 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa mgeni rasmi katika maonesho hayo, huku mgeni wa heshima akiwa Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Chapo. Kwa niaba ya TPA, tuzo hiyo ilipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Plasduce Mbossa. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Dkt. George Fasha, alisema mafanikio hayo yanatokana na uongozi imara wa Bodi ya Wakurugenzi, ushirikiano wa wafanyakazi pamoja na dhamira ya taasisi hiyo ya kuendelea kuboresha huduma kwa wateja. Amesema tuzo hiyo ni uthibitisho wa juhudi zinazoendelea kufanywa na TPA katika kuimarisha ufanisi wa huduma za bandari, kuonge...

WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU WANANCHI KUTOZWA FEDHA ZA MAFUTA KWENYE MAGARI YA WAGONJWA

 Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amepiga marufuku tabia ya kuwatoza wagonjwa fedha za mafuta wanapohitaji kusafirishwa kwa magari ya wagonjwa (ambulance), akisema kitendo hicho kinakiuka sheria, sera na maelekezo ya Serikali. Ametoa kauli hiyo leo Julai 4, 2026, alipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Suguti, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, ambapo aliwaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha hakuna mgonjwa anayekwamishwa kupata huduma za rufaa kwa kuombwa fedha za mafuta. "Ambulance ipo, mnamwambia mgonjwa achangie mafuta. Haya ni mambo yanayokiuka sheria, yanayokiuka sera na yanayokiuka maelekezo. Haya ni mambo yasiyokubalika," alisema Waziri Mkuu. Alisema Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa hospitali, ununuzi wa magari ya wagonjwa, ajira za wataalamu wa afya na kuboresha upatikanaji wa dawa, hivyo hakuna sababu ya wagonjwa kucheleweshwa kupata matibabu kwa kuombwa...