Skip to main content

Posts

Showing posts from November 6, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Jinsi Ukaushaji wa Dagaa Kwa Kutumia Solar Dryer Unavyosaidia Kukausha Dagaa Kwa Usalama, Muda Mfupi na Kwa Ubora Katika Mwalo wa Kayenze Ndogo Mwanza

  Na Emmanuel Chibasa Katika mwalo wa Kayenze ndogo, wilaya ya Ilemela, jijini Mwanza, wavuvi na wafanyabiashara wa dagaa sasa wanashuhudia mabadiliko makubwa kupitia teknolojia ya kisasa ya nishati ya jua, inayotumika kukausha dagaa. Mradi huu, unaoendeshwa na kampuni ya Millennium Engineers, umeleta matumaini mapya kwa sekta ya uvuvi kwa kuwawezesha wavuvi kukausha dagaa kwa ubora unaokidhi viwango vya soko la ndani na nje ya nchi. Kwa Nini Teknolojia Hii ni Muhimu? Teknolojia mpya ya ukaushaji dagaa kwa kutumia mitambo ya nishati ya jua ni muhimu kutokana na kutajwa kuwa suluhisho la kukabiliana na changamoto ya upotevu na uchakataji wa dagaa zenye ubora na hivyo kuongeza tija kwa wavuvi na wachuuzi katika ziwa victoria. Wavuvi na wafanyabiashara ya dagaa wanasema, Kabla ya mradi huo, wailikua wakianika dagaa kwenye mchanga au kwenye vichanja vya miti kando ya ziwa Victoria na njia hizi za jadi zilikuwa na changamoto kadhaa, zikiwemo kuathiri usafi wa dagaa, kuvutia ucha...

Jamii Yashauriwa Kutunza Mazingira Ili Kukabiliana na Mabadiriko ya Tabia Nchi

  Na Fesha Kinasa, Mara.  JAMII imeshauriwa kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira na uoto wa asili kwa kutenga maeneo ya  kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa na athari kwa viumbe hai.   Hayo yamesemwa Novemba 6, 2024, na Mdau wa Mazingira Robinson Wangaso wakati akikabidhi Miche ya miti 150 katika shule ya Secondary Salama  iliyopo Wilaya ya Bunda  Mkoani  mara. Wangaso amesema kuwa, ili kuhakikisha mazingira na  uoto wa asili unalindwa kwa manufaa endelevu ya Mwanadamu na viumbe hai.   Ni  jukumu la Wananchi  wote  kupanda miti na kuitunza vyema katika maeneo yao na kushiriki katika agenda ya serikali ya  kuifanya Tanzania iwe ya kijani.  Ameihimiza pia  Jamii kuzingatia matakwa ya serikali na Wadau wa Mazingira kwa kuachana na tabia zinazoathiri mazingira ikiwemo kukata miti ovyo, kuchoma mkaa na kulima maeneo ya vyanzo vya maji yaliyohifadhiwa kwani at...

Wananchi wa pongwe msungura watoa shukrani zao kwa Jwtz

Wakazi wa kijiji cha Pongwe Msungura kilichoko Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani wamelishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa msaada mkubwa wa vitu mbalimbali  vikiwemo vyakula vilivyotolewa kwa ajili ya watoto wao. Akizungumza kwa niaba ya  wazazi  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Pongwe Msungura Bw Joel Kajonga amesema JWTZ limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi na wanafunzi kijijini hapo. Naye Kamanda wa Kikosi cha 8 kinachokwenda kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Luteni Kanali Theofili Nguruwe amesema JWTZ ni jeshi la wananchi hivyo litaendelea kutoa msaada kila itakapowezekana. Msaada uliotolewa shuleni hapo ni mahindi kwa ajili ya chakula, maharagwe, sukari, madaftari, kalamu, viatu, mabegi vyote vikilenga kuongeza morari wa kusoma kwa wanafunzi. Mbali na msaada huo pia wataalam wa afya wa JWZT waliweza kutoa matibabu na elimu ya afya kwa wazazi wa kijiji hicho.

Mtanda;Mambo ya kukimbia na masanduku ya kura yamepitwa na wakat

  Mkuu wa Mkoa wa mwanza Said Mtanda amewahakikishia wananchi pamoja na wadau wa uchaguzi kuwa Mkoa huo umejipanga kuendesha uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye mazingira huru na haki na yanayozingatia sheria.  Mtanda amebainisha hayo katika kongamano la viongozi wa dini mkoani mwanza lililolenga kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo utakaofanyika November 27 mwaka huu.  Mtanda ametumia kikao hicho kilichoshirikisha kamati ya amani ya viongozi wa dini kusisitiza kuwa Mambo ya kukimbia na masanduku ya kura yamepitwa na wakati.  "Uchaguzi wa serikali za mitaa ni mchakato, hatuna mpango wa kumzuia mgombea yeyote kuchukua fomu,kila aliyejiandilisha atapata fursa ya kupiga kura,kura zitahesabiwa kwa uwazi na kushuhudiwa na wakala wa kila mgombea na matokeo halali ndio yatatangazwa" Alisema Mtanda na kuongeza kuwa "Kuhusu suala la amani,tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha uchaguzi unapita salama na hakuna anayeguswa kwa namna ye...

Mtanda ahimiza matumizi sahihi ya magari ya serikali

  Serikali imeipatia wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)Mkoa wa mwanza vitendea kazi ikiwemo magari manne pamoja na pikipiki nne ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa wakala huo. Vitendea kazi hivyo vimegharimu zaidi ya shilingi millioni mia nane na vimekabidhiwa kwa Ruwasa na Mkuu wa mkoa wa mwanza Said Mtanda ambaye amehimiza utunzaji wake pamoja na kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara. Mtanda amesema kuwa hatua hiyo itawezesha magari na pikipiki zilizotolewa kutoa huduma endelevu. ‘’Serikali ya Rais Samia inaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za maji nchini pamoja na kuongeza vitendea kazi na leo tumeona magari manne ya kisasa,kwa mfano haya yanakwenda sengerema na ukerewe,hizi pickup sijawahi kuziona kabisa na naamini kabisa meneja huko ukerewe atafurahi sana’’alisema Mtanda na kuongeza kuwa ‘’Magari ya serikali lazima yafanye kazi inayokusudiwa na pale tunapoona kwamba magari yale yamefika ukomo tufuate utaratibu wa wa kuyauza kwa watumishi wanaowe...