Skip to main content

Posts

Showing posts from March 5, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Kufanya Ziara Karatu na Monduli

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja mkoani Arusha katika Wilaya za Karatu na Monduli. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anategemea kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa  skimu za umwagiliaji katika Bonde la Eyasi, lililopo Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha. Pia, Mheshimwa Dkt. Mwigulu atafanya mikutano ya hadhara Karatu mjini pamoja na Mto wa Mbu Wilayani Monduli

Wadau wa Maendeleo na Vyama Vya Siasa Mkoani Mara Wampongeza Rais Samia Kwa Kutekeleza Ahadi Zake

Na Mwandishi wetu Jovina Massano ;Musoma. WADAU wa Maendeleo na vyama vya kisiasa mkoani Mara wampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa akiomba kura kwa  wananchi. Pongezi hizo zimetolewa katika kikao Cha Baraza la Ushauri la  mkoa(RCC) na wadau wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa  mara baada ya kupokea taarifa ya usajili wa Kaya zisizo na uwezo katika mpango wa Bima ya Afya kwa wote uliozinduliwa  Januari,23,2026. Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani hapa Kuhunga Patrick Msambichaka amesema katika mkoa huu Serikali tayari imewaripia wasio na uwezo wapatao 62,444 mpaka sasa wamekwisha fanya uhakiki na kusajili kaya zisizo na uwezo na kuwafikia wahitaji 17,205 katika kata zote za mkoa  sawa na asilimia 27.6. Katibu wa Jimbo wa chama Cha ACT Wazalendo Musoma mjini Abdalah Songe amesema Serikali imekuwa sikivu kwa wananchi wake mchakato huo ni mzuri na una manufaa kwa w...

Mpasuko Mkubwa Chadema, Zanzibar Yadai Haki

 Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kwa upande wa Zanzibar, Mh. Said Issa Mohammed amesema Kuwa lengo la kufungua shauri la mgawanyo wa mali za chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sikutaka kufutwa kwa chama kama wanachama wengine wanavyo dhania. Hayo amebainisha mapema hii leo, Machi 5, 2026, jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kutoa ufafanuzi wa mambo kadha kuhusu chanzo cha kufungua shauri la mgawanyo wa mali za chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), ambapo amesema chama cha hiko katika mwaka 2015-25 kilifanikiwa kupokea ruzuku ya kiasi kisichopungua cha shilingi milioni 117 kama pesa ya kuendeshe chama ambapo kwa upande wa Zanzibar kiasi cha milioni 2 tu ndicho kilipatiwa ambacho hakiendani na ghalama zauendeshaji wa chama kwa upande wa Zanzibar. Aidha mwenyekiti huyo mstaafu amesema kuwa hadi kufikia sasa chama cha (CHADEMA) kimehama katika jengo lake la makao mak...

EWURA Kanda ya Kaskazini Yawanoa Viongozi wa Wilaya ya Korogwe

  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kupitia Kanda ya Kaskazini, leo tarehe 5 Machi 2026 imetoa elimu kwa viongozi wa Wilaya ya Korogwe katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa GMCC. Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, George Mhina, alisema lengo ni kuwajengea viongozi uelewa kuhusu majukumu ya EWURA na maeneo inayoyadhibiti ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Katika semina hiyo, washiriki walipatiwa elimu kuhusu umuhimu wa uvunaji wa maji ya mvua, matumizi ya nishati safi ya kupikia, leseni za mafundi umeme, ujenzi wa vituo vya mafuta vijijini pamoja na namna ya kutatua migogoro katika sekta za maji na nishati. Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema amewasisitiza viongozi hao kuwa mabalozi wa elimu waliyoipata kwa kuhakikisha wanaifikisha kwa wananchi ili kuongeza uelewa na matumizi sahihi ya huduma za maji na nishati.

FCC Kusimamia Sheria Katika Kuwalinda Watumiaji wa Bidhaa Nchini

 DODOMA  SERIKALI kupitia Tume ya Ushindani FCC imewahakikishia watanzania kwamba itaendelea kusimamia kikamilifu Sheria ya Alama za Bidhaa ili kuwalinda watumiaji dhidi ya bidhaa zisizo salama au zisizo halisi, na hivyo kupunguza hasara za kiuchumi zinazotokana na udanganyifu.  Aidha, Kudhibiti bidhaa bandia kwa mujibu wa sheria kunachangia ukuaji wa uchumi.  Kauli hiyo imetoleo leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo na fursa kwa vijana. Amesema kusudio hilo la serikali ni kuzifanya Biashara halali zinabaki na mapato yao, jambo ambalo litapelekea kuchochea uwekezaji zaidi, kuongeza ajira, na kuendeleza ubunifu.  "Bidhaa bandia huzuia ushindani wa haki, kuathiri vibaya biashara halali, na kuhadaa watumiaji, hivyo kuunda uwanja usio sawa wa biashara". Amesema  "Jitihada za kuzuia bidhaa bandia zinaboresha sifa ya biashara kitaifa na k...